Monday, June 25, 2012

KAULI YANGU...!!

Mengi mengi yasiwe na haja ya kuyapitia,mengi pengine isije kuwa kwamba nimeyapitia,inapofika wakati haina haya ya kusumbukia,inapofika wakati ina haja sana ya kuyasumbukia,pengine ni machache yaliyo na kwingi kwa kutokea mengine ni machache yasioeleweka kwa wengi waliotukia,maana kuwapo sasa ni kuingia humo,tena ikieleweka imetokea wapi,hapo tukaja kuogopa ajabu zaidi,maana isiwe maswali kwa kuuliza,wala isije kuwa majibu kwa kujipatia,hapa hatutaelewa hata hayo machache yaliyo na kwingi kwa kutokea,mwalimu anasema a shika hapa,soma na uelewe,mwalimu akiwa na darasa pale darasani,hatujazoea nini kama kwani 'practical' tunafanya darasani?

Mengi machache yalitangulia,yalijua yanakuja haya sasa,kwani kwa kipindi kinapoingia ndiyo pale mengine tutaweza kutamkia,tena nikasema nimependeza sana,tena ukasema umependeza sana,haapa nafsi yako lazima ikubali,tena ipende kwa kuelewa imekubali nini,haya machache yamesemekana kuwa na uwalakini,labda tusubiri mengine yatakuja na umakini,hatujachelewa sanaa kwa kutaka kuyajua,hapa ni mwanafunzi na darasa kwa maana ya kusubiria lile linalokuja,kwani ni mwanafunzi alitaka aende la juu na amalizie na la chini,maana hapa tukisema saba mpaka moja wengine wana nane,kweli tumependeza sana,maana sisi wote wa usiku na hata wale walio kuja mchana,tukisema chukua haina maana ya kusema tumeibiana,pale au hapa tunakuwa tumeibiana,pengine maneno hayana maana,pengine ikafika mchana ukafanya ya jana.

Nimezunguka sana wa kesho kutwa watafahamia,wengine walikuja na kusema eti kwa nini sijafanya vile,labda sikuwauliza kwa nini nimefanya hivi,pengine kwa kukalili ndiyo ikaeleweka,hapa wakiwa wameshika machache ya mdomoni bila akilini kuyafikiria,sijui wala isiwe swali kwa kusema yangetokaje,maana bila kutazama itakupasa ujijibu mwenyewe.nasubiri vingi na haki yangu ntendewe,maana ya kuwa nayo ni vile inavyotendeka,hatuwezi kuwa na akili tukaziweka tukasema pale kakosea,wapi kapatia na mbona hukusema?hapa tutaingilia mlango wa chooni,maana hata huko mbele kulivyo kaa kaa ni kama vile imewekwa,si ni njia fupi…basi yapasa kuweka miba.pengine njia itaeleweka.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...