Navutiwa na kuona watu wanafuraha maana ni furaha kwangu
pia,inanivutia kuona watanzania wameamka na kuacha kulalama,inavutia kweli kwa
kuona yale magumu angalau watu wameanza kuyafanya,hapo hata kama hayawezekani
lakini kuna imani na tumai ya kuliweza japo moja,hii ni kwakuwa tumeweza kukua
katika upande fulani wa maendeleo,ikiwa pamoja na vizazi kuongezeka.
Pengine inavutia sana kwa kuona watu wakijishugulisha kwa
vile maisha ni magumu,maana ingalikuwa ni kula tu isingelikuwa na maana ya
kuvutiwa na majengo na mambo ya mjini,ingawaje tunasema mjini kuna upatikanaji
wa mahitaji kiujumla na zaidi ni haki tumevutiwa na vitu hivyo,pengine tunataka
tuwe nani lazima tufanye vile vinavyotuvutia,labda ikija badaye vitarudisha fadhila
ikiwa na sisi tutavutia.
Unapofanya yale ya kwako ni kufanya ngazi nyingine katika
kupanda maisha yako,tunaposema maisha ni yako ya maana ukifa leo wengine
watabaki ikiwa walivutiwa tofauti,ingawa ni vigumu sana kwa mwanadamu kusema
kile kinachomvutia kabla ya kufanya,pengine wengine wataogopa,wakisema mbona ya
kwako hukusema,haihitaji nguvu katika kuonyesha kile mtu unachopendezwa nacho
ni akili na msimamo ya kuwa ni wazi kufanyika.