Friday, June 8, 2012

NAMNA..

Tumeyachagua wenyewe,hapa machache yameongeleka lakini yasipigiwe vigeregere,
usiombe kusubiri,usiombe usubiri,
maana pengine mazoezi yatakuwa makali sana kipindi hicho,
yataongezeka kwa kulingana na muda,pale tukitaka kupumzika bila hitaji letu,

Tukataka kutulia na kupigiwa makelele majumbani kwetu,
pengine tukiwa hatutaki usumbufu,
pengine sisi ni wasumbufu sana,
hapa ni kuelewa,hasa kwa mmoja na mwenzake mwenye uelewa.

Yanayochagulika ndiyo hasa tuliamua kuyafanya,
maana hapo baadaye tukasema ziikuwa ni ndoto,tena tusijue tumeota wapi na lini?
bali tukafananisha si tunaijua jumamosi?ya kila mtu ndiyo iliyo ya kwake maana pengine ilipogeuzwa ilifanyika kwa namna ya kugeuka,

pale itakapogeuzwa zaidi itageuka na yenyewe,
maana muda unasema unataka kwenda na sisi ili na wenyewe ufurahi,
pengine ndiyo maana tunahadhibiwa kwa kutokuwa na muda.
Hapa mengine yaliyochagulika yakawa ndiyo hayo yaliyopita,
si kama imegeuka vilee..tumefikiri sasa bila kujua uzee wa mbao kabla ya msasa,
tutazeeka sana,kama tutapigana na bila  ya hamasa.

MOYO WAKO.

Inapofika wakati isiwe na maana ya kumchagulia mtu,pale inapokuwa imewezekana basi ndipo huwa yanaonekana ya maana,maana hatuwezi kusema usiku ni muda wa kulala na wakati watoto bado hawajala,tukitumia damu hatutaweza kujishafisha na dhambi zetu bila maelewano,na tukataka kuelewana ili hata kwa yule asiyeelewa akaelewe,

Wana jeshi wengi wametuzunguka,matapeli kweli tunawakumbuka,wakijifanya wakihasi hata kwa kuuchoma moyo mkuki,tungalitukitaka kujua jana fulani kasema nini basi ni lazima tukae chini tukumbuke,askari mmoja aliyemdhuru askali mwenzake,maana pale yaliyotoka yale ya moyoni,yalikuwa tofauti sana na vile ilivyokuwa katika kupigana,haikueleweka,pengine hawaelewei,mwanajeshi aliye bora hapigani,mwanajeshi waliye na moyo bora anapigana..ni anataka haki,na haki ya moyo hutenda kile kisichorudikana,hufanya kazi pale ikawepo imesemeka,na hata kufanyika pengine.


Jamani tufuatane,jamani tuungane,katika vigumu vya kuunganisha ni mioyo,iwepo mioyo tukapeana hadi wanaume,pengine ndiyo maana yapasa kuoa,yapasa kuwa na mtu wa karibu japo ya moyoni kabla ya mkuki tukayaskia,mioyo ikiunganika ndiyo pale kunakuwa na upendo,pale tukapendana hata kwa bila ya kuonana.

Moyo wako ukisema vizuri usikilize,maneno yako ukiyaone mazuri yasikilize..tunapotaka kuwa watu wazuri ni tunataka kuwa na moyo mzuri,tukumbuke damu imesambaa kwingi,imeingia akilini mwa watu na pasieleweke ikigombaniwa nini?kama ni pesa ni kuzitafuta na vile ilivyo furaha iyo ni ya mtu,furaha ya mtu anayo mwenyewe,kwa yule anayeitafuta furaha asipoifahamu yake tumwangalie asijeleta vita tukachomana mikuki.

DUNIA.

Walio na kusikia wasikie kwa jinsi dunia na mihimiri yake inavyojizungusha,kutoka pande moja na kuelekea kwengine,labda kwa lugha hii ndiyo itakuwa rahisi'kwani yule aliyeamua kuweka kulia na mwengine aliweka kushoto,wote wakiwa na maana ya kitu kuelekea ila kupasa kuonyesha utofauti na utofauti uliopo ni huo wa kushoto na kulia,hivyo mengine yatakuwa na maana moja,hivyo pegine tukaweza kuelewa kwa pamoja.

Tatizo lije pale chaguzi zinapoingiliana,matatizo yatakuja pale chaguzi zinapokuwa tofauti,ikiwa imechagulika vyema kwa kupatiwa maana yake,na nyengine ikaonekana sio njema kwa vile na chaguzi lake,hapa na pale mmoja akataka kushoto na mwengine akaelekea kulia,hivo ikiwa ilifikirika kwanza.

Katika  kuelekea kuna kuchanganya,katika muelekeo labda tupate njia zile zilizo pana,ili pa kupumzikia pasije pakawa na uhaba,ya kila siku yakatendeke yakiwa hata ikawa mara saba,tusameheane kwa hilo,tusameheane hata mara sabini,na ndiyo maana ya kuweka umahala,ndiyo maana pakawa pakawa.kote pamekuwa ni sahihi,fanya wewe,anza wewe.

Haja ya kulia na kushoto ni mengi,ya kati yale yanayosimama,kwani tunaweza kusimama kulia lakini katikati.kulia na kushoto ndiyo kumetofautisha,tufanye tuchukue vyote hata katika maumbo,hata tukalizungusha tukipeleka kulia na baadaye litakuja kushoto,hivyo ni kuwa makini hasa kwa pale tunapokuwepo,inazunguka na baadaye kushoto kukawa nyuma na kulia mbele,au kulia nyuma na kushoto mbele.
Tuelewe kwa mduara uliopo,maana hata ikaelekea kushoto yaweza kuelekea na kulia,inajizungusha..

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...