Sunday, January 29, 2012

HITAJI,,


Hitaji huwa linatokana na mtu mwenyewe,nafsi yake na mapendeleo ya kwake.Pale mtu anapohitaji liwe la ulazima ama si la ulazima katika mazingira yaliyo au yatakayo ya ulazima ikiwa na maana ya uwekezaji,yale ya hasara hakuna asiyeyapata labda tusikitike kwa kupoteza watu kwenda kuwa wafu na isiwe hasara,hiyo mitazamo inatokana na kile kilichomo kichwani na sio mwilini,maamuzi yanatokana na mtu pamoja na nguvu zake,pale nguvu zinapotumika tunaweza kusema maamuzi yalichukulika mahala Fulani,Ni wengi wetu tunaohitaji,hii haitokani na kwamba mahitaji ni ya lazima,mahitaji mengine ni yale yanayotupelekea kuhitaji.kuna kipindi mwanadamu hutenda katika mahitaji yake,hii inaweza ikawa ni kwa ulazima au ombi ikiwa mahitaji yako yamekulenga wewe mwenyewe.

Bidhaa zinapouzwa zinataka bei,ikiwa unahisi kulaliwa bei..usiuze,kwani yaweza kuwa matokeo unayoyahitaji siyo yenyewe.Isiwe lazima kumfanyia mtu mahitaji yasiyo kuwa na ulazima kwako.Kwa makusudi yapi sasa?pengine tunawaza tukiingojea samahani au itakuwa ndiyo mahitaji ya kutumia nguvu,maana lugha nyingine hutumika kurahisishia mambo,zikiwa pamoja na samahani,wachache tukatumia lugha hizo tukijua bado tunamahitaji mengi ndani yetu,pengine ikiwamo misemo hiyo tofauti inaendana na thamani ya kitu,tumekuwa wajanja saana katika kufanya mambo yetu,na hii inatupelekea mahitaji yetu kuwa ya kijanja janja tu,hatutafika mahala endapo tutahitaji kijanja,kwani tutapata kijanja hivyo ilivyo.

Pengine wengine hubaki pale jambo linapotokea,sio kukaa na kuwa nyuma bali kufikiri vyema mahitaji yao,ikiwa ni wao ndio wanataka kufanikiwa,mara nyingine tunapokuwa safarini tuwafikirie na wengine maana wao wamebaki huko,hatuna haki ya kupaita ni nyuma kwani kila mtu anahitaji lake,na ikiwa mlengwa amekuwa na malengo halisia.tusiseme tuna shida wakati wenye nazo wametulia,maana wao sijui ndiyo wamezizoea au ni mahitaji kama ilivyo kwa uhalisia,na tunaposema hitaji hilo linaweza likawa ni la mtu basi tusifikirie vibaya kwani iliyo nyeupe kwa mmoja si impendezayo mweusi anayependa hiyo,ni kama vile uongozi,ikawe pale tukajua ni nini maana ya uongozi na sio tukaenda na bado tukazidi tukidhania lengo letu,hapa watu watatushaangaa sana,ingawa uchache ndiyo uhalisi wa hitaji,vile vingi vinatafutwa baada ya kuona utamu,utamu wa jambo na wenyewe huja baada ya kutaka kuwa na miliki,tunapomiliki vitu vingine vinaweza visiwe katika mahitaji yetu,vingine vikawe kama ni mwongozo katika mahitaji yetu,Yule anayetaka kuyajua ni lazima akubari ,tena ikiwa kwa maelezo maana ujanja unaweza kuingia pia.

Pengine tuseme hakuna anayetaka kutangulia,na hili tusiliite hitaji,maana tumefanya kwa ulazima,kwa wale wanaojinyonga waliamua,hawakuonja kifo lakini walipaswa maana lilikuwa ni hitaji kwa muda huo,haina budi kushangaa kilichocheupe na wakati ni cheusi tukitafutacho nacho hatuna,labda tufikiri kabla ya matendo,matendo yetu yakatupelekee kuwa watu wenye mahitaji mazuri,kwa Yule anayelenga ni lazima apate na kama asipopata atakuwa amelengaje?labda tuseme lengo la mlengwa halikulenga malengo,matokeo ndiyo malengo ya mahitaji,katika kufeli hakuna kufauru ila tunaweza jitahidi zaidi tukafauru,hivyo basi tunaweza kufanikiwa kwa jambo lolote ikiwa tu tumelenga na kuwa na hitaji nalo.pengine imefika wakati tuyatangaze,maana wachache wameanza kununua,ingekuwa ni kuhama tungeshafika huko,au tukaupande ili uishe ikiwa ule ulio bora kabisa tusipewe ruksa,mambo ya msingi ndiyo haya yanayotupita kwa kusikia hata,kwani ikiwa kumbukumbu zimejaa na tusisahau pale hitaji linapofikia turudi tena tusimame kihisia pia,kwani walioweza walianza hawakuhusika ya kuwa kila mtu ana lake hitaji.

By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...