Tuesday, June 5, 2012

JANA NA LEO.


Jana ikawa siku ya maandalizi na leo ndiyo leo,ndiyo ikawa na maana ya uangalizi pale la muhimu likawa matoleo,ikiwa kwa mara chache yakikaribia usoni huruma kwa mwenzio,ikiwa mara chache yakikaribia rohoni ya nini kwa mkeo,hakuna asiyependa maana maadui wapo,hakuna asiyechukia maana tunaopenda tupo,maisha yameharibu kuta kufanya nyufa na kuonekana leo,maisha yameharibu vitu kufanya watu na mahusiano yao,isiwe hatari ya mwenzako ikawe kinywani baada ya kileo,isiwe adhabu ya mwenzako ikawa samahani kwa leo

Pengine umechelewa kucheka,pengine umewahi kununa,maana ulipaswa kucheka jana na kununa leo,vile ikawa jana na leo,pengine hata mavazi ya jana yasionekane ni yaleo,tutasahauliana jamani tusijefanyiana ya haya ungeyafany a jana,usijeugua magonjwa ukasema yamekuja leo,ukitafuta sababu na kurudi jana na kusema walipasa,walileta wao.

Mengine haina haja ya kumwachia mungu,pengine haina haja ya kumsemea ndugu,ya leo uyaache ya jana kafanya nani uangalie usije vuna mabua ukaja fanana na nyani,ya dunia yameongezeka na hizi pilika kiu zikijaa vinywani.

Ya leo yamekuwa machache kwa imani ya wasio tamani,ya jana yalikuwa mengi kwa imani iliyotamani,maana umetaka uje sasa,maana umetaka ufike leo,kumbe ulitamani yale ya jana yaje leo,kumbe haujatamani kwa ya leo yakafika kesho,hapana haya ya leo kwa kweli yabaki hapa,yaishie hapa na kama yakitaka kuondoka yakaenda basi yarudi jana.

Kesho ije itatukuta vizuri,kesho ije kama ni kuta
umezipamba vizuri,

IKULU..

Kule kwetu kuna mahala panaitwa makunguru,ali hali ingalikuwa nzuri tungalihamishia ikulu,



  

mambo yamekuwa mengi hata ya kujistili nayo yamekosa uhuru,ikabaki kupuuza uliyonayo na kusubiri msururu,maana vya kugawiwa  na yenyewe imekuwa ndiyo vinakunusuru,ikidhihilisha nia za watu kuelekea ikulu,ubadilishe maana na tafsiri ya  safari yako usije kupata laana yasiyo ya maana kwa sababu pengine hata sizo zako,ikulu ni patamu labda ujaribu nafsi yayule,ikiwa kila mmoja anayo nafasi ya kuona kile akifikiliacho,ikiwa kila mmoja akitaka yale mazuri machache kumfikiapo.

Matunda yametoka mtini pale,vijana wahini mwende illi mkayale,miti isije kauka mashambani,kijana ufanye hima usilale,pengine wakati wa kueleweka ndiyo huu,ikiwa watu wanahitaji kuelewa tu,kujua kama iliyopo ndiyo sahihi na hakuna nyingine,maana zaidi utafanya kukopi na baadaye kutoa kile kilichotoka,hapo unakuwa umetohoa,usipende viongozi hao,kila aliye mtu aonyeshe nguvu zake na ainuke,shamba liko tayari kwa kulima na miti ni michache,shamba limekuwa laini kwa kulima kwa wa mjini wachache.

Kuitangaza nia sio kama kuzamia,kuitangaza nia sio ya kutaka kushika mkia,maana wa kuongoza akiwa ametangulia wakuongozwa hupaswa kuvumilia,sio zikaje taabu ukasema ungevumilia,yatakiwa upate sababu na moyo kuutia utaishia njiani pale madongo yanapokujia,yataishia kinywani kwa kidogo utakayopatiwa.usiumize sana matumbo kwa kula chakula na mawazo kufikiria,usipate presha sana na moyo wako kwa uwoga wa kutokuchaguliwa.

Leo twende kesho wengine walitangulia,kwa uchache uliopo usipofanya leo ya kesho ni kwa wengine kuwatukia,yapasa sasa ukiwa na imani utaingia,yapasa sasa kuomba ruhusa ili ukafikirika kuingia,haujabuluzwa sana kwa nguvu ukaingia,haujaambiwa sana kwa macho na masikio yakasikia.unaisubiri kesho ije maana wengine walitangulia,unasubiri kesho ije maana majibu yalitangulia,maswali ya leo umetakiwa kujibu kesho kwa kuamkia,maswali ya kesho ujibu leo ukifikiria,ikulu imenona kwa utamu ninaouhisia,ikulu sio Dodoma ni dare s salaam naskia!

Ngoja tuache tuone na utasikia,maana ya kesho kwa wengine ni vigumu kuyafikiria..

TAFUTA..

Ombeni mtapewa tafuteni mtapata,imani na kweli ya mtu kumwelewa,ama imani kujielewa,vyovyote basi na majibu tukayaelewa,leo ni mara ya ngapi nairudia,imekuja sasa naurudia,kwa kuwa umekuwa ni mziki mzuri,pengine kwa kuwaona watu wakicheza,pengine kwa kuona mziki ukicheza wenyewe maana watu wanaweza kucheza vibaya kuliko mziki ulivyocheza wenyewe na hapa tukasema ni makosa ya mtegenezaji ikiwa hatukujua Yule aliyeimba,wimbo huu mtamu kweli,Tanzania Tanzania nitaaiimbimbia daima.

Kwa ufupi tukaja bila kuchoshana,kwa kirefu tukaja ili kuelewana,watu wamekuwa wakali kwa ngoma wapigiwayo,watu wamekasirika kwa ngoma na unyago,pengine tusijue kuucheza tukasema tumeweza maana wengi wao waliotangulia walikuwa wakijikweza,hizi sio stori kwa watanzania walioko jikoni,hizi sio stori kwa watanzania ambao hawaoni.

Hapo nakasirika,hapo nakumbuka,maana kweli mwisho tuweke nukta,tukija huwa tunaeleweka,tukiwapo huwa kinasomeka,kwa wale watanzania walio na hulka,sio kwa vina tukasema yamesababishika sio kwa kina tukasema tukasemeheka,pengine makosa yetu yakawa yao,pengine dhambi zetu wakabeba wao,dunia imekuwa ni chungu kwa kuelekezwa na mtandao,dunia ya kuchunguria haijafanana na sufuria zao.

Mbishi mbishie akitaka jibu mpatie,mjanja msikilize akitaka swali muelekeze,maana hawa wajanja wamekuja wengi,pengine tukawaita majina yao,lakini wasifanane na wayao,pengine tukajiita majina yetu na wala yasifanane na yao,kati na kati wametuweka pembeni yao,karibu na kati yatupasa kufikiria majibu yao,hivi ni vichache baadhi vipo kwa wao,mengine ni machache labda tuanze na kwao.

Tunaondoa uwoga kwa kuomba kilichopo,cha baadaye wacha kije kwa msimamo uliopo.sikubali leo kiduku kukitilia mkong’oto,sikubali leo kwa watanzania kuishi katika maporomoko,tukumbuke leo kwangu kesho kwako,tukumbuke ya leo yangu kesho yako.

tafuta,tafuta iliyo ya kwako..Tafute kile kilicho chako!!

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...