Monday, July 23, 2012

DARASA HURU....


Hapa unasema tu,sio unasema sema tu ili mradi umesema maana watakwambia umesikia wapi?hawa sio wapelelezi ni wambeya tu wa mitaani,leo atakuja na lake la kusema basi faraja kubwa kwa dunia kwa kudhani na lake litakuwa limechangia kuizungusha dunia,ni mengi san ya kuongeleka ndani ya darasa huru maana humu tutasema mbona ulisusa ukaja,siku hizi kuna masomo na ukiona hutaki katika  zetu za kihuni huni wanakutupilia mbali,sijui ndiyo kifo.maduka yameongezeka ikiwa na maana kodi imeongezeka pia,kuna jamaa wanalia sukari bei imepanda sasa mnatakaje,familia za watu zi sile? 

Darasa huru uwe mvumilivu maana hakuna viboko humoo..hakuna fimbo wala sio mwili kwa kuukaribia,ni vipigo tu vya hapa na pale,maana katika maisha tunakubali hivyo vingine vipo tena vingine vinaumiza sana hata usiwe na raha maishani mwako navyo hivyo vimo ndani ya darasa huru,maana huwezi kufundishwa kuvua na wakatI hauwezi kuvua,utafika wakati tunataka tunasema leo nimeenda mjini nimekosa hela,sasa kwa nini,maana ilipaswa kwanza,haya katika darasa huru yanapatikana endapo wakati unaruhusu hasa ukiwa unataka kusikia mwalimu anakwambia nini,labdda mwalimu hakutaka wanafunzi wajue’moja jumlisha moja ni mbili’pengine kama kuna mwingine  anafikiria ukijumlisha moja nyingine ndiyo tatu,sasa hapa kuna wale walioishia kuelewa 1+1=2,1+1+1=3,na wasioelewa 1+1=2,hapa naona wengine wameelewa namba..kweli tumetofautiana kuelewa..darasa huru litakuwa ni gumu sana..wanavyotutishia hao waliomo..!!..imesemeka..

Ngoja nimalize kidogo kwahelini maana nmeandika na kazi za nyumbani yaani ‘home work’..wahaya ni watani zangu hilo neno linawezekana kuwa la kwanza kuonekana,nilisikia mmesoma sana sasa ‘home work tu mnashindwa kuzimaliza?’..au ndiyo mnamalizia kuoga..’mshachelewa nyinyi watu wao walishakwenda’..hapo sura ikiwa na furaha kama vile ukicheza mziki wa chakacha,hata tukiwapeleka madarasani bado kwani ni kama wanacheza tu..

KAMPUNI.


Maana wao wananunulika tu,hiyo ikiwa ni kama bidhaa,tena kwa noti mbili zenye thamani moja,hii kweli ni kioja..tufanye noti moja ikawa mfano wa kununulia bidhaa moja na tena ikaja noti nyingine na namna ile ilivyo na biashara kufanyika hapo tunasema kuna uharamu,tena uharamu mkubwa sana bila kugundua maana nitapenda kuelewa wageni wanapokuja kuingia kwenye kampuni mnatoa zipi,zile za kwanza ama hizi zilizofuata,maana pengine zikija za tatu tusiwe na mashaka na za pili,maana za kwanza si zilikuwepo.

Leo ndugu zangu makampuni yanaongezeka,watu wanauza watu na sio mali,maana kama hautataka kufanya kazi katika kiwango cha chini basi kafe njaa,wewe bisha kesho ikutokee maana usiiombee..kesho watoto wetu watakuja na hasira sana maana hata tukishindwa kuwa na kampuni,nchi imegeuka kuwa kampuni,ya nini nishindwe kuwa na nchi yangu,pengine ni wewe,pengine ni mimi  endapo tunakubali ,nina mengi sana kuhusiana na hapa na kama kuna mahala zilibaki basi na sisi tugawieni,maana mbona zipo nusu nusu..au mnasemaje wateja? 

Hapa ni mengi tu jamani mmeyamezea,sijui ni baba zenu wamewaambiaa?maana bora hapa vile viboko vya mchungwa,pale mchungaji anapokuwa hajui kuchunga..haya yamekuwa mateke ya kuambiwa’aya pangeni mstari..kila mmoja anakuja hapa anapigwa teke la tumbo moja moja anaenda zake kulala'..hapa kila mtu angebaki nyumbani kwake ‘kura’ ampigie nani?ndugu zangu muda huu wanosikia wachache sana,ila itakuja kueleweka,maana  hayo yatakuwa ya ‘kodi’ itabidi tuyamalizie ndani ya kampuni..

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...