Friday, February 24, 2012

LINALOKATAZWA LINAHITAJI KUENDELEA

                                                                                 
Yote yaliyopo yapo katika muda,ikiwa muda unapita na mateso ama starehe vinakuzidi,kwa wale wasio teseka labda watuambie raha zao maana wasipojua na kwa wengine nayo hayo ni mateso,kwa lolote lenye muda uliopitwa lina haki ya kukumbukwa,kwani kwa kile akitendacho mtu wakati wowote na mahala popote ni dhamana yake katika maisha yake hakuna kile kibaya kama kile kilicho kizuri kwa zawadi yake kuwa yale mema mitaani hali imeharibika ikiwa watu wanaona ni kheri kupumzika kuliko kupigika,waliopigika haina haja ya kuhadithia kwani kila mtu anapigika katika namna atakavyoweza kupiga,muda unapopita kinachopotea sio muda bali ni mambo yale ambayo yanapaswa kufanyika katika ule muda.

Utakaa na vipaji chako ukisema unaweza au ukaona umefanya ukajisifia umeweza hapo utakuwa umeweza kweli kwani haina haja ya kumtizamia mwenzako wakati wewe ndiyo kwanza u mwanzo,taabu ije pale mtu anapoambiwa hajaweza na ujue imejulikanaje,maana uliambiana haina haja ya kumtazamia mwenza ugomvi kwa muda Fulani ni vyema kwani ni njia ya kuleta amani,amani ni imani.,asikukataze mtu kupenda ufanyacho hapa ikiwa unafanya chochote na una mlengo nacho,akatazaye aonyeshe lililo bora ilivyo zaidi linalokatazwa maana watanzania tumezaliwa na kwanini sio mimi huku tukisahau yale ya kwanini mimi,maana yao ya kujutia yanakuja baada ya kutenda ikawa umejifikiria na kukuta ni mabovu katika jamii tena kwa ugunduzi ikiwa ulishindwa kukatazwa,kumbe ile kwa nini mimi ni kujifunza zaidi ya kwa nini sio mimi,ningelikuwa mkubwa ningeliwakataza wale wa kwanini sio mimi.

Dunia hii ni ya kufurahisha sana,maana yale yanayokuwa matamu ndiyo yamewekewa sheria,tena isiwezekane kufanyika sio ya kwamba hakuna uwezo bali isifanyike,yaweza kuwa ni sawa na mwana akatazwapo kuchezea wembe na mzaziwe,kwani ungeliingia katika fikra za mwana naye ukamsikia akisema anataka akate kucha hapo ungempa wembe mpya,asije kujikata na ule wametumia watu wengi,apate ulio na makali na aone mapendezo ya ncha za kucha pindi akatapo,kumbe ikaja naye akataka kuona utamu kwa japo kujaribu kwa kipande cha wembe kilichotumika,alikatazwa bila hata ya sababu akaona kumkalipia mwana pasipo na sababu ya maelezo ni kumfanya aendelee

Kipindi Fulani imesikika kwa mzazi kutembea na wana,hapa ni kwamba hata mzazi na yeye hakujua alipoambia huyu ni mama yako au ni baba yako,maana inapaswa hata aibu sasa isipo kuwa wote katika nafsi hawafahamu kitu heshima,wanaokataza ni wakubwa tena wanaokatazwa ni wadogo,wakubwa ndiyo wanaweza kuwa wazazi wa wadogo,ikitokea wadogo ndiyo wamekuwa wazazi wa wakubwa hapa inabidi tutunge sheria kari sana,tena isiwe kuna kuzaliana tena maana tutakuwa ni mbwa,hivyo ndivyo wasemavyo wale wanaokataza wakiweka miiba ili hata mbuzi hao wakipita wapate kujichoma,endapo utakuwa kama mbwa walio na njaa ya kula kweli utajichoma sana na kuumia huku usifahamu dawa za maumivu ndiyo zilihitaji kufanya maendeleo,kwani ikiwa utapona na dawa hizo si utarudi kula majani yale tena?Njaa ya mmoja haimfikirii mwingine,ni namna ya kutaka kuendelea kuishi katika namna unazozipenda,na hapa haifai kuzikataza wacha ziume tu ili zisije zikaendelea.

By: Benson G Makaya,

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...