Wednesday, November 14, 2012

DUNIA YA FURAHA..


Katika malengo yanayomfanya mwanadamu kuweza kuishi pengine ikiwa ni kwa muda fulani ama ki namna ilivyo kwa mtu akataka furaha iliyoje ndani ya maisha yake,na ikiwa mwanadamu unaishi na hutaki furaha kuna ulazima wa kuonekana kutokukamilika,kwani hata mahitaji pengine yasiwe yako,ikiwa tunapokutana tunafundi shana,leo ikaja zamu yako kwa kutokueleweshana na kesho akaja  mwanafunzi ili kumuelekeza,furaha haipimwi na mizani labda wanene wakawa na roho kubwa,ingawa maisha yako ni kile unachokifanya,kile kinachoonekana katika biashara yako,kazi zako ndiyo mtazamo wa maisha yako.

Unaweza kuwa na maana kubwa katika lile ulifanyalo,ikiwa hakuna kile kinachoweza kukamalika bila kujitoa/nguvu,kutoa nguvu inapasa kufanya kila mara,ikiwa kama mazoezi,mtu akaogopa kufanya lile lake kwa kuhofia mengine kwani unaweza ukawa unaishi maisha ya mwenzako,kila mshindi hushinda kwa kuonyesha njia,kila mshindwa hushindwa kwakuonyesha njia pengine ile ile,kila mtu anawakilisha zawadi ile aliyopewa na mwenyezi mungu,kwa kupita katika  majaribu,kulia,kucheka ,kuchekesha hata kunyamazisha,hayo yote yakiwa  ni madhumuni ya maisha yako,kusaidia watu na kusaidiwa hii ieleweke kuwa  ndiyo njia ya kupumua,ni njia ya kufikiri..njia ya kuishi,maana bila hivyo haikuwa na maana ya kuishi katika dunia ya furaha.

Inapasa kujua wapi ulipo katika maisha yako,furaha yako umeibeba mwenyewe,kila mtu anapaswa kufanya jambo ambalo kimsingi litapelekea mapenzi,na hii ikiwa inatupasa kuwapenda hata maadui zetu,unaweza usimchukie mtu lakini yeye akakuchukia,ikiwa kuna watu ndiyo wametufikisha hapa tulipo,kwa mapenzi ama uadui,maisha hayana uadui,wewe ndiyo adui wa maisha yako,wewe ndiyo mbaya wa maisha yako,kinachobadilisha mabaya kuwa mazuri ni matumizi na  muda wake,ikiwa kama mvumilivu hula mbivu,na siye vumilia si kwamba atakula mbichi,maana na furaha haipimwi kwa kilo.

No comments:

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO : Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha...