Sunday, September 23, 2012

KWA MUDA MFUPI...


Ni wazi mandeleo ya mwananchi huletwa na nafsi yake mwenyewe,hii ikiwa ni katika kuamua endapo kuna  jambo lifanyike ama la..na ikiwa imechagulika na ieleweke,maana pengine  ni  kwa faida ya wananchi,na katika faida ni lazima isiwe na kudanganya toto,na endapo imekuwa bila ya kufahamika basi hiyo ni sahihi maana hata sisi wenyewe tunaishi kwa muda mfupi tu,na pengine kupitia wengine yaweza kuwa ni kwa faida yao tu,maana kama unajijua unakaa kwa muda mfupi ujenge ya nini?

Hapo kwenye kujenga yatasemeka mengi,maana kwa vingine ni lazima kufikiri endapo kuna tegemezi na hiyo ikaeleweke kama ni la muda mfupi ama kudumu,vinadumu vyote lakini si nafsi ya mtu mwenye mawazo mafupi,utanenepa kwa kuwa unakula,utakula na usinenepe kwa kuwa haujaridhika,tena maswala ya muda mfupi yakiwa yanakuchanganya.

Fikiri kwa muda mfupi ili kuweza kueleweka kwa kuwa wengi wanataka majibu,usikurupuke ya kuwa muda ni mfupi ikaja ndiyo sababu,hata yale yaliyofanyika ni namna ya kutaka sababu endapo yakauliziwa,kesho tutaendelea kulalama kwani wale wa kwanza muda wao unaelekea kuisha,tungalikuwa na thamini na yale yanayotutegemea,hakika hata  muda mfupi usingekuwa ni sababu.

MAISHA YAKO.


Unapofanya hivyo unasogeza namna ya kupokea vyema ikiwa katika muda mwema,na katika vitu vya kuzingatia katika maisha yako pengine ukatafuta mtu au watu mkawa mnashirikiana katika mambo mnayofanya na kukuta kuna kusema maana vizuri vinakatisha tamaa kwa kuwa mwanzo unasemeka ni mgumu,unapokuwa na lengo ni vyema kutumia na nguvu zako kwani katika baadhi nyingine ya kuamini ikiwa nikutafuta na kutaka kujua wewe ni nani na pengine nini kilichopo ndani yako.zile nguvu zako ndiyo zinaashiria undani wako.ikiwa ni kihalisia zaidi.

Leo utasema ya mwenzako lakini ya kesho ni yako,maana haukuyasema jana,hiyo ikiwa ni namna ya kunyimana,pengine isifahamike kwamba hata ile iliyo ndogo haipo,kwa iliyopo kuonekana kama ni nyingi kwani umejaribu japo kujipendezesha na uturi pia,kesho inayokuja ndiyo hiyo ya hukumu yako,maana wengi wametegemea samahani kutoka kwako.

Maisha yenyewe yako wapi?Ni usemi tumeusema,tumeuskia.hapo ukiwa umeona tofauti na kile halisia maana kama ulinyimwa na ni bora kusema pengine wengine walijisahau.ndiyo maaana ya kesho kuja na kusema samahani.unapojinyima una maana ya kutengeneza,ama pengine ukanyima na kukuta unafanya mbadala wa kutengeneza yaani kubomoa ,hapo ikijengeka chuki,Chuki ni kama upendo maana upo katika maisha ya kila mmoja wetu,asiyekuwa nayo sasa ni kwa sababu ya muda na maisha yake.maisha yako ni tofauti na ilivyo.ni swala la kutambua tu.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...