Nikisema iilkuwa wakati wa matumizi nitadanganya umma,ila
kama sikuweza kusikia basi kushuhudia baadhi ya matukio ya kipindi icho,vijana
wa kisasa wanasema wanakumbuka enzi zao,enzi ni nyuma na ujenzi,maana
inawezekana enzi zikawa ni nzuri kuliko ujenzi,unaweza kujenga kile usichikitegemea
na bila kujua utachanganyikiwa kwa kuporomoka hadi kujikuta huna maana
kabisa..kile kinachopoteza hata thamani ya kukopeshwa hicho kitabaki na maana
pekee,pengine ikiwa wanaotumia hawana maana pia,bora kuwa hauna maana kuliko
kufanyishwa hauna maana.
Wengine watasema naleta vita kwani wao wameshazoea kama
miaka ile ya 75,unajua ili kubadilisha namna ya kukaa ni kumweka adui
pembeni,dawa ya adui hakuna asiyeijua kama siyo aibu za kuoneana rangi,ikiwa
moja imependeza na nyingine imeiva,zote nzuri tuangalie wasije badilisha mpaka
zikawa sita maana kila kijiji itabidi kitumie pesa zake,tena karatasi za kuingilia na kutoka’ zikae sawa
maana mda si mrefu adui anaiporomosha thamani.
Nimebaki na maswali mawili matatu yanayonishusha
thamani,pengine kujumlisha ni kutoa,maana ikiwa kukuwa kwa mgomba
ni kukomaa lazima tuangalie na virutubisho,unaweza kukua mwili tu..leo
ukajibadilisha rangi hii,kesho ukaona upendeze na nani na fulani…yote yako
hayo,kama unazo zaidi ya moja zenye thamani moja mpe hata wa jirani ya mbali ya
nchi nyingine pengine zinaweza kupanda thamani zikiwa huko maana nabii hasifiki
kwao.