Kuna ulazima wa kuchagua wewe ni nani ikiwa unataka
kukamilika,pengine ukiwa na malengo,mipango yako iliyokamilika na ikitakikana
kufanyika ama imeshafanyika na wanadamu kuona namna ya vile ilivyotendeka ikiwa
wao ndiyo huleta makamilifu ya sifa,chako ni chako,kichafu na kisafi ni vyote
vilivyo kamilika ikiwa ni katika namna inayotakiwa,kwani pale anapopenda mmoja
mwengine anaweza penda hapo ilipo ya kuwa ni katika kukamilisha matokeo.
Mabaya huwa ni mazuri kwa kuwa yameweza kuwa na uwezo wa kuwa
mabaya .kukamilika ni namna ya kitu kilivyo,na endapo hakijakamilika ni lazima
kupeana namna ili inapokuwa inataka kukamilika iweze kukamilika katika namna na
maana ya vile ilivyo.pengine ni utofauti unaofanya mtu asiwe na
ukamilifu,akiamini yeye ndiyo yeye,kwa kuweza jambo na wengine
kushindwa.hayajawa mashindano maana hata muda wa mchezo wenyewe unapangwa
na wewe mwenyewe.
Maisha yanajengengeka na namna ya ukamilifu wako,ikiwa
haujatimiza jambo na unahisi ya kwamba si mkamilifu basi jaribu kukamilika kwa
kuweka kile unachokihitaji kukifanya kuwa kama ni baba au mama maana hakuna
pengine pa kuwapata,si ndiyo ikawe fulani ni mtoto wa fulani na fulani,si vile
ikawa haieleweki kwa kutokukamilisha
uzazi,na ki ubainadamu wengi hupenda kujikamilisha na kutokukamilisha ya
wengine.wakijua yao yamekamilika.