Jana ikawa siku ya maandalizi na leo ndiyo leo,ndiyo ikawa
na maana ya uangalizi pale la muhimu likawa matoleo,ikiwa kwa mara chache yakikaribia
usoni huruma kwa mwenzio,ikiwa mara chache yakikaribia rohoni ya nini kwa
mkeo,hakuna asiyependa maana maadui wapo,hakuna asiyechukia maana tunaopenda
tupo,maisha yameharibu kuta kufanya nyufa na kuonekana leo,maisha yameharibu
vitu kufanya watu na mahusiano yao,isiwe hatari ya mwenzako ikawe kinywani
baada ya kileo,isiwe adhabu ya mwenzako ikawa samahani kwa leo
Pengine umechelewa kucheka,pengine umewahi kununa,maana ulipaswa kucheka jana na kununa leo,vile ikawa jana na leo,pengine hata mavazi
ya jana yasionekane ni yaleo,tutasahauliana jamani tusijefanyiana ya haya ungeyafany a jana,usijeugua magonjwa ukasema yamekuja leo,ukitafuta sababu na kurudi jana na kusema
walipasa,walileta wao.
Mengine haina haja ya kumwachia mungu,pengine haina haja ya
kumsemea ndugu,ya leo uyaache ya jana kafanya nani uangalie usije vuna mabua ukaja fanana na nyani,ya dunia yameongezeka na hizi pilika kiu zikijaa
vinywani.
Ya leo yamekuwa machache kwa imani ya wasio tamani,ya jana
yalikuwa mengi kwa imani iliyotamani,maana umetaka uje sasa,maana umetaka ufike leo,kumbe ulitamani yale ya jana yaje leo,kumbe haujatamani kwa ya leo
yakafika kesho,hapana haya ya leo kwa kweli yabaki hapa,yaishie hapa na kama yakitaka kuondoka yakaenda basi yarudi jana.
Kesho ije itatukuta vizuri,kesho ije kama ni kuta
umezipamba vizuri,
umezipamba vizuri,
No comments:
Post a Comment