Tuesday, June 12, 2012

INUKA...!!


Amka nguvu unazo,
Usitake kusimama sasa,usikate tamaa mapafu unayo,utake kuamka na wala sio kukaa,hakuna muda  unaomngojea mwenzake,kuna muda pale ukasema na nguvu zikaja,
pengine isijulikane nguvu hizo zimetoka wapi,hapo watu watakuwa wameamka,ikiwa kwa mmoja hataweza kujua ni namna gani anaweza kuwa na mwamko labda ajaribu kufikiri kuhusu kuamka,
maana kwa kile akifaamucho mtu huwa hakimbadilishi yeye zaidi ya kubadilisha mawazo yake,
na hayo mawazo ndiyo yanamuweka mtu kuwa hapo,
akiwa amelala ama ameamka anakuwa mahala pamoja.

Unaweza kupoteza uwezo wako kwa kujilinganisha na maisha,kwani katika akili unaweza kuwa na kujiamini kusiko kuwa na kufanya kazi,hapo utasafiri bila usafiri hapo utapaa bila ya hewa,maana imekuwa hadi mashine zinahitaji kupumua,ikiwa kisingizio ni imechoka.


Watoto wetu wanakuwa na kujaribu kuamka,watoto wetu wanatambaa na kuona wanatembea,wakiwa na imani ya kufanya wafanyavyo wazazi wao,pale akijuwa tofauti mwana basi isiwe tofauti kwa wazazi,maana pengine watoto wanakuwa tofauti na namna ya vile ulivyokuwa mzazi wao,sisi ni wazazi sasa,,tukumbuke ni namna gani tuliwafanya wazazi wetu,wengine tukijiita mababa na pengine wa mama bora ikiwa imetoka kwao

Hata ikawe leo kazaliwa Fulani basi si haki kumuita nani,maana ilikuwa ni kwa yesu pekee,na ingalikuwa bila kujulikana basi yesu angetoka mwanamke,na hapa usifahamu zaidi,pengine usiinuke katika kila kitu,ikiwa unaweza kula vile vilivyotakiwa kuliwa huku umekaa,

Ukae na utazame ni namna gani wengine wameinuka,bila ya kufananisha nafsi bali namna ili kuweza,maana unaweza angalia nafsi ukashindwa na kuhisi na mwengine kashindwa,kumbe ni nafsi zilizo pamoja na kutenda vile visivyo na umoja.ufahamu kwamba kile kinachofikirika kwa mmoja ni kile anachokitafuta na kile anachokitafuta sio kile anachokitafuta mwengine,Inua fikra.

RAFIKI YANGU..

Muda si mwema bila ya kuoneana wema,
pengine ni aibu kubwa kusikia ilitokea kwa sababu ya vile maana baina ya wengi hawahitaji maendeleo,
ni hapa panapokuwa na utofauti,maana imefikirika hivyo
hapa panapoweza kutufanya kuoneana hali,maana hata tukaangalia wakati ni kweli haijulikani je walioweza wakoje?,ni wapi maana mara nyingi tukae,tuongee hata kama si vya leo,tusidanganyane hapo,
tusioneane wivu wala kutamaniana kitofauti hapo yatatendeka vita na la wawili kuona kana la mmoja,
maana kwa sasa ifike tuanze kuambiana namna ya mioyo inavyoenda maana kiasi chake tumejua hata mwanzo wake uko wapi,

Pengine ilianza taratibu na baadaye ikaja hii yote ikiwa inatokana na hali ya hewa,
hapa tutaweka usiku na mchana hata jua lingewaka kutwa nzima mwanzo wa maisha mpaka uzee lazima pangelikuwa na usiku maana wengi tumependa giza sana,tungeweka mahema japo hata tulale,
tufikirie mengine pengine sio ya kirafiki,
tutaumiazana mara nyignine hapa tukiwa tunafuata kwa kusahau na ya kwetu maana tunaposema tuelekee tujue tunaelekea wapi,pale mawazo yanakamilisha jambo kwa kuweza kuona na kutafakari,
maana pale yanapotakiwa yale yaliyoonyooka yapo tiyari machoni hivyo yapasa kuelekea moja kwa moja,

 
 
Tusiseme labda kukiwa na mabonde  tutafanyaje kwa kuziacha fimbo hizi yamakini tusifikiri maana ya pili,
maana walituambia ni moja kwa moja,tusijekuwa  sisi ni wa jinga kwa kutokuwauliza tunaweza kuhama lini duniani,maana tumetoka musoma ni safari hiyo ilikuwa ni safari ndefu sana,
ni kweli wewe ni rafiki bora maana ndiyo hata leo umeniokoa na wabaya nyoka,si juzi ulisema nakuja na ndipo nikagundua uwepo wako..umeniweza kwa yote na umekuwa na upendo na fani yangu,
Kwa kazi ya udereva niliyosomea ilikuwa ni kuangalia pale itakapo tokea,
maana inatembea sana,na pale tupange vikubwa basi basi gari lake litachukua muda sana kufika,si kuna vituo watu wanashuka?hapa tumai na imani ni kuweka kwa dhati,Pale unahisi kuanguka unasema kwani unaielewa?yule asiyeilewa ya mwenzake  ajaribu kuiangalia na yake,maana nafsi tuone kama si tofauti tena bila kusema asante sana rafiki,siku zangu zimekuwa na wewe,Umenipeleka vile nilikuhitaji nilivyokwambia asante,Tena kwa vile imani na mwili vimeelekea kwako

Asante siku..

KULA BATA..

Unapofika wakati ni lazima kuacha,embu tazama wengine wakiwa tofauti na wengine,hapa tukiendelea kujua zaidi ndiyo tutagundua kwamba pengine wengine waliacha,maana haya mambo yamekuwa tofauti sana,si ya kuwa watendaji ni tofauti,si ya kuwa kuwa matukio ni tafuta,hapa tukatambua lengo kwanza.
 
Najaribu kushirikisha nafsi naona hazifanani,labda tushike manati ili kuleta ushindani.hapo ndiyo ikajulikane tulipotokea,hapo ndiyo ikajulikane ilipotakiwa maana ilipasa tuwe huko,isingekuwa na sababu bila ya kusema nini,yaani nini ni kuhitajika pale jambo linapofanana na mazingira.



Pengine tunahitaji mashine ili tukazifanyie kazi,ikiwa elimu ni msingi hapo hakuna ushindani,maana kama kimeeleweka hivyo asiyekuwa na elimu atabaki na lake,pengine ni ujuzi tu,hapa katika kusoma lazima tupate uwezo na nadharia za kufanyia kazi na hapo ukaitwe uzoefu.

Baadaye inakuja sasa watoto hawatakiwi kusumbuka kama baba zao ilivyokuwa,ikiwa wazee walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita hiyo ikiwa sio ushindani labda Fulani anahitaji kuwa namba Fulani,raha mtu anaziona za mwenzake ikiwa taabu ipo kwake,

Pengine bila kulinganisha nafsi zaidi tutabaki na kuendelea kuwa hivyo,imekuwa inafanana sasa kama ilivyo kwa nyoka na chura,basi mmoja ataruka ruka na mwengine kutambaa hiyo  yote ikiwa ni safari ya maisha yao,na katika kuishi maisha  ni lazima kutaka mazuri.
Ikiwa bila taabu na sababu kwanza,basi lazima tufanye kazi,lakini hapa inategemea na taabu,maana taabu si ya kwako tu,pengine tuchague muda wa kufurahi,na tutafurahi kweli kweli.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...