Monday, November 5, 2012

CHUNGA KAULI..

Hata zikiwa nyingi wachache hutaka moja tu kauli kuielewa,kwa kujua kwa yale mengi hakuna wa kuyaweza naye.ukisikia kauli lazima uishike isiwe kauli  nyingine zikasahaulika,ama ikaonekana vile walivyosema wengine,kwamba kauli ya mtoto kumwambia mkubwa yaweza kuwa makosa ki heshima,lakini siyo ikawe mkubwa kwa mkubwa mwenzake,ikawa si hekima,maana itaoneka dhambi kwa kujaribu kuyafanya ya juani wakati kauli nyingine ni za gizani.

Ni wazi hakuna lililo sahihi zaidi yako Mungu,kwa Yule anayebisha ni sawa na kufananisha ndiyo na hapana ,ukikaa na kukuwa bila kuelewa utanawa sana kichwa kwa kupata moto tena hutaelewa nini cha kufanya pengine ukiwa haujafanya kitu hapo mwanzo lakini kauli zako zikakukuponza.

Ninatoa kauli yangu pale inaponibidi ikiwa nazijua haki zangu,akili yangu inajua cha ziada nje ya mwili kinachoendelea,hivyo kauli yako yaweza kukuliza ikiwa hujachukua dhamna ya kuyabeba majibu yatokanayo na kauli zako,ni mizigo ya ndani,wachache wanafunzi huelewa nini mwalimu anachofundisha,maana kila mwanafunzi anaelewa yake pale inapokuwa nafasi na wakati wa  kila mmoja kutoa kauli yake katika uelewa

Ni kweli kauli nyingine ni makosa sana kutamkwa,si vyema kusema kitu usichokifahamu na kugeuza kauli yako ya kweli,ni wazi hata samahani isimaanishe kitu hata ikawe kwa mtu kuuana na mwenziwe.kauli nyingine hazitakiwi kukumbukwa,kauli nyingine zina maana ya kuleta kauli nyingine zisizo na maana.Chunga kauli.


No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...