Sunday, February 19, 2012

Makaya's Forum: MAKINI.

Makaya's Forum: MAKINI.: Tuangalie,tuone ni tunatumika katika utofauti wa namna gani ikiwa pamoja na mashine au mashine zinatumika ikiwa kama ni mifano yetu,zik...

MAKINI.


NIangalie,Nione ni natumika katika utofauti wa namna gani ikiwa pamoja na mashine au mashine zinatumika ikiwa kama  ni mifano yangu,zikimaanisha mimi ndiyo mashine na zenyewe zimetengenezwa kwa mifano yangu pia.bora hivi ilivyo maana ikawa haina haja ya kuzoea kile kilicho halisia,kwa umakini ni lazima ujitambue ya kuwa nisiwe mvivu,nataka kazi na nisijue huko makazini kuna nini nachokifuata,Haina haja ya kuwalazimisha walimu na wakati wanafunzi wenyewe hawaelewi,nikisema waelekezwe wanafunzi nitaingilia majukumu ya walimu,tena inaweza kuwa chukizo kwani muda wote huo shuleni wanafunzi wanajifunza nini?au unavyovijua hujui kama ndivyo unavyovifanya,maana tabia yao ni kufundishwa ili iweze kufanyika,ikiwa kwa kuona ama kusikiliza yote ni lazima niwe na umakini nayo,kwani yale yanayopita yananipitia hapa nilipo,utachaanganyikiwa kwa kutokuwa makini,kwa kutokuwa mwangalifu na ufuatiliaji wa mambo yako usifanye kuwa unapelekwa kila mara,kwani itafika kipindi utachoka kupelekwa pelekwa kama mashine,ikiwa ulikuwa unapelekwa basi wapo waliokuwa wana upeleka peleka,na wao wanaweza wakaamua kukupeleka kipindi pale umechoka,hautakuwa utumwa,hayatakuwa mateso,ni sawa na jambo usilolijua,labda kwa namna itakavyo tokea ndivyo italeta maana itakayo kuwepo,labda kwa tahadhari ufikiri na uamue kwamba unahitaji kujitambua.

Yule anayefundisha bila kuyajua mazingira yake ana uwalakini wa kuitwa mwalimu,lakini ya kuwa kuna uhaba wa kufikiri bora ikawe kujikimu,maana imefikia wakati utaamua kuwa mwizi alafu ukakataza kuiba, ,na ukija kukamatwa uelewe ulikuwa kama magurudumu ya gari,ikiwa kuna kona ulikatishwa tu,kwa hiyo siyo mageni sana katika kutokuyaelewa,wachache wanaelewa  kwa jinsi tunavyoelewa,anapotangulia mwalimu darasa hupanga yale waliyoambiwa na mwalimu,njia mara nyingi huonekana kutokana na hali ya hewa,ingawa unaona kwa umakini lakini unajikuta ukielekea mahala usipopafahamu,na hii yote ikiwa bado unaona labda njia hizi zinahitajika kufanyiwa ukarabati kila muda na watu wakajua,maana tulio maskini tunalia muda wote,na sio kwamba hatupo makini,kwani mengine sio ya daktari.unapolia sio ni watoto,unatoa machungu uliyonayo ukifikiria ulipotoka mpaka ulipofika,kama mtu afanyapo kazi kwa nguvu na kutoa jasho ndivyo ilivyo kwa mateso ya moyo inapokupasa kulia.
Kama walivyojijengea,nguvu usimalize kwa yale waliyokuwekea,ikiwamo inaruhusu usiiruhusu kwanza,wajichunguze wenyewe wanafunzi,hata ukageuza ramani Yule aliyemakini hapotei kwao,ingawaje, zaidi uendelee na umakini wako ili yale ya mbele yakafanane na ya nyuma pia.Umakini unahitajika kwani yaliyobadilishwa kutoka juu kuja chini mengine ni mepesi yakaweza kudondoka yenyewe ,ukumbuke wokovu upo,na kama uliokolewa jana haina haja ya kurudia kwani wengine wanahitaji pia,vingine ujiokoe mwenyewe maana umepewa kila kitu,na Yule asiye nacho kwa kuona hivyo afanye lolote na ataelewa maana, ,maana tena ikiwa wale ambao hawawezi wamepewa nafasi za mwisho kabisa katika kufauru,ikiwa umakini mdogo pamoja na fikra  ndiyo huo unaweza kuwa uwezo wetu.

By:         Benson G.Makaya.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

FIKRA.



