Unaweza kusema unataka kushika na wakati bado hujashika, ikiondoka dhana ya kwamba haujui, pengine kisifuatwe kile ambacho Yule mmoja akasema,maana ushauri unapatikana kwa kila mmoja, unapofanya yale yanayo kufurahisha maishani mwako usijaribu kuifananisha na kwa mwenzio, maana Kauli zinaweza kuwa sawa huku matendo yakiwa tofauti.
Usifuate mkumbo kama hujaweza kutoa kauli, kubali unapokosea si ya kuwa hakuna aliyepatia, nikisema mimi nimesema mimi, nikisema sisi basi tumesema Pamoja, mengine huwa yanatia hamasa ya kufanya ikiwa yanaeleweka mambo yaliyozoeleka hufanyika kwani yanaeleweka na isije ukaamini sana lako ambalo limefanywa na mwengine.
Siwezi kusema kauli zangu ni nzuri kwani hata wengine wanayaona matendo kwa namna ile wawezavyo, matendo yako yanaweza kuwa mabaya na kauli zikafanya kulainisha matendo hayo. simaanishi mmoja akisema nenda na wewe uende, bali ikawe mmoja kasema nenda na ikafikirika utaendaje, tofautisha kauli yako kwa namna unavyoweza kutenda, ama matendo yako ili kuweza kutamkwa.