Saturday, August 18, 2012

VYOMBO..


Vingine vikiwa vinaleta habari na vengine vikiwa na kutumika kutokana na matumizi yake,hata habari ni matumizi maana imetumika kupitia hivyo,ikiwa kuna waheshimiwa wanahaki ya kuonekana katika vyombo hivyo,ikiwa ni majanga ama iwe ni namna yoyote ya kumtaka mwanadamu aweze kupata ufahamu,ufahamu ni jambo jema sana na kwa Yule anayefahamishwa ameelewa,maana ni lazima uelewe hata ya kuwa haukupanga kuelewa,hizi ni bidhaa,kuanzia pale inapoanzwa kutengenezwa mpaka inapofika,bidhaa mara nyingine huwa zinamtindo wa kuchacha na baadaye kuharibika ikiwa ni mwisho wa matumizi ya bidhaa hiyo,ni haki lakini ni dhahma kwa lile linaloendelea na kutaka faida wakati bidhaa kiujumla zimechacha,tutaharibiana matumbo hata kama ni wazi tuna njaa ya siku tatu.hazipaswi nyingine kukaa katika vyombo vya habari.

Leo utasikia waziri kafanya hili na kesho tusisikie nabii kafanya nini,hili linaashiria kutokufanya kwamba,haimaanishi watu wanakwepa majukumu yao ama vile ilivyo kwa upendeleo,hii ni namna ya vyombo vilivyoelekezwa ni vipi viweze kubeba chakula,maji,maono na masomo,pengine ikiwa kama abiria katika usafiri,na kama itatokea ajari basi hapa ndiyo tutaizungumzia yaliyojiri,vyombo vikiwa na mlengo zaidi wa mwenye chombo kuliko Yule anayeuziwa bidhaa,ama  kweli hii ni biashara,ingawa haina maana ya kushangaa,pengine ikiwa mambo ni baadhi ya yaliyopo katika chombo kilichotubeba.

Dunia ikiwa kama ni chombo mahususi ambacho kimsingi tumeweza kuwa humo,kama kutumika mpaka tunaisha,mara nyingi vyombo ni vile tunavyokuwa navyo ama tunavyoviacha baada ya sisi kuwa na hitaji la namna nyingine,pengine ikiwa .pengine tuangalie kile tunachokiweka katika chombo ali mradi kikakaa vyema,pengine hata jamii ikaelewa kama sio kueleweshwa,maana kwa vyombo vingine hata kama vimejaa watu wanapanda tu,bila kujua chombo chenyewe hakisemi,vingine hivi tunavyowaandika watu ili taarifa ziwafikie zisiwe kumchafua ali mradi ukauza,maana hao wanaochafuka wakiamua kuchafua kweli inawezekana kukosa hata mahala pa kuziweka bidhaa,ama na wao wauze hata  bidhaa zikawa hakuna.abiria jichunge..mizigo haibebwi.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...