Poleni watanzania,wabishi na mimi nimo..!!maana kwa misiba mingi kufikia,pengine
wengine wanasema mungu ametoa na mungu ametwaa vile tukafarijiane majumbani
kwetu,muda huu huu wengine tumechelewa kufika eneo la tukio japo tukarusha
kamba kuwaokoa wachache pengine ilitakiwa kutokuruhusu leo na kuwa kesho lakini
ndiyo imetokea,haya ni majonzi yetu,hapa tunastahiki kushtuka,maana si kwa
kutokuwa kawaida bali kuwa tumeuweka uongozi pembeni na kuweka ubinadamu,maana
fikiri unaambiwa mtoto wako yupo humo,pengine je wewe ungekuwemo humo?haya ni
kiimani zaidi,haya ni ya mungu.
Tusife moyo kwani japo tunarekebishana kidogo,tukumbuke
hiace zote zimeacha kutembea mijini na sijui ni kwa sababu ya udogo,ajali ama
foleni,pengine bahari imekuwa na mabonde,na madeleva wameshindwa kuendesha
kwani walizoea tambarale,pengine ni wazi inahitaji kuvichunguza vyombo
vyetu,maana ndiyo tulivyonavyo na kama watu ni wengi inapaswa kuwabeba ikiwa
watu hao wanashughuri za kimaendeleo pande ya pili
Zanzibar ni kwetu ndiyo maana tuliungana,kama ingekuwepo
sasa ni mimi na wewe,katika muungano kuna mengi humo,mwisho tunapata
undugu,kutoka dare s salaam mpaka Zanzibar sio mbali kwa ndege lakini tumezoea
meli,na boti huu ni usafiri unaotukidhi na maisha yetu,hivyo tunahaki ya kuwa
makini na vyombo tulivyonavyo,ikiwa kama vinataka kuzeeka basi tunavifanya
virudi katika ujana kwa maana kikizeeka sana hatuna budi kununua vipya,poleni sana
ndugu zangu,poleni sana watanzania wenzangu..
Mungu alaze roho za marehemu pema..!!