Monday, July 9, 2012

NASHANGAA.!


Nashangaa kuona watu wanashangaa,maana sijui kipi ni kigeni,ama mimi ni nani,wewe je?pengine tusifikiri utamu wa sukari tukasahau wa asali,wengine watasema si yale yale tu lakini ile kuandika nyingineyo yenye maana mbadala bila kujua kama kuna maana tofauti hapo hatutaelewana ,hapa nafsi zitatutoka zana baada ya kuja kushangaa kama kweli ya fulani ndiyo ya kweli,ukisahau anaendelea kuishi kwa nini tusimkataze utapeli wake,maana zaidi utaingia kwa watoto wetu hapo inakuwa ni jasusi na mtutu.hatutashangaa vifo hapo,yamkini uwepo tu.

Karibu nyumba ya pili kuna sherehe,kumbe hapo mgeni kamkaribisha mgeni,hapo mwenyeji kaingiliwa na mgeni,haya mengine ni baadhi ya furaha katika yale machache yanayokuja,pengine tusijekushangaa hata yaliyopita,hapo yatupasa kuyarudia na sijui mageni ni yapi..?zamani ndiyo watu walikuwa wanashangaa mataa kwa sababu walikuja kwa ajili hiyo,siku hizi hata vijijini kuna mataa..kila mtu anatafuta lake,kila mtu anasiri yake moyoni..kila mtu na kitu vipo hivyo kwa sababu hiyo.

Tunakuja kustaajabu haya ya musa sasa,naona tunashangaa jua kuwaka mpaka jioni,maana yawekuwa nastahili la kuzama,kaisari kama unataka nipe ila kama unaitaka chukua,maana lipi limekuwa bora kama sio la kuambiwa?angalia hayo yote ni kwa sababu ya kaisari,mwanangu angalia pengine usisahau kusali.nashangaa kuona nilitaka kuandika mengi na nimeishia hapa,hili geni sasa,hili jipya akilini pengine linatoka ama linaingia,kumbe kwa geni yastahiri..

YAACHE YAENDE..!!


Maana mengine yamekuja kama tishio,mengine yamekuja ili yakionekana yaonekane ya kileo,wanajua wachache wale wanaoitwa walevi,maana kila mtu anajiona yeye mwema,katika kuishi maisha yale mtu akaishi anavyotaka,maana hata ukahamia kaburini nahisi utasikia wachache wakinong’oneza,maana wao si hawajawahi…!!hawajui nini maana ya kuona pale,ama kufika pale,pengine yale ni mengine yaache yaende,pengine yale ni mengine waache watende,

Muda huo unapofika ndiyo unakuwa wakati wangu,maana pengine ndiyo wako sasa,kama vile tunamcheka Yule anayecheza kipindi kifupi bila ya kujua urefu ukoje,mengine ni ya lazima kuelewa pale inapotakiwa kufanikiwa,maana kila mtu na mwenzake wanataka kufanikiwa,wakiwa  na tegemezi na kwenda nayo yale waliyo nayo na kama ni maadui basi kheri waongezeke,hapo wakiwa wawili pamoja na Yule mshamba,maisha sio kuelewa sana sana ya kutaka kuelewa sana,maana hapo tutakuwa tunaelewa tu,labda kukumbuka,na wala haina haja ya kuyakumbukia wacha yaendee..

Kesho tutalia zaidi ilivyo ya leo,maana hichi cha leo tulikijua tu,pengine tumezoea sana ili kutaka kueleweka,akiyafuata  Yule mjinga na mwenzake atamcheka,hapo tutapigana na kukumbuka umoja wetu usioeleweka,kuna Yule amepata kitu na asijue nini kile zaidi ya Yule anayepata kitu na kujua nini hiki,hiki kinatumika,zaidi ya vile ikafikirika maana kwa mwengine anaweza kuwa hafikirii mmoja unapofikiria,pengine sio wengi,pengine sio mengi,haya mengine tuyaache yaende tu!!

UCHAGUZI.


Hapa isipo katika maana ya nafsi,ikawe ni kwa nini imekuwa hivyo ama ukapenda ama ukakataa,yaani kwa nini tunachagua yale yanayohitaji kuchaguliwa,maana siyo kwa vile nimechagua kwa nafsi yangu,hapa ikawe imesemeka ndiyo maana ikachagulika,maana kama hakuna kilichopo ama kufanyika kwa nini ichaguliwe iyo?
hakuna namna ya kusema tunaweza kuendelea na wakati uwazi unaonekana,tena uwazi umedhirika pale kwa  mda uliotumika,maana uwazi ni kweli,

sasa ikawe hadharani sio mahala pa wazi maana hata unayoyachagua yanakuwa mabaya,ama yakijiweka urembo ndiyo ije haja ya kuyatunukia,uzuri wa kuonekana hauongozi maana,uzuri wa moyo tokea chemichemi huonekana,maana baadaye huwa bonde kubwa kwa ajili ya watu kukata kiu zao,pengine wakashangae huko,maana kwa kujiuliza ni ile chemichemi kweli?

Hapo baadaye tumeaminiana mpaka tunakuja kuchaguana,sasa uangalie kwani  hatujachagua familia,maana utasikia aah Yule ni kiongozi wa kati,maana walishamchunguza mwanzo wakisema alipendelewa kwa kupewa,sasa aliyempa naye si alichagua,hapa unasema ilo ni sahihi kupitia nafsi, ikiwa kwa nini sijui kama itaelezeka kwa haraka,maana waliochagua hawajapata kitu kabisa.wamegoma kusema,wamegoma kufanya kazi,hii hatari na chaguzi.

Mungu anawapenda watu wake ndiyo maana ya kumtoa mwanaye yesu kristu,alijua ni kwa sababu gani anamtoa yesu,hatukujua kwa sababu gani yesu alikuja kwetu,ndiyo maana ya kufundishwa,Kesho inaweza fika matokeo ya chaguzi langu kutokea,hapo ikiwa ilifikirika kwa nini na  nafsi haina haja kuhoji kuwa ni ya nini,ni matokeo tu.ni mfano tu.

Chaguzi limelenga tukio,kama unahitaji kulijua lengo ni lazima ufikirie chaguzi zetu,maana kesho ni siku ndiyo,ikiwa jana ulichanganyana sidhani kama leo tutalewana bila ya kuchagua usahihi,lazima tufanye masahihisho,lazima tuelewe kwa nini hatukuelewa,kushindwa,kuweza kwa kuwa lolote mahala pale,ikiwa tulichagua hilo.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...