Friday, September 21, 2012

MTIHANI...

Jirani karibu maana ninatafakari kwa yale yaliyo ya mbali, Tukibadili lugha tutaelewana tu ya kuwa ni mtihani,na kama kuna kuishi ni lazima kuufanya,leo umekuwa mtihani baada ya kutaka machache yaliyo kwa wachache ,leo umejuaje kwani  mungu naye ameleta lake kwa kuwa pengine wengine wanaweza kushangaa kwa kuwa hata wale wa mbali waliweza kusema ni hiyo ili iliyo ndogo  ikaeleweka kuwa na muelekeo wa kusema kwamba mimi hii ni yangu ili kulainisha lazima.

Kiswahili ni lugha ambayo hata mwelewa akasema haleluya maana ni lugha ya dini katika utaifa wa namna yoyote,wale wa kwanza katika kuanza ni wale wanaotaka kuwa wa kuelekeza katika namna ya kuelekeza kwamba unaweza,maana kuweza kunahitaji uwezo wa mwendo wa kusimamisha ili kimo kikaeleweka .

Tunarudia na kusema,Kile nini unachokifanya katika maisha yako ni juu yako mwenyewe,kifahamike au la,pengine usiishi kwa kusema kwamba ukitaka maana,vingine vinavyokuwa tofauti ni tofauti zenyewe maana hata unapochanganya ni sawa na kuuleta ugumu wa tatizo katika tatizo lenyewe,ikiwa hata mwalimu anakosea kusahihisha,hapo kuna kujiona mjinga kana kwamba kama ni kazi basi wamefanya wengine kwa kupitia wewe.sio kukupitia bali ilikuwa ni mitihani tu.

MFUMO WAKO


Leo umetaka kuongozwa na nani maana inaashiria mfumo unapajua  unapoelekeza ,pengine ikawa vyote ni vya kijani,kwani kwa vile vinavyosemeka vikiwa na lengo la kufanyika hali kadharika ikawa ikifikirika tumbo la kila mmoja ili ikaeleweka imependeza,maana kwa sasa usipofanya wewe utakufa masikini,hivyo watu wameamua kunyanyuka na kusema nataka bila ya kujua shauku hasa la mioyo yao,maana siyo kila njaa inahitaji chakula,fikiri umeijua njaa yenyewe?pengine hata na chakula chenyewe kiwe tofauti basi.

Ni wazi zinalika,ni wazi utaifa unapotea kwa sisi wenyewe.ikiwa ni kweli wananchi wapo makini,ikiwa ni kweli viongozi wapo makini,hapa hakuna aliyemkosea mwenzake kwani hata Yule anayeongozwa afikirie kuongozwa,zaidi ya kutaka kuongozwa vile unavyotaka ni kutaka kuwa kiongozi.kama umelima mchele na umevuna mahindi jua shamba si lako,na kama uliweka alama ya kusema usipotee basi mshukuru mungu wako kwa maajabu ,maana yatakuwa yamtendeka.la sivyo badili mfumo wa kulima.

Mashati hata tukishikana yatachanika na tutabaki watupu,bila kuelewa mfumo haitawezekana kwenda mbele wala nyuma,wewe ambaye upo katika mfumo ndiye utafahamu maana na mfumo wake unaweza kuwa umeelekea kule unapouelekeza au ulipoelekezwa bila kujua kama unaendana na mfumo wako,maana pengine kwa wengine ikawa ni lawama kwa namna ya hali ilivyo,hizi siasa zinaweza kubadili hata mfumo wa maisha yako.Wenzetu wanatumia lugha’system’kukiwa kuna kila aina ya maana ya neno hilo kutokana na yaliyopo.

BADILI MFUMO WAKO BADILI MATENDO YAKO

ZAMA ZA SASA.


Inapofika wakati kitu kimeharibika huwa inaleta matatizo  katika mazingira hasa ni kutokana na kutokutegemea kwamba kama zama  za sasa si kama zile za zamani,ni wazi nimekubali tekinolojia,ni wazi nimekubali mabadiliko Ni technologia,ikiwa nataka kubadilika na kwenda na mambo ya kisasa,ali mradi ieleweke na ijulikane kama kuna uwezekano wa kufanyika kwa jambo,isiwe imepitiliza kwa kuwa Wakati mambo yaliyotendeka yalitokana Na kile kinachofanyika zama za mda wako huu.

Imekuja kipindi sasa najenga uchumi wa  mwenzangu bila ya kujijua,maisha yangu nimeyafanya bidhaa ya bei rahisi ni si kama zile za kwake anazozitengeneza kwake,maana nimeletewa mng’ao ili nijue kinapendeza,najenga huku nabomoa na ifikapo kipindi najua kutakua hakuna namna ya kuona tena mbele kwa kushikwa akili na mwanga wa vile vinavyong’aa kupotea,pengine kuongezeka umaarufu katika hitirafu,ikiwa nimeruhusiwa kuwa dereva wa maisha yangu.haki taifa linapotea kwa kile kidogo cha zama za leo,maana kila mtu anaminya jicho moja anakuangalia  na anafungua la pili anakula vyake.

Zama za sasa inaonekana ni wazi vyakula vimepungua,ardhi wanalima wageni maana wenyeji mmelima sana.tena mara ya kwanza walikuwa wakilima na kujenga,labda ndiyo wanaanza kujenga tena.maana katika maamuzi ya kiongozi mmoja yanaweza kukupa uhuru kama yanavyowaza kukupa vita na kukunyima amani kwa kiongozi huyo huyo,hapa ikiwa tujiongoze,zama za sasa ni za ukweli na uwazi,hizi ni zama zako

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...