Katika kila kitu kuna sifa,ili kitu kiweze kujisikia kwamba
ni kitu kinahitaji sifa,sio kila sifa ni nzuri,wala sio kila uzuri ni
uzuri,inaweza ikawa ni hivyo kimaandishi na maneno yalivyo lakini katika maana
ikatoka tofauti na uzuri ulivyo,uzuri ni
kwa uzuri tu.Katika yote mazuri huwa juu ya watu,kwa watu haipendezi kukawa na
uzuri bila ya watu kuwa wazuri,ikiwa watu tunatakiwa kuendana na vile
tuvifanyavyo au tunavyoweza kuvimiliki,ikiwa mtu ana chake tunaweza
kutofautisha uzuri ikiwa na watu pia tuko tofauti,ikiwa katika mavazi na undani
wetu zaidi,kwani sio wote wanaovaa vizuri kuonyesha vyao,ieleweke kuvaa vizuri
sio kupendeza kwani wengine hufurahisha maumbile na mioyo kwa kuvaa wawezavyo
ikiwa ni tofauti na uzuri,mavazi ndiyo yanayomfanya mtu aonekane katika namna
inayompendeza yeye,mavazi ndio humtambulisha mwanaadam,tena tusifike mbali kwa
kuulizia jinsia maana mavazi tunayaona wenyewe.
Wanaocheka sasa baadae wanaweza kutafuta wao,kama lengo ni
kuuelewa uzuri.tukiwa tunajifahamu ni sisi tusitake na wengine watujue tusijifanye
tupo juu wakati ni chini tusipopajua,tutaumia tukiwaza mazuri yamepita bila
kuonekana wakati ni sisi wenyewe tulikuwa katika mabaya,ingawaje haikupendeza
kwa mabaya kuongeleka pengine yangekuwa ni sawa na yale mazuri,labda
utofautishaji tu,ni kama pale tunapoimba na kusoma na ifike kipindi tusielewe
kama tulikuwa tunaimba ama tunasoma,kwani muda mzuri wa kufikiri yote hayo
ungekuwa ule wakati hasa kabla ya kutenda,ingawaje sio kosa,na hakuna wa kumpa
mwenzake lawama kwani kila mtu ni mzuri katika upande wake.
Lugha huwa zinachanganya sana,tatizo sio kusikika,tatizo sio
njia ya mawasiliano,tatizo ni kusikia,kivingine tumeweza kusikika tofauti na
vile maana ya mtu inavyoweza kumjia ikiwa tunasikia kwa lugha nzuri na
safi,kama ni mbaya basi inapaswa kubadilishwa,maana hata sasa tumekuwa
tukijitahidi kufahamu lugha nyingine,na hapa tuone uzuri,ya kuwa sio ile ya
kwanza haifai bali na ya pili imekuwa bora,na ya tatu mwishowe tutakuja
kugundua zote ni nzuri ila utofauti ni pale katika matumizi ya lugha hizo,ikiwa
wengine wanatumia lugha chafu haimaanishi ni wachafu,labda lugha chafu
ilitumika kumwambia mtu aache uchafu wake,lugha ile inaweza kuonekana ni nzuri
kwa mchafu,yakuwa ni yake.
Nguvu haibadilishi rangi,kile kinachokuwa kibaya baada ya
kupungua basi ni kizuri maana ni kimepungua tu,kumbe itafika kipindi tunaweza
kujaza uzuri wetu hadi mioyoni,maana imekuwa kama ni sura
tunazibadilisha,maumbile tunayaweka vile tunavyotaka wabaya waone vizuri,yaweza
kuwa nasi ni wabaya na tunatenda ili
tuonekane tumefanya vizuri,lakini katika yote ni heli tumefanya,maana tusiogope
kujifunza,ikiwa watu wanajenga madaraja sio kwa ajili wapiti peke yao,na kwa
kile chochote kilicho kibaya kimetendeka nasisi tukajifunze juu ya hicho,tusije kunywa sumu na haya maisha
yalivyo magumu,maana siku hizi tunapona,tatizo linakuja katika kuendelea kuishi
kwani mtu aliyekata tama anastaili falaja,lakini hawa wa kutoa faraja nao
wamekuwa wafanyakazi,wanatafuta mshahara ingawaje mwanzo waliweza,na ndiyo
maana ya kufika mpaka muda huu
Tuiache imani ibaki kama dhamana,ikiwa ni lazima turudi na kufanya yale
mazuri ya maana.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66
57.