Thursday, October 18, 2012

BAADA YA HABARI....



Huwa yanakuwa mazungumzo kwa kuwa aliyeleta habari alidai kumaliza kutoa maelekezo,leo ukiwa unazungumza kwa kutaka kuhadithia habari bila kujua hiyo ndiyo habari yenyewe,pengine ikawa ni taarifa kwa kuwa habari yenyewe ni kama muhtasari,ukijaribu kuonja ni vigumu kuondoa ladha tumboni,labda isingetangulia taarifa basi hakika ingekuja habari kamili ingawaje imeonekana hakuna aliyesikiliza habari kwani baada ya habari kuisha mazungumzo yanaweza yasiendane na habari.


Haki sawa kwa kila mwanajamii,haki si sawa kwa mtoto na mkubwa,labda iwe umesikiliza tofauti na kuona mageuzi katika kichwa cha habari,lakini mazungungumzo yaliyofika baada ya habari yameonekana ni habari yenyewe.mengine hayapaswi kuyazungumzia humu maana wengi wao wamekuja kwa kasi wakitaka japo kuelewa kichwa cha habari lakini wameonekana wataelewa habari yote ikiwa bado umri hauruhusu.


Msomaji wa habari anapaswa kuwa kama daktari,maana kuna mengine yametukia sasa hivi,kuna mgonjwa ameingia wodini baada ya daktari kumaliza muda wake wa kazi,muda mwingine ni wa ziada,muda baada ya kazi..ukifanya kazi muda baada ya kazi bado huitwa ni kazi lakini unakuwa umejitahidi kwa kuzidisha muda,pengine ndiyo huwa ni kazi nzuri zaidi,pengine huwa ni taarifa nzuri zaidi..ikiwa mtangazaji kamaliza habari labda atuletee mazungumzo ili ijulikane baada ya habari nini kifuate ama kilifuata.

NAFASI YANGU ILIPO.


Kama nikianza na kupanga mstari kwa kuwa ni foleni baadaye ntajikuta nipo pale pale tu ikiwa kuna uvumilivu wa kile kilichotakiwa kufanyika maana kwa muda kumepelekea machache kusemeka na kuonekana ni bora , bila mshangao imehitajika kitu cha kunyooshea ili kuunyosha mstari angalau wa pili naye akafuatia humo humo, maana kwa kawaida ya foleni wengine watataka kutanua ikiwa wana uchukuzi wa nafasi ndogo wakizifuata njia ama nia.

Jaribu kuamini kama unapopita mguu wa kushoto na wa kulia unapita humo, pengine yasiwe madharau kwa waliojisahau maana hawakupaswa kupita huko ulipopita zaidi ya kujua umepitaje, ukiwa mwalimu,ukiwa mwanafunzi maana hawa watu wanahitaji kurandana, ingawaje siyo lazima sana kwani nafasi nyingine wanapaswa kupewa wasiojiweza.

Lugha hii ikichanganywa na nyengine unapata wengine tofauti maana utakuja wakati na kusema umejileta ,kwa kuwa kile kilichoonekana sasa hivi yapasa kujua ndani yake kuna nini Kama vile leo inavyokuwa ni mkopo na kesho ni siku ya kulipa deni lakini unaweza kwenda ‘tena’ baada ya kusamehewa deni na zaidi  kukopa tena, madeni yanapokuwa mengi unajileta na kujisogeza kwenye mtego wa kuichanganya nafasi yako kuchanganyana na ya kule usiyoyategemea.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...