Hakuna anayeelewa kwani wengine wanasubiri waelewe wengine ndiyo
wanafanya, bila kujali muda yapasa kufikiri pengine kuwa na wazo, Tumetofautina namna ya kupanga muda wetu, muda haungoji
mtu, ukiwa na subira utapata,pengine hata ukiwa na subira na usielewe unasubiri
nini, utakuwa umechezea muda wako , unapopanda ngazi usidhani ni mlima maana kwa kupanda
na kushuka, korofi nyingine hazina maana ya kuleta kuongeleka, muda wako ukifika
kitaeleweka.
Leo jambo na mambo yameongeleka, kwa yale uliyoyasikia
machache ndiyo ya kuweza kuukamilisha muda uliobakia, pengine ikiwa hakuna muda
uliobaki basi itapaswa kuongezwa, ikiwa kuna mgonjwa hilo ni la
pili maana wa kwanza hakujiweza, ukisema upo njiani lazima ujue
unapoelekea, na uliyefika ulitumia njia gani ili ikiwezekana ukawe wa tofauti. Unapofikiri fikiri na
utofauti uliopo, maana kwa kujifananisha unaweza kujiona Kenge wakati wewe ni Mamba.
Ikiwa umekubari kuwa mamba ni lazima ujue kuogelea nchi
kavu, mwanadamu anayeishi katika maji huyo kazaliwa huko, na akija nchi kavu
lazima aogelee mavumbi. kwa Yule anayeelewa mda wake ni lazima kuufanya si ya
kuhofia mavumbi, maana kama kuchafuka unaweza usitakatishe roho wakati wa kusuuza ila ukaja
muda wa kuvaa na kusema mashine hazikufua vyema, muda ndiyo unaotufanya kuzeeka, haipaswi kuustarehesha muda wako.