Tuesday, January 16, 2024

HASIRA YAKO

Unakasirikia maisha yako wengine wakiwa na furaha,ikiwa lengo si kutaka kuijua furaha ya mwengine bali kujua ni namna gani hasira zako zinakupeleka,binadamu tupo tofuti,mmoja hali nyama ya mbuzi kwa kuwa inamtoa vipele mwengine hali nyama ya nguruwe kwa sababu ya dini sasa nikikasirika usiniulize nimekasikia nini,nina mengi.

Kasirika,usikarike pasipo na sababu.upumbavu wa mtu mmoja usikufanye uvunje simu na mwengine kufikia kumkata mtu panga.angalia unapokasirika sauti yako ya ndani inakwambia nini na kabla haujatenda kwa kutumia kiungo chochote cha mwili yakupasa kutafakari,maana kuna wale wenye hasira za ndani(chuki) hawafanyi mambo yao hadharani.

kama ilivyo katika michezo mmoja akamchezea rafu mwenzake basi wanamichezo waliiga kwenye maisha,na ndiyo maana unasikia michezo haiitaji hasira,ukisusa wenzako wanakula na wenzako huwa wanakula mpaka baadaye ukakitamani tena hicho chakula,kasirika vizuri.

Dunia hadaa utakasirishwa wakitaka kujua maamuzi yako,ukishajua umekasirikia nini maamuzi yako yawe tofauti na hasira zako kwani kweli maisha yana mengi lakini kuna mengine sio ya kukasirikia fikiri mtu anakasirikia mafanikio yako na atayekumbatia maamuzi ya hasira zako yampasa kuwa yeye.

ISHI NA YAKO

Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha ya mwengine kwa kuwa umefika mahala fulani,tambua maisha yana stepu,uliyopo sasa mwengine alipita juzi ukicheka leo mwenzako kulia ni sawa na kulia wakati mwenzako anacheka.

Usibabaike na waliowahi kufikia ukitakacho,tambua muda wako ikiwa unajiandaa jiandae vyema ili ukikosa isiwe lawama kwa wengine,maana imekuwa mmoja akishindwa akatoa sababu za mwengine kumuangusha.

Usifikiri ni raisi kukaza jambo,kuna mengine yanakaza mpaka kufungua inakuwa kama ni kukaza,ujiandae vyema maana kuna vilio,maumivu yasiyo na machozi na hata usumbufu usiohitajika.yatambue magumu yako na jipe muda kuyatatua ikiwa humu duniani wote mpaka muda huu tunatafuta maisha.

Kheri udongo unarudi utokapo maana ingekuwa foleni kubwa barabarani kwa kuwapa heshima wajionao miungu,usifikiri wakati wa magumu peke yake mwishowe ukawapa lawama watu wasio husika na maisha yako,tambua nafasi yako si ile aisemeayo mwengine,watu huwa wanaongezea kwa kile ulichonacho.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...