Mengi mengi yasiwe na haja ya kuyapitia,mengi pengine isije
kuwa kwamba nimeyapitia,inapofika wakati haina haya ya kusumbukia,inapofika
wakati ina haja sana ya kuyasumbukia,pengine ni machache yaliyo na kwingi kwa
kutokea mengine ni machache yasioeleweka kwa wengi waliotukia,maana kuwapo sasa
ni kuingia humo,tena ikieleweka imetokea wapi,hapo tukaja kuogopa ajabu
zaidi,maana isiwe maswali kwa kuuliza,wala isije kuwa majibu kwa kujipatia,hapa
hatutaelewa hata hayo machache yaliyo na kwingi kwa kutokea,mwalimu anasema a
shika hapa,soma na uelewe,mwalimu akiwa na darasa pale darasani,hatujazoea nini
kama kwani 'practical' tunafanya darasani?
Mengi machache yalitangulia,yalijua yanakuja haya sasa,kwani
kwa kipindi kinapoingia ndiyo pale mengine tutaweza kutamkia,tena nikasema
nimependeza sana,tena ukasema umependeza sana,haapa nafsi yako lazima ikubali,tena
ipende kwa kuelewa imekubali nini,haya machache yamesemekana kuwa na
uwalakini,labda tusubiri mengine yatakuja na umakini,hatujachelewa sanaa kwa
kutaka kuyajua,hapa ni mwanafunzi na darasa kwa maana ya kusubiria lile
linalokuja,kwani ni mwanafunzi alitaka aende la juu na amalizie na la
chini,maana hapa tukisema saba mpaka moja wengine wana nane,kweli tumependeza
sana,maana sisi wote wa usiku na hata wale walio kuja mchana,tukisema chukua
haina maana ya kusema tumeibiana,pale au hapa tunakuwa tumeibiana,pengine
maneno hayana maana,pengine ikafika mchana ukafanya ya jana.
Nimezunguka sana wa kesho kutwa watafahamia,wengine walikuja
na kusema eti kwa nini sijafanya vile,labda sikuwauliza kwa nini nimefanya
hivi,pengine kwa kukalili ndiyo ikaeleweka,hapa wakiwa wameshika machache ya
mdomoni bila akilini kuyafikiria,sijui wala isiwe swali kwa kusema
yangetokaje,maana bila kutazama itakupasa ujijibu mwenyewe.nasubiri vingi na
haki yangu ntendewe,maana ya kuwa nayo ni vile inavyotendeka,hatuwezi kuwa na
akili tukaziweka tukasema pale kakosea,wapi kapatia na mbona hukusema?hapa
tutaingilia mlango wa chooni,maana hata huko mbele kulivyo kaa kaa ni kama vile
imewekwa,si ni njia fupi…basi yapasa kuweka miba.pengine njia itaeleweka.
No comments:
Post a Comment