Tuesday, July 24, 2012

HAPO ZAMANI..

Sio lazima kuuongelea wakati uajo bila ya uliopo,ni watu tuliopewa hali,mali na utambuzi mkubwa sana juu ya dunia hii,inapofika kipindi haujajua kuhusu hali au mali basi jaribu kuelewa maana ifikapo baadeye hiyo itasemeka ilipokuwa zamani,zamani ilikuwa ukiamshwa kutoka kulala ni kula ama uende shule,nikiwa nazungumzia vijana wazee ni vigumu hata kukumbuka enzi zao.

Tulivaa vizuri bila majina yetu ya kisasa,zamani bwana ni kama majumba ya kitasha,maana utakutamani kama vile kwa mwizi pale mlango unapokuwa hauna kitasa,tunaenda tunafikiria mbele,tunaenda tunaangalia mbele,naipenda sana hii namna ya vijana wa sasa,maana wale wazee wa zamani walitabiri mavazi yao,na kama ukifuata matakwa yao jiandae kuwa maana watu wamekuwa zamani.

Zamani kuna mengi ambayo hata hayasemekani,zamani hata sitaki kutamani maana nikikumbuka ni sawa nguvu kuirudisha imani,kuna watu wa kisasa wana akili chafu sana,hii ikiwa ni tofauti na zamani,kwani kwa kuwa na muonekano mpya na akili za zamani,ama tuseme akili za nje lakini mwili ndani,hatari sana tukilinganisha ya sasa na zamani.tutaenda kwa imani tu.ya zamani ni mengi,hapa yalikuwa kama chenji tu.

KUSUDI


Unaweza kufanya jambo bila hali yoyote,maana kutokuifikiria na hata ikikatalika mwanzo mwishoni ukikosea utasema samahani,kwa sababu unafanya bila hata ya kuuliza,ukasema haukujua kwa sababu haukusikia mahala pengine,kumbe unafanya maksudi,maana kama kosa linakujaje na mwalimu yupo katika mahala husika,Pengine mwalimu hajui kufundisha.

Unapokaa chini labda ujiulize ni kwa sababu gani unapenda,na hapo utausingizia moyo,na baadaye useme kuwa moyo wako unauma,ya kwamba haujiskii vizuri,kumbe mwanzo ulikuwa unakujiskia vizuri. kumbe haujielewi,haukujielewa ni namna gani furaha unayoitaka unaweza kuipata,yapasa kwenda mahala fulani,yapasa kuthubutu kwa kuufahamu uzuri wa ua mwanzoni,na mwishowe unaweza kuona kweli lile ni ua,lakini baadaye ni lazima kuelewa   unafanyaje na hilo ua.

Kufa ni lazima hata maana yahitaji ua  kumwagiliwa na sio kukukaukia,mapenzi yamejaza matunda yote,maana hata kama ni mgonjwa anachagua lile alipendalo na usipojielewa hutapenda,ni maana ya kutokujua asili ya mapenzi yako labda haifai kuumiza wala kuumizwa pale unapopenda,na hii haina maana viongozi kutowapenda wanawaongoza

Mengine haya ya leo unalaumu kwa kukosewa,bila kudhani ya jana wamefanyaje,maana ni yale yale tu,na kama kubadilisha basi haina maana ya kushindwa,labda kuwapa miji kwa wale wa maksudi,kama ilivyo maksudi huwa haiumi,mtu anaweza tenda vyovyote,hasara ya mwanzo yaipasa kuibeba,kwani walishaamua kufanya maksudi,Angalia kesho yako inakujaje maana mambo yanaweza kubadilika tena na kudai Pumziko la jana.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...