Wednesday, February 1, 2012

LENGO NI KUYAELEWA.


Lengo ni mambo au vitu ambavyo mwana adamu anavyomiliki katika akili au fikra yake ikiwa ni katika kuyakamilisha yale ambayo yana kusudi katika upande wake,katika kuelewa mambo au vitu ni lazima tujue ni sababu gani au ni katika namna gani ambavyo hivyo vitu tunavyovihitaji vinaeleleweka,ndipo hapo inahitaji wote tupaswe kuelewa,hapa tuelewe,ni lazima tuelewe vile vilivyo katika malengo yetu.

Katika baadhi ya mambo kuna yale mabaya na mazuri zaidi mengi hasa pale lengo linapotimia,yale mabovu ndiyo haya mazima katika upande mwingine,na yale tunayoyasema ni magumu ndio hasa yanayohitajika,ikiwezekana.tunayoyafikiria ni mengi mno,ikiwa yamo yote hasa zaidi tunapoyasema nayo tukayajumuisha,

Hii yote ni katika kuweza au kuelewa jambo au mambo,kadri siku zinavyoenda wanaadamu tunapaswa kujua zaidi,ikiwa ni kuongeza ufanisi na uwezekano wa nafasi endapo hata ikatokea isiwe ni tofauti ya vile malengo yetu yalipo,hata kama bado hatujapanga tufikiri nini kitakacho tusaidia,

Angalau kwa sasa ili na baadae wakafanye wengine mazuri yale.Lengo sio kubishana,sio tu moja na likaeleweka,tuyatafute,tusiyafuate,tuyatende au wengine ndiyo watende,ikiwa tu kwa umoja imeshindikana,tuone kwa yale yanayoelezeka na yasiyo elezeka,lengo ni kuyaelewa,yote yanafanana ingawaje yote yakawa ni tofauti,vile vilivyoumbwa kwa mfano ndiyo vile vinavyoleta utofauti yaani vile vilivyopita katika mikono yetu sisi wanaadamu na tukavisema kwamba ni vyetu,

Tukiwa na maana halisi ya chanzo na mahala Fulani yalipotokea,kimsingi ili kukuchanganya ni lazima tuelewe ni wapi palituchanganya,ili mwalimu asiwe na kazi kubwa ya kurekebisha au hata kuacha tuangamie ya kuwa tumekuwa wagumu sana kuelewa.

Usitumie nguvu wakati uwezo unao,ninaposema usitumie nguvu sio kwamba usishinde njaa wakati ni wazi uwezo hauna,kwani ikawa hivyo ni dhambi za kuiba zitaongezeka,na ikiwa lengo ni kuyaelewa kwa wenye dhambi hufurahia majumuisho,kwani yaweza kuwa utajiri pia.

Kushiba kwa moyo ni kuridhika,kuelewa ni pale akili inaposhiba vyake pia,pale aelewapo mmoja sio lazima na wa pili afuate hivyo,tuogope wengine wasije wakazidisha maana na wao ni furaha yao kucheka wengine,kama inavyokuwa hakuna njaa inayoshindikana kwa tumbo,kwani inapozidi na yenyewe huuma,hapo ikiwa inataka kutambulika kwa lengo lake.

Tujenge madaraja yaliyo imara,kwa upande mmoja wengine tutadhani tutapita sisi tu,wengine labda watajenga ya kwao,ikiwa na sisi tuliyojijengea hatuwazi tumejenga wapi,isiwe tumeelewa tu utofauti wa tumbo na moyo kiuhalisia,ni kama pale iwapo shida na raha ikatokea,pale baadhi wakidhani shida za mmoja ndiye raha zake,ikiwa kwa wao hizo zinaweza kuwa ni raha,lakini yote ni malengo tu,na labda tufahamu shida zipo tu labda iwepo kuna unafuu.

Kwa yale moyo uyapatayo ni rahisi zaidi kuliko haya mengine niyasemayo,tusifahamau pale tunapohitaji mabadiliko,fahamu ziwepo na hasa zikawe ni suluhisho pale mabadiliko yanapotokea kwani tuna haki ya kuyafahamu mabadiliko hayo kabla,tunapojua tunaelewa,kuelewa sio kufahamu,kufanya ya kuwa vile si hivyo,au hivi ilivyotakiwa lengo ni kuyaelewa,yote ni mambo,ule uzuri au ubaya ni utofauti,kama vile chafu na safi,au kueleweka ama sio kueleweka,chaguzi ni lako katika nzuri au tofauti,chafu au safi ikiwa ni kueleweka ama la.tufanye yataeleweka tu,kwa Yule aelewaye yawe yanaeleweka tu.

Lengo hili halikuwa langu,ikiwa limeonekana katika upande mwingine ni lazima uelewe  maana usibishane ingawaje hatujaambiana,hili au lile liwe lengo letu tena tulilolikusudia,lengo letu linapokuwa moja si kwamba wewe utafanya vile mimi nitakavyo fanya,au tutafanya pamoja ikawe mwalimu akasema Fulani ame nakili kwa mwenza,tuyaelewe na tuone utofauti wa malengo yetu.

By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714 33 66 57.

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO : Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha...