Sunday, July 22, 2012

DANGANYA TOTO

Kweli ikifahamika kweli itaumiza,maana wakubwa wamekuwa kama watoto,na watoto wanashindwa kuelewa maana wakubwa wamedanganywa na vile walivyotakiwa kudanganyia watoto ni mchanganyiko maisha magumu mtu anajiuza nafsi kwa kidogo kitu ni chakula ndiyo tena ukibisha sana utanunua hata kavu.siku hizi si kwa wanawake tu ndiyo maana hata ikaruhusiwa ndoa za jinsia flani,maana hata hawa hawa wanaume wananunuliwa na hii sielewi sijui ikiwa kununua na kuuza ni tofauti?maana Yule anayenunua danganya toto ili akadanganye toto naye kadanganywa na muuzaji,hapo baada ya kugundua mtoto amedanganganywa kweli..

Leo tunataka barabara ili tuendeshe magari yetu pale sebureni,watoto wakijinadi kwa wazazi si kuna yale magali ya ramani?samahani watoto wenzangu wa uswahili haya yanafuata yalipoelekezwa,pengine yalikuwa machafu basi yanaenda mtoni kuoshwa,na ikiwezekana huyo muoshaji anayehitaji atapata na mengine bure,ila lazima atie saini,sasa umepewa au mumebadilishana?maana watu wanakaa vyuo miaka saba mnataka muwashibishe na makaratasi..?hakuna mtu anayependa kula cha mwenzake,ndiyo maana kila mtu ana kwake,vile vya kwake kula na watoto wake,ili wasidanganyike..

Nani huyo asiyedanganyika maana wanaodanganya wanajua,kwani ile huwa ni tabia,pengine atakaa pembeni na kujifikiria baada ya kujua ukweli,pengine inauma sana ukifikiria ulipodanganywa kitoto toto,achana na hilo imakuwaje taifa zima kudanganyika?maana hapa bila kujua matokeo ya kile tunachokishangilia,tutakufa sisi na kubaki wao,tunaweza kukubali kudanganyika kwa kusema ni ‘Shida’bila ya kujua hata kama ulizaliwa kwa shida,kama kuna mtu alizaliwa kwa raha basi huyo ndiyo anawapa shida wengine..

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...