ONA ni vile kwa namna uliyoumbwa
ili kuweza kuvitambua vitu kwa urahisi,kwa kutumia macho yako umeweza
kuona vingi sana,na kila kimoja kikiwa katika maana yake ya utambuzi kutoka kwa
yule muonaji.Kutokana na utofauti wa maumbile ambao uko mbali na usawa wa
kusema kuwa wote binadamu tu sawa,kama wengine walivyopewa macho kwa pengine
wale wasioona mungu anawalinda kwa namna yao,na ndio maana maisha yakaendelea
na vitu vyote kuonekana kama vilivyo,kila jicho
litaona imeandikwa kwa namna iliyopo na itakayokuwepo,kwa yeyote anayeomba
msaada anakuwa ameshindwa,lakini kwa nguvu ya mpambanaji hata kuomba msaada ni
kupambana maana iliandikwa kwa yule atakayeomba atapata,
Hapa huwa inakuwa ni kama haujaona,kwani pale unapopata unashindwa kufanya na hatimaye kupotea,kwani wengine wanahitaji kuona pia,yule aliyekosa miguu atembelee mikono na ikishindikana atafute namna,unaendelea na safari,yule anayeomba,asirudi na kesho ya kuwa aliona jana,ikiwezekana kifichwe maana itazoeleka,ikiwa sio roho mbaya yule aambiwe nenda katafute,vipo pale hata kama havipo basi aelekezwe njia.Ubishi ndio huleta upofu,maana mbishi hataki kuonekana ameshindwa,zaidi ni kwa namna ya yeye atakavyojifanya HAONI..

Kuna mengine sio lazima kuyaona,maana yatabaki kwenye mboni za macho
yako na kwenda ndani ya mwili,kwani hata wachache utasikia “yale mambo yamemwingia damuni” ,hapo
watasema wao na unahitaji kuya POKEA,ikiwa kwa kuona yatakuwepo mpaka katika vidole vya mguu kwani kule
ndio mwanzo kuliko mwisho.Viungo vya mwili sio vya kutufanya ushindwe
maisha,ikiwa ni kichwa kwa ujumla,mikono,na vinginevyo,ikiwa mtu hasikii ndio maana
ya kujua kusikia,kwani hata umuulizapo mtu asiye sikia anatamani nini naye
aseme ‘kusikia’maana hata akawa ametamani kusikia vizuri ni nini hasa
ulichomuuliza.
Ni kweli sio wote tunaosikia,na hapa ieleweke sio wote tunaoweza kupokea katika muda muafaka,kwani ikiwa sauti imetoka watakaosikia ni wale waliohitaji kuipokea sauti hiyo,iwe wanasikia au hawasikii.Wale wanaosikia lakini wanaweza wasisikie endapo pale mtu ameongea na kama ni ililetwa zawadi basi watapata wachache kwani kuna wale walio iona zawadi,wengine walisikia lakini wasijue ni zawadi gani na kuna wale walioitiwa zawadi ikiwa kila mmoja na yake,wale watakao pokea si tu ndio wale walio itiwa zawadi kwa maana ni za kwao.endapo mtu amekosa zawadi na aliitwa basi ajue ni huwa inatokea hiyo,hata maisha ya kwako si ya kufananisha na mwenzio.

unapopokea yakupasa upokea kwa shukrani,labda usiwe umezipenda zawadi
zenyewe,na hata iwe hivyo zitakuwa za kwako tu,kinachotoka machoni hupita na
moyoni kabla ya ruhusa ya kutoka nje,moyo unapopokea ni inapasa kuushirikisha
na ubongo ili kuweza kujua kama ni imetambulika pia ni haki,moyo wa mwanadamu
haufai kufuga uchafu labda uwe wa mtu wa namna hiyo.Mwisho ni matendo,yawe
yanatoka moyoni,ikiwa moyo wako utajulikana kutokana na matendo yako jua unapotenda ni kama pale unapoongea,unapoongea una TOA yaliyopo moyoni na
kuyaweka katika mazingira ya kawaida,ingawa hata ya moyoni ni ya kawaida kwa
wengine katika mazingira hayohayo ya kawaida,ikiwa haionekani kwa macho lakini
ni macho yaliyopelekea akilini,hivyo yapasa kupumzisha akili,kama vile unapopumua kwa kutoa na kupokea hewa ili uendelee kuishi,labda imekuwa nzuri kutoa kuliko kupokea
ya kuwa unaotoka ni uchafu.
'ona sahihi,pokea vyema na utoe kwa moyo mmoja'.
By: Benson G.Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com