Kufikiri ni kuwa na hitaji la kurekebisha jambo,kunatokana na mawazo,kwa hiyo fikra zinaweza kuwa ni mawazo,kufikiri ni kitendo,kurekebisha ni kufanya,fikra hujaza matendo hayo,zikiwa kama fikra halisi huwa haina ulazima ya kuwa iwe vile ama hivi,itakavyo kuwapo ndiyo hivyo,ya kuwa kila mtu ana fikra zake,akiwa na malengo mwanadamu hupanua fikra ili kuyafikia,hiyo yote ikiwa tunaamini kwa yale tunayotaka yatokee katika mandhari yetu ikiwa ni baada ya matendo yetu au yenyewe tunayoyafikiria yatokee ndiyo tutende,tunapotaka kuyafikia yale yaliyo mema,fikra zetu ndiyo huonyesha usahihi wetu,fikra ndiyo zinatutambulisha kwani inasemeka kwa kile tunachokifikiria ndiyo hasa tutakacho kitenda ikiwa tu kimeonekana. Mara nyingine kisionekane kwa Yule anayetenda na hiyo inatokana na kuwa haijulikani,Yule anayetenda  anaweza kuwa na ufahamu mdogo ingawaje yeye mwenyewe akiona anaweza,kwa muonekano  ni wengi tunaweza,ndiyo maana ikawa  fikra zetu zikatutuma mahala na muda tofauti.

Mara nyingi tumekuwa tukikaa na fikra zetu,tukiziamini ndiyo zenyewe,ingawaje vile vya mtu anapewa yeye mwenyewe,ikiwa tunavitenda au tuonyeshe maana ya kile tunachokitenda,mabovu yapo mengi sana,ikiwa na mazima yapo,mabovu ni haya hasa tunayoyafanya kwa kila fikra za kila mmoja wetu ikiwa kwa Yule anayefanya pia naye anasema yake ni mazuri sasa sijui tunayafuata yapi,hata kama sio ya kuyafuata tufikiri tumeyafuata mangapi mpaka hapa tulipo,maana tusingeweza fika katika wakati huu bila kujua ni wapi tumetoka,hata tunapoenda tutayafanyaje hayo?basi tuyaangalie yale machache waliyofanya wengine yakaitwa ni mazuri,maana hata tukiwafuata watu wazuri tutakuwa kama wao zaidi kibaya kinakuja pale tutakapo fikiri zaidi,na hapo tutakuta kuna upande mmoja umetokezea katika upande mmoja ule mwingine wa kwanza,yaani nafsi moja imekuwa kupitia nyingine,na mara nyingine nafsi itakayo iga isifanye vizuri vile ilivyofanya ya kwanza,hapa tutachafua hata wale tuliowaita watakatifu,tutawakuza zaidi wale tunaohitaji kuwaita watakatifu ikiwa hata kwa Yule aliye fuata muelekeo alifuata njia nyingine,ni haki kutumia njia yako pale ufanyapo ili mradi jibu liwe sawa,hii ni katika maisha na sio darasani..maisha ni kama darasa.labda tuone utofauti wa walimu,wanafunzi,majengo na mazingira yote ya shule hii iitwayo maisha,maana kwa upande mwingine mazingira yanachanganya.

Kama shule ilishindikana ni vigumu kwa mtu kumweleza fikra ni nini,sio kwamba haiwezekani,ila inaweza kushindikana kuelewa ikiwa fikra ni tofauti,sio kama 1+1=2 au hesabu ya kinamna yeyote ili lije jibu ambalo kwa aliyefundishwa anajua,au atakuwa amesahau,ikafike kipindi tukaelewe ni namna gani tunaweza kuziendesha fikra zetu,binadamu tunaishi tofauti na hii inatokana na fikra,ikuzwapo fikra ya mtu mmoja ni tofauti na mwingine,labda tuambiane kuhusu ukuaji wa fikra zetu,isije tukashindwa na hili darasa la maisha kwa kutaka tuelewe namna ambayo fikra ya mmoja ikataka tuelewe hivyo,lengo ni kuelewa,na hili kuelewa inakupasa uelewe,vile inavyokuwa tofauti ndiyo njia ya kupanua uelewa,kwani utofauti unakuja pale mtu anapoelewa sahihi,na ikiwa mtu ameiona tofauti basi hataweza kuitenda tena tofauti labda iwe fikra zake zimemtuma,na sio kwa Yule anayetaka kuelewa,kwa wengine imekuwa ni vigumu,wao wakitaka kuelewa namna ile wanavyoelewa wao,tunapofika hapo tunakuwa hatueleweshani wala hakuna maelewano, kwani kila mtu anaelewa lake zaidi ni tujue lipi ni la msingi tutalazimisha kuongea ili ieleweke kuna maelewano lakini  watakaoelewa ni wale hasa wanaolazimisha,maana walikua na nia hiyo ya kueleweka kinamna yeyote walivyolazimisha.

By:       Benson G. Makaya,
Tel:     +255 71 33 66 57.
Email;bensonsmakaya@gmail.com

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...