Unaweza kufanya jambo bila hali yoyote,maana kutokuifikiria
na hata ikikatalika mwanzo mwishoni ukikosea utasema samahani,kwa sababu unafanya bila hata ya kuuliza,ukasema haukujua kwa sababu haukusikia mahala
pengine,kumbe unafanya maksudi,maana kama kosa linakujaje na mwalimu yupo
katika mahala husika,Pengine mwalimu hajui kufundisha.
Unapokaa chini labda ujiulize ni kwa sababu gani unapenda,na hapo utausingizia moyo,na baadaye useme kuwa moyo wako unauma,ya kwamba haujiskii vizuri,kumbe mwanzo ulikuwa unakujiskia
vizuri. kumbe haujielewi,haukujielewa ni namna gani furaha unayoitaka unaweza kuipata,yapasa kwenda mahala fulani,yapasa kuthubutu kwa
kuufahamu uzuri wa ua mwanzoni,na mwishowe unaweza kuona kweli lile ni
ua,lakini baadaye ni lazima kuelewa unafanyaje na hilo ua.
Kufa ni lazima hata maana yahitaji ua kumwagiliwa na sio kukukaukia,mapenzi yamejaza
matunda yote,maana hata kama ni mgonjwa anachagua lile alipendalo na usipojielewa hutapenda,ni maana ya kutokujua asili ya mapenzi yako labda
haifai kuumiza wala kuumizwa pale unapopenda,na hii haina maana viongozi
kutowapenda wanawaongoza
Mengine haya ya leo unalaumu kwa kukosewa,bila kudhani ya
jana wamefanyaje,maana ni yale yale tu,na kama kubadilisha basi haina maana ya
kushindwa,labda kuwapa miji kwa wale wa maksudi,kama ilivyo maksudi huwa
haiumi,mtu anaweza tenda vyovyote,hasara ya mwanzo yaipasa kuibeba,kwani
walishaamua kufanya maksudi,Angalia kesho yako inakujaje maana mambo yanaweza
kubadilika tena na kudai Pumziko la jana.
No comments:
Post a Comment