Friday, April 19, 2019

UNAPOWAZA

Eti kuwaza sana ni vibaya,nawaza sana nakuwa na mawazo nawaza sana yaliyo mema nawaza sana kuongeza kupata maisha sio kama ya fulani bali yale niliyoyawazia,wakati mengine yanapita Shukrani kwa muumba hazitaweza pita,Mwisho wa kuwaza unaelewa mwenyewe maana sio uwaze tu hata yasiyo na majibu,

Mbaya katika mtihani ni kuanza na swali gumu kuliko yote  kumi utajikuta umefeli na kuyashagaa matokeo yakakupa mawazo tofauti  yakuwa kabla ya kuingia katika mtihani uliwaza ukitoka utakuwa na mawazo tofauti zaidi ya yale uliyo kuwa nayo sasa,sijui niwaze nini nikufurahishe, nakusema siwezi ogopa ila muda haumdanganyi mwamuzi labda anayeamua akaamue.

Hivyo unachagua wewe,chagua wewe kuwaza nini mengine ni  mazuri asikwambie mtu mawazo mabaya,ni kheri akakuongezee kwenye huo ubaya maana hata moto anaoupata yule anayechomelea na  yule anayekaanga viazi ni tofauti nawaza tu,ukitaka kutokuwaza fanya starehe,ukifanya za kutosha na hautakuwa na mawazo ya kutosha,naposema starehe kila mmoja anayo katika mawazo yake  unawaza kufanya starehe gani nasema hivyo maana kuna kauli inasema maisha ni mafupi sana hivyo inakupasa kuishi kwa thamani,matumizi yako yakaendane na mawazo yako ila pindi unapowaza kinyume huna budi kuwaza yaliyofanyika maana huo hua ni mwanzo wa mmomonyoko wa yale yanayofuata.

ukiwa unawaza yanayofuata ukawa hujui hasara yake maana kwa muda huo yanakuwa hayana mashiko na mmiliki yaani wewe uliyestarehe kwa mawazo yako kabla hujawaza sasa iliyopo ambayo ni baadaye.

Sikuwaza umri ni kama haya makubwa  ninayoyawaza,wala kuna mengine sijawaza lakini yamekuja katika haya,mawazo ukiyaamini,yanakuletea imani yako inachokiwaza hata ukajiandae na utofauti ili kutokuyazidisha yaliyopo,maana nawaza sikufika hapa kama nilivyo wala sikuwa mimi kama nilivyo,sio tu kwa sababu ya nini ama fulani nikiwaza kwa mawazo yangu ni imani maana sikuijua kesho zaidi ya yule aliyeniambia niache kufanya ya kesho kwa kuwa hata usiku wa leo hayajafanyika.

Unapoona mengi kuna mengine yanakuwa sio makubwa yaliyowazwa zaidi ya kuonwa ikiwepo vingine nawe ukawaze hivyo,nikikiona nakielewa zaidi maana nikikiwaza ntakuwa kama nakiona,shida pale nawaza nisichokiona ninapowaza cha kesho na leo sijaimaliza hapa huwa naamua kufanya lililopo bila ya kuchelewa.

Kuna kucheleweshwa lakini aliyewahi kawai kesho ujifunze kuamka mapema ili kuyawahi mawazo kingafu ,maana kama mawazo yanaingiliana basi hata matendo pia,unapokufa wakisema utakumbukwa wengi ni kwa matendo yako,mengine waliyoyawaza husahaurika ,kufa leo uache mazuri yaliyotokana na mawazo yako na iwe kwa faida yako.

Nawaza ni kheri nizeeke muda mwingine ntakuwa nimepita mengi,nisionekane tu kwa mtu anayeona aonavyo bali nikajifiche kwa vile waonavyo,nilikaa na kuanza kuandika haya nliwaza mmoja atawaza yale ni mawazo tu,lakini kwa jinsi navyoona hata yule asemaye naye anataka kuonekana na mawazo bora,kuna vitu Mwenyezi Mungu amekupa na mwengine hana,Kama unaweza kufanya chochote bora fanya katika ubora uwazavyo.


KATAA


Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika  hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofauti na vile inavyoweza kusukumika,upepo  unaweza vuma kuelekea kusini na yenyewe maisha  yakataka uelekeo wa  magharibi  itakuwa na kueleweka vile inavyoonekana uelekeo ulivyo.

Unaweza ukawa umekatalika upande wa kushoto lakini kulia ukafanya kazi na kama vile ilivyo katika viungo vya mwanadamu,wengine wakatumie  kufanya mambo yao kwa upande wa kulia na wengineo  kushoto yaani pande zote na hiyo ikawe ni kulingana na mazingira ya jinsi ulivyoweza kuumbwa.

Unapokataa jambo ni lazima ujue kipindi cha kukubali pengine muda unaolikataa jambo ndiyo muda mdogo wa kusubiri na kupata jambo lingine likiwa ni lile lililokataa  uelekeo ama ni  jipya,yule aliyekataliwa jana na sasa anang'aa ni katika maisha ya mwanadamu huwa yanatokea,

Yote sio ya kumwachia Mungu Mengine hata yeye aliyakataa akaumba Amri ili uweze kujikataa katika nafasi uliyopo pengine ikiwa na mahitaji ya mabadiliko ama vinginevyo,ingawaje yaweza kupelekea kukataliwa na jamii na watu wanao kuzunguka lakini kataa kukataliwa kwa sababu ya maono ya watu,

Wengine wakadhani umejikataa lakini ni namna ya jinsi maisha yako umeyataka yawe,unapokaa chini ona waliokataliwa wakakata kutokukatalika,maana kuna vile vingine hukataliwa kwa sababu anafanya fulani.

Muda mwingine unaweza kudhani hata ulikosea kufanya kile unachokifanya au ulikosea kuoa,ulikosea kununua mashine fulani hata pengine ulikosea kumwambia mtu fulani jambo fulani na mengine mengi.Kile kinachosukuma mwelekeo kinatagemea uwiano wako na ukikataa kwenda kulia na msukumaji anasukuma kushoto basi jua utaenda kushoto tu.

Sio kila sikio linasikia kile chema kinachoweza kupitia mdomoni baadaye,midomo mingine hukataa kutoa tafsiri sahihi ya kile kilichokipokea kwa kuchelewa kufika taarifa ama kukataa kufikisha kile kilichotafsiliwa na kukifikisha kikiwa na maana tofauti inayoweza kukatalika.

Ingawaje hata kukataliwa kuna faida zake pia usijisikie wa chini pale unaposukumwa na mkatazo,kataa wewe kabla hujakataliwa,yule ajaye kakukataa atapata sababu baada ya wewe kujua kujikataa kwa faida.

Usijisikie hali yoyote katika kukataa,kukatalika,kujikataa ama kukataliwa pengine fikiria matokeo yake kwanza na ukajua leo yangu iliyokataliwa ni Nuru yangu kesho na hata kama kesho  yako inaonekana kukataliwa kataa mawazo ya kuona kukataliwa.


Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...