Tuesday, October 11, 2016

KUZA KIPAWA CHAKO NA KATAA KUSHINDWA.

Vitu vinavyokuja kirahisi mbele yetu kama zawadi inaweza kukupelekea katika sehemu nyingi chagua na kuwa na uzuri  katika kila jambo, amua kutoka ndani ya mfuko wa moyo wako na kuangalia nini unataka kufanya katika maisha yako ukitakiwa kuyandeleza maono na mawazo yako.

Usijifiche bali fanya ni lazima kufanyia kazi kipawa chako ikiwa ni nguvu na tabia ya mtu, amua kwamba utajisukuma ili kufika mahali Fulani kwa nguvu zako mwenyewe,

Nguvu ya mwanadamu ni kubwa sana Zaidi ya ufikirivyo kile ulichoamua hakuna mtu awezaye kukukataza, anza kuongeza na kuimalisha malengo yako kwani mafanikio unayachungulia unayachagua wewe mwenyewe na kipaji chako kikufikishe pale.

Kila siku yakupasa kutafuta nini njia ambayo utafika siku na watu wakuulize na washangae umefikaje pale, maisha yanaweza kuwa ni silaha kwa muda mwingine na vitu vingine watu hawafundishwi hivyo sio kila kile ufanyacho ni mafanikio  yakupasa kuwa na nguvu zaidi ya maisha yako yenyewe na namna unavyoyapima mafanikio binafsi, kubali kwamba kuna watu wanaitafuta iyo nafasi uliyonayo, 

Hakikisha unatumia siku yako vyema haijalishi ukiwa na furaha ama chukizo yakupasa kutambua kuwa ni wewe upo katika hiyo hali na nini kifanyike,ukiwa unajua unachokifanya haikupasi kuwa na maisha ya katikati inakupasa kuvuka vizuizi, usijaribu kuacha kupigana na kukata tamaa, jiamini na Pigania Maisha sio leo wala kesho Kwani umekuja kuishi.

Tambua uko katika misheni ambayo inahitaji ukamilisho wako, usijikatae kwa kukosea maana wengi waliofanikiwa wamekosea sana, utajifunza kutokana na makosa bila kujali ni makosa ya aina gani maana mwenye makosa ndiye anayetegemewa kufanikiwa, sema ndiyo kwa kila jambo linalohitaji kuendelea mbele, jaribu unapopata wewe ni lazima utambue kuwa kuna nafasi nyingine katika maisha,

Kwa kile utakacho toa ndiyo hicho utaingiza, usirudi nyuma kamwe muda wa kushindwa ulishapita,kipindi kigumu huwa kinapoteza vipaji vya watu wengi na kujikuta wakibaki wakilalama na kufanya hakuna, funguo ya kufanikiwa ni kujiamini  kujifunza na kutenda kupitia makosa hayo hayo, 

Toa sadaka yako leo  kwa ajili ya kesho nzuri inayokuja na utumie ubongo wako vizuri ili kukuendesha kuwa na furaha na mafanikio unayoyategemea.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...