Monday, June 11, 2012

LENGA..

Nayawaza  madanganyifu kwa kuona yanayoongelewa,ikiwa tutaongea kwa utimilifu basi tutaongea kwa kusemelea,mengi yaliyokimbiwa yamefutwa mwanzo ikiwa ilitegemewa,pengine isiwe imekuwa bali ikakamilika kwa kuwa.

Hapa tunazungumzia matukio,ikiwa ni mara zote kwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho tukasema ile ikawa na imekuwa kwa maana iliumbwa.

Halazimishwi paka kwa kula mchuzi wa samaki,hiyo ikiwa ni mwanzo labda kwa vile tumezoea,hapa tumezoea mengi na mengine tukadanganyika,mazoea haya yatatushindisha kwa kuwa tumetegemea hivyo,
pengine haya ni mengi sana kwa kuona,
ikiwa wametazama sana wa zamani na leo tusiseme tumeona,tunahitaji mengi sana na hili la leo liache liendelee kwanza maana imekuwa hivyo

Huu ni mtazamo kwa kuwa umeonekana,hasa kwa vijana kwa kuwa yote imekuja kwa maana,tusizungumzie leo ikiwa tunategemea kesho mbovu maaana tutafanya kuumia kwa kuwa na sehemu  iliyo na maumivu bila ya uvimbe,
huu utakuwa ni ugonjwa mwingine kabisa,hapa tukasema sijui ni nini lakini ndiyo imekuwa hivyo,ikiwa imepasa imetangulia,na wote tukiwa pembeni bila ya kuelewa maana hatujajua kama tumeweza.

Tumalize na mwisho kwa lengo la kulenga,tukapeleka pale ulipo mwisho ya kuwa tumejifunza hivyo,
yaani hayo yakiwa ni baadhi ya mazoezi,katika Fulani ikawe ni Fulani na nani,
hapa tukiwa hatuna imani,hapa tukiwa hatujasema jamani,tusipojua imeleta maana gani maana ikafika muda isije kueleweka namna ya ilivyo,hivyo inakuwa imekuwa.

KITAELEWEKA TU.

Vijana ni taifa la kesho,ujana ni nguvu ya leo inayoleta faida kwa ajili ya kesho,unapenda sana kusema maneno fulani,hapo ikiwa ni katika kujipa matumaini na hata vile ilivyo katika kuweza,maana utasahau ulisema nini ulipokuwa unatumia nguvu zetu,hata pengine isije usielewe,

Pengine isije kuwa nguvu zako ulizitumia tofauti,hapa ukiwasahau hata wale waliokuwa wanakugaia vitu ulipokuwa mtoto ukilia,pale ulipokuwa hujui kusema lolote la kubisha maana haikuwa na maana ya kuweza kufanya jambo pekee.

Hakuna yasiyokuwa magumu bila kujua kwamba ni zamu yako,umeona washindi wengi wametutoka dunia,hivyo ikiwa ni namna ya zamuzamu inapokuja,
lazima upokee vile unavyopewa hata kwa kusema asante,maana wengine wanashukrani zao za kutoa.leo usiisuburi sana kwani inaweza kuchelewa hivyo ujaribu kwenda,twendeni kwa mwendo huu huu ikiwa ni kwa umoja,pamoja tukaungana.
Hasira ya mkwezi ni kama ya daktari,pengine ujue kama daktari ni mkwezi..maana uhesabu kwa nini imekuwa hivyo,pengine na sisi tukawe hivyo,kwa kutokusema sio kama ingewezekana,bali kuweza kwa kuonyesha tu kama unafanya,yapo mengi ya kufanya pale uvumilivu unapokuwapo,hii ikiwa kuna mahala fulani furaha ipo tu hewani.

Ujana ni shimo la taka linalohitaji kujisafisha,vijana ndiyo watu watata na hata mitaani kupigana,hii ikiwa inaondoa maana,hapa ni sawa na kusema hautaweza kuwaombea walevi waache pombe bila ya kujua kwa nini wanalewa,yatakuwa sio maombezi haya,mitume walikuwa wanajua,hivyo hata matibabu yamekuwa sahihi tokea enzi zetu za mababu.

Cha mwisho kinachoelekea katika namba moja ni vyema ya kuwa kimejua chenyewe ni cha mwisho,hapa vijana tujijue ili kieleweke,maana utaishi kimfano na kulalamika kama hakijaeleweka.nguvu na imani viambatane,

SEMA WEWE KWANZA VINGINE VITAFUATA..

SEMA KWELI..

               
Hakuna sababu ya kudanganya wakati unahitaji useme ukweli,
uzungumze ujue kile kilicholeta maana,maana haijaja kuwa kweli bila kudanganyana,haijaja kusema kweli bila kuchanganyana,
pengine ukaona pale umekosea kufanya vile,pengine ukaona pale tu ulipopatia,
haki iliyo ya mtu lazima kusema ukweli,pale walipo matapeli  usogee ili kuepukana na ukweli pengine ukajua bora kwa kuchanganyana na matapeli.

Karibu mgeni nyumbani hakujazimwa taa,karibu mwenyeji ya ndani na njiani hakuna kukataa,pengine ulikuja mara ya kwanza na uliona bila taa,pengine ukakataa kurudi kwa kufanya bila manufaa,kwa ukaribu jirani angalia njiani.

 Kinachoendelea ndiyo majibu hasa ya uliyoyapanga,ikiwa kama ufahamu ni mdogo basi litagundulika hilo na sio kwamba kwamba kwa anayefeli maisha anakufa,
hapa ndiyo unamwelewa mungu,hapa ndiyo utakaa na kujua msamaha wa mungu maana ingawa ukashindwa yeye atasamehe,na usikatae hilo kwani umesamehewa mara ngapi?

Yatakuja mengi mengine mapya yatasemeka yalikuwepo,hiyo ikiwa na yenyewe yamechoka huko yatokako,
yakiwa yanahitaji msaada basi yatapenya hata kwenye nafasi iliyo ndogo yako,
ukataze  yale yasiyokuwa na msingi ili uone kitakacho bakia,
maana haitakuwa na maaana dunia kujazwa na vyoote hivi.

Sema kweli visikuchanganye na kwa uwingi uliopo usidanganye !!


ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...