Ikiwa mungu ni kila kitu na wa kila mtu,mwanadamu amepewa uwezo
wa kuweza kufanya maisha yake,kufanya maisha yako ikiwa siyo kujaribu,yaani
kutokuwa na uhakika wa kile unachokifanya na baadaye ukaja muda ukasema
unajaribu,hata ingali ikafika kipindi wakubwa watalazimika kufanya vya watoto
na hii ni kwa sababu wakubwa waliwaambia watoto kwamba usifanye kile cha
wakubwa.katika kufanya maisha hakuna kujaribu na ili ueleweke unaishi ni lazima
kutumia nguvu za lazima.na wala siyo lazima kufanya ulazima huo ikiwa haina
ubishani katika kila mtu anapofanya maisha yake
Haikuwa na maana kwa mtu mkubwa kavaa nguo za watoto,maana
hii ni fashion,ama ikawe jitu kubwa linataka sifa za kitoto.maisha hayana ngoja
wala subiri,leo ukiwa mahala fulani fikiri kama na jana ulikuwa hapo,jua mwisho wa
maisha ni pale utakapo kuwa hau ishi tena,hakuna mtu wa kuweza kuishi maisha ya
mwenzake,ikiwa chaguzi la mtu ili kueleweka ameishi siyo lazima awe na kile
wewe unachokitaka,unaweza kutumia nguvu kulazimisha kuota ndoto uliyoota jana
ya kuwa ilikuwa nzuri sana na kujikuta umechelewa kuota ya leo,unaweza sema yote hayo ya
mungu ya kwako fikiri, fanya yanayotokana na maamuzi yako
Kumbuka umeletwa duniani
ili uishi,umeweza fanya mengi kwa nguvu zako na baada ya kumaliza akatajwa
Mungu hapo ikiwa uliweza,toa nguvu zako..jiamini wewe ndiyo wa
kufanya lile la lazima,ikiwa furaha ya maisha yako ni wewe mwenyewe,hauwezi kunywa
pombe na kuiomba ‘KILEVI’ kikuleweshe kidogo,unasahau pale unapoanza na kukumbuka
mwishoni kwani utamu wa mwanzo huonekana pale nguvu zinapoisha,siyo lazima
kulima ikaeleweka unanguvu nyingi na haujaja kujipaka rangi ili kuonekana umpendeza,maana
utapaka rangi zote na kujikuta umekuwa na rangi ya kopo la kuchanganyia mara nyingi huwa inakuwa haieleweki.
NI WAZI KILA MTU ANAJUA,HIVYO KAMA UMESHINDWA KUELEWA VINGINE FANYA UNAVYOJUA WEWE ILI KUSIWE NA LAWAMA.