Sunday, May 20, 2012

YA MDOMONI.

maana leo imekuja wakati hakuna wa kusema ndiyo Yule atakaye kataa na mwenyewe utamfikishia hapana yake tunashindwa kula kwa yale magumu yakuyasema tunalala juani tunaamkia juani,

tukitaka yapi maana yale ya mdomoni ukiyachelewesha sana baadaye ni ugomvi,watakuja wenye njaa na baadaye tuwaite wakoloifi,wanyang’anyi,wakija na kula karibuni kwa mgeni ni njema sana kwa karibu ya shukrani pia,maana kheri inatoka nje kuja ndani,

kama ungalikuwa ugali wa konde ni mchafu basi ingekuwa vyema kama nasi tungepita kwa ujazo wa mafuta vipimo vingine ni vidogo sana,haki mafuta kutokuweka kabisa.maana miili yetu,viungo vyetu vimeamua kujishughulisha kwa usaidizi wa damu nasi tunaseme asante Mungu,

Leo yalikuwa hauyaoni haya kesho utasema hauyaoni haya,yapi yale ya muda mrefu yakakumbukwa maana kwa muda unavyokwenda,kwa matendo yanavyokwenda,na hata nguvu zikaribu kuisha uwezo ndiyo wasemeka kujulisha vyote vikiwa vigumu na virahisi

pale ulipolizungumzia jambo fulani tumai ilieleweka,maana kwa muda huu uliwaweka wengine wakae pembeni ikiwa kwa wafogo na wakubwa 

pale palipokuwa na mafungu basi kuna elekezi tofauti yapasa kufahamika isiwe tofauti na kinyume na taratibu kujichagulia,ikiwa taratibu ni sisi wenyewe tunajipa ikiwa ni namna ya kuishi pengine kutaka kuishi kama nani pengine ikawe nani ndiyo imani maana yapasa kuishika sana,

ukajue wewe kama unakufa kwa nini,ukajue kama utaharibika au Mungu tusamehe pengine tumetupa chakula cha mdomoni tukidhani ni uchafu kumbe ni ya kutoka kwetu mwilini haki,

By:Benson G.Makaya

PAMOJA


Mara ya kuwaza ndiyo inayoweza kuzungumzika vingine kwani haikuweza kuwa pamoja,
tumefanya sana,tumepigana sana,tumeona sana,yote yakiwa yanaeleweka,yanapokuja mengi yanakuwa na uchangamfu,kwa pale moja litakalo leta umoja kuwapo na utofauti,kwa mmoja aliye na umoja ni rahisi kuelewa utofauti ya kuwa ametoka huko,tusizungumze vitu tukiwa na maana ya wote,bora ikawe ni kwa umoja unaoleta umoja ili kuikimbilia kheri,

kheri ya wote ipo mbali palipo na yale ya kuchanganya yanayovunja umoja,ikiwa kwa upande mmoja kueleweka hivi na baada ya muda kueleweka vile,baadaye ukaseme ulikuwa hauelewi ni kwa sababu ya muda,imekuja kubwa ukataka ndogo na ndogo umeishindwa,maana unapofikiri kukataa basi umeweza kukubari katika lilelinalokubarika,

yakaja machache yakawa mengi,yakaja mengi na kuonekana machache,yote yakitumia muda ambao unaeleweka tofauti,wenyewe huja kwa namna ile ya kusemeka,
upita kwa namna ile ya kuhadithika,kwani yaweza kupita mbali na kuwa historia,
yaani ni kipindi kirefu sana

Umoja wangu ni katika kuyaunganisha mawazo yangu,ni katika kuunganisha mawazo yangu yanayoitembeza akili yangu,haki kwa aadui kuwaza kuua ikiwa upendo kwa adui mfu,maana hata lile la kuua si lamaana kwake,labda tuone kwa umoja,pengine labda tunakataa kuona kwa umoja,pengine ndiyo maana ya ufilisi wa mali zetu,ikiwa po na utofauti chuki huwa karibu

umoja hujaa mahala pamoja na kushindwa kubebeka,hiyo ikiwa nguvu zimezidi pamoja,kwa upande fulani hatutazungumza ya kufundishwa ili wengine wasielewe,basi tuongee ya asili ili na sisi wenyewe tuendelee,tena hapo tutaelewa wote,pale ukimkuta mwalimu hajaelewa basi ahairishe somo,ubongo ni wa pamoja kwa kujua leo si kujifanya kulijulikana,

maana kila leo linatoka lake,hili litasema lina umoja wake,lile litazungumzia umoja,
lile litaleta umoja,malengo yatakuwapo,hapo hapo panapokuwa na maungano,sio mwingiliano kwani uweza wa umoja ni mapigano,na sio kama meza ilivyogeuzwa kwa kula chakula cha jana tukidhani cha leo hakijapikwa,wandugu wanaficha cha leo maana na kesho kitafika,kwa kufikiri ya leo pia,kumbe hata bila jana leo siyo siku nzuri,asante kwa chakula leo imeonekana,ni umoja usiojali siku,ni umoja unaojenga siku

Tusirudie tena tukashindwana kuelewana,hapa na maandishi kidogo kwani utakumbuka yale ya ndugu mtayaona,watu hawa,sisi yaani na wao pia,usifanye kwa vile zimewekwa alama,
ujue hata ni wapi pa kuweka alama,ukafikiri kwa madini,ukayaona ya leo maana hazina yetu ni ile ya jana,

basi hata ikawa zamani,tunasubiria kupata nguvu ili watupe mashamba,
tunasubiria kumaliza ili watupe makazi,tunasubiria kueleweka angalau tukaletana pamoja,
hapa sio ya mbu wala kipindupindu inzi,ni ukali usioleta madhara na hasara kwa mpigaji,hakuna kupigana kwani kuelezana utaratibu kwa pamoja.

By.Benson G.Makaya

MAMA



Bila wewe nisingekuwepo.
nguvu na imani imepitia kwako,umekuwa mshindi kwa  njia zako za ukuzaji,umeweza hakika nakupa saluti,maana jeshi uliloliunda si kama vile likafikirika,nguvu zimeongezeka kuona uwepo wako mama,sio tu leo ndiyo maana naendelea kupigana,mimi na nafsi yangu pamoja,nikiwa naimani kwa zuri la kujengwa hung’aa limalizwapo,maana ndiyo sijui utakuwa mwisho ama ni mwanzo wa kutembea,hapa sasa ntakuwanimesafiri muda mrefu sana,

machoni pangu umekuwa mbali hata sitaki kukusahau,
ni hapa bado nina hitaji la kukuona mama,unajua kwa nini hata sikuite mama,maana sidhani hata ingekuwa vile isingekuwa hivi,umenijaribisha kwa mengi sana,hiyo ikiwa ni njia ya kutaka nifanikiwe,sisemi mengi yakuwