Tuesday, June 12, 2012

INUKA...!!


Amka nguvu unazo,
Usitake kusimama sasa,usikate tamaa mapafu unayo,utake kuamka na wala sio kukaa,hakuna muda  unaomngojea mwenzake,kuna muda pale ukasema na nguvu zikaja,
pengine isijulikane nguvu hizo zimetoka wapi,hapo watu watakuwa wameamka,ikiwa kwa mmoja hataweza kujua ni namna gani anaweza kuwa na mwamko labda ajaribu kufikiri kuhusu kuamka,
maana kwa kile akifaamucho mtu huwa hakimbadilishi yeye zaidi ya kubadilisha mawazo yake,
na hayo mawazo ndiyo yanamuweka mtu kuwa hapo,
akiwa amelala ama ameamka anakuwa mahala pamoja.

Unaweza kupoteza uwezo wako kwa kujilinganisha na maisha,kwani katika akili unaweza kuwa na kujiamini kusiko kuwa na kufanya kazi,hapo utasafiri bila usafiri hapo utapaa bila ya hewa,maana imekuwa hadi mashine zinahitaji kupumua,ikiwa kisingizio ni imechoka.


Watoto wetu wanakuwa na kujaribu kuamka,watoto wetu wanatambaa na kuona wanatembea,wakiwa na imani ya kufanya wafanyavyo wazazi wao,pale akijuwa tofauti mwana basi isiwe tofauti kwa wazazi,maana pengine watoto wanakuwa tofauti na namna ya vile ulivyokuwa mzazi wao,sisi ni wazazi sasa,,tukumbuke ni namna gani tuliwafanya wazazi wetu,wengine tukijiita mababa na pengine wa mama bora ikiwa imetoka kwao

Hata ikawe leo kazaliwa Fulani basi si haki kumuita nani,maana ilikuwa ni kwa yesu pekee,na ingalikuwa bila kujulikana basi yesu angetoka mwanamke,na hapa usifahamu zaidi,pengine usiinuke katika kila kitu,ikiwa unaweza kula vile vilivyotakiwa kuliwa huku umekaa,

Ukae na utazame ni namna gani wengine wameinuka,bila ya kufananisha nafsi bali namna ili kuweza,maana unaweza angalia nafsi ukashindwa na kuhisi na mwengine kashindwa,kumbe ni nafsi zilizo pamoja na kutenda vile visivyo na umoja.ufahamu kwamba kile kinachofikirika kwa mmoja ni kile anachokitafuta na kile anachokitafuta sio kile anachokitafuta mwengine,Inua fikra.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...