Wednesday, June 6, 2012

VIMO..?

Naamka baba nishike mkono,nimeshtuka maana tusije fika kikomo,wameshuka maana hawakulisoma somo,wamechemka kwa sababu ya kuwapo humo,pilika na mazoea yameibua mengine,birika na vya kuzolea yamekuwa mengine,tukaamke tukasahau iwapo kama ipo,tukatembee tukakumbuka kama yapo yapo,yakatembea tukawepo kama ya kukumbuka yapo,pengine ni namna kubwa sana,pengine ni asili kubwa sana,palipooza tupaache maana muda si mrefu patapasuka,embu tuone la pili hata la mwenza maana haya machache yamejichanganya na meupe.

Kinachokuwa na msingi nikuweka nakshi,kinachokuwa na mchuzi ni kuweka nazi,pengine tukaseme kama mwanzo ya kuijua minazi kuliko nafsi zetu,ikawe ni kwa yaliyojaa na mengine kushindwa kutoka,hata kumwagika maana na nafasi imekuwa ndogo hasa kwa wanaowakilisha tu,mbio zisiwepo maana hata nafasi yenyewe ni ndogo,kile kilichokatazwa ndiyo kwanza kinaanza.

Ya jana ndiyo yaliyoleta maana ya leo,ya jana ndiyo maana ikaja leo,muda wowote ni wa kulala hasa pale unapochoka,kwani kulala sio usiku kama sio kupumzika,basi hapa tutaoneana,ikiwa tutapangiana hata muda wa kulala,pengine tukafanye shuguli zetu usiku,hii ikiwa sio mabundi bali Yule aliyefanya mchana alichoka na kwenda kulala wakati mwengine Yule akiwa amelala.

Msingi ni mkubwa kuliko kitu,kuonekana kwa juu lazima tutafute kwa chini,tukainue hata yale yaliyopo majini,maana sasa yahitaji kufanya hayo yote ya ndani,tumejiziba sana tuangalie tusijepumulia mipira,tumejiziba sana tuangalie kwa wale walio na hira,kwani yaweza kufunulika na kutokuonekana kitu hiyo ikiwa walishachukua wataalamu.


ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...