WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.. NI mshiriki wa EPIC BONGO STAR SEARCH ANAYETOKEA MBEYA,HIVI SASA AKIWA KATIKA FAINALI HIYO ITAKAYO FANYIKA DIAMOND JUBILEE IJUMAA TAREHE 9 MWEZI HUU..HAYA MACHACHE KUTOKA KWAKE MWENYEWE WALTER...
"Nashukuru sana watu
wangu, ni Maombi na Kura zenu tuu.. Nashukuru kuingia FAINALI na nakuomba
endelea na moyo huohuo kwa kunipigia kura kwa kuandika neno EBSS12 kwenda namba
15530".
Hiyo ni status aliyoiandika
Walter katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter jana baada ya kurushwa kwa
show yake ya nusu fainali iliyompelekea kuingia fainali itakayofanyika Diomond
Jubilee, Ijumaa ya tarehe 09/11/2012.
Pamoja na hayo Walter
aliongeza kuwa anamshukuru Mungu na watanzania kwa hatua aliyofikia kwani
haikuwa rahisi kihivyo.
Pia Walter ameongelea suala la
yeye kuwa amnatokea Mbeya kwani ni jambo lililokuwa linachanganya watu wengi.
"Mimi ni mzaliwa wa Mbeya na naishi huko na mama yangu na
wakati wa audition za EBSS nilikuwa nipo Dar katika michakato yangu na ndio sababu
nikasailiwa kama mshiriki kutoka Dar".
Aliongeza, "Naomba watu wangu waendelee na moyo huo huo wa
kuwa bega kwa bega na mimi na waendelee kunipigia kura kwani kura ndio kila
kitu hata kama nitapendwa vipi"
Walter ni mshiriki aliyeingia
FAINALI pamoja na wenzake wanne, hivyo washiriki wa EBSS waliobaki katika
fainali ni Walter, Nshoma, Nsami, Wababa pamoja na Guiter gira Salma...
Ili kumpigia kura Walter
Chilambo, andika neno EBSS12 kwenda namba 15530".
No comments:
Post a Comment