Saturday, February 18, 2012

MACHO YANAONA SAHIHI.



Ni wazi macho hutumika kwa kuangalia,kuona,kutazama yote yakiwa kama ni matendo yake,na hii yote inatokana na namna tofauti ambazo zimefikirika,na hata ukazifikia.macho ni moja kati ya viungo vya mwanadamu,NI macho!!

Pale mtu anapofahamu inapoelekea yeye mwenyewe katika nafsi yake kuwa na utambuzi na wakati mwingine unaweza usiwe wa kiujumla mtu wa kujielewa,unapoelekea ni mbali zaidi ya ulipotoka,ni kama pale umefika mahala  na kusahau yote uliyokuwa ukilalama nayo kwa mara ya mwanzo,yakiwa yale yamegeuka kuwa mazuri,na uzuri wake haujaja tu baada ya kuacha kulalama,bali ni pale uliposifia vizuri,maana unaweza kushukuru mungu kwa kufika bila kujua mahala unapoelekea,ulipo.tumshukuru mungu,tena kwa njia nyingine hazina waelekezaji…inahitaji nguvu kweli na uvumilivu ili kujua pia kuelekeza,si watakuja na wengine,wao ndiyo wakiwa hawajui kitu kabisaa,watatulilia pamoja na hata ukiwakataa utakuwa umezikataa nafsi zetu,maana ikiwa unakubari mifano hai isiyoonekana ,uangalie yasije timamu yasiyowezekana,yatatusumbua tu ingawa yanaonekana yasiyokuwa na ufahamu,tena hata kuwa na ubishi,wakiamini wao ndiyo wameishi,au tuone labda kama utasahau hata majina yetu maana ingali wote tungeitwa “SALUMU” ingelikuwa haina haja ya kuhukumu,labda ubaki ukituhumu ingawaje wanaonekana lakini ushaidi hautadumu,wanapoteza wao ili ieleweke wanayoitaka,maana ndiyo chaguzi pekee litakalo baki.na hii pekee usizani kwamba ni ya kwao tu hata kwako pia,yaani yangu ndiyo itabaki.maana kila mtu ataona ya kwake.

Yaliyopo yametoka mahala,yaliyopo sijui yametoka wapi,kwani nasema hivyo ya kuwa siyo yote mwanadamu akayafahamu,mengine yapo katika miliki na uwezo wa watu wengine,na endapo ukikubariana na hili basi lazima ujue kwamba lile au yale uliyoyashindwa ndiyo yetu,maana yangelikuwa si yetu usingeyafanya,au useme kweli sio yetu basi uangalie mara ya pili,maana wakati unavyosema si vile unavyomaanisha,ikiwezekana ujue wakati ni mwanadamu mwenyewe,kama kijana wa kiume akaota ndevu na asinyoe huo utakuwa ni wakati wake,amemaanika hivyo.na hata ikawe siyo mara ya pili ila ni tendo lililoonekana,maana kama tendo linaloeleweka ni litatimia kwa kitendo ni lazima ujue chanzo,ili  yakija mafuriko usilalame,maana ulijua yatakuja na kutuzomba,tena kwa walio mbali wafahamu..MAFURIKO!!.shida za kuonekana hazipaswi kumwinua  na kumtuma mwanadamu,anayeona na kutenda katika utatuzi ni mwana adamu mwenyewe,isifike kipindi ukalazimishwa kuishi,tena ikawe ni amri kwamba sasa ni “LAZIMA” ,ingawa usipoitumia lugha hii katika mambo yetu utashika mitutu,watoto wataona baba zao wanachokifanya na kwa sababu wao wamekuja kujifunza,wamekuja kukua,wamekuja ili wawe wakaitwe watu wazima na wakajue,watashika mitutu yenye technolojia ya kizazi chao,hapo vita itakuwa haina heshima..watoto wataonekana wakubwa,na kwa wakubwa labda uwasikilizie,ingawa wanasema vita haina baba. 

Tunapoelekea hakutazamwi mtu ukaambiwa ona,sio kwa macho.unapoelekea ni mbali lakini si kama kule ukasema ulipotoka,kwani wengine watasema ni karibu kutokana na maisha yao kiujumla,unapoelekea ndiyo kwa mungu.tunapokaribishana majumbani mwetu tunategemea HODI,kama kuna mgeni ataingia bila hodi huyo atakuwa mwenyeji sema ni sababu ya mgeni aliyetangulia hakumkuta mara ya kwanza.

 UKITAKA KUJUA NI LAZIMA KUJUA UMEJUAJE?

By:        Benson G.Makaya,
Tel:     +255714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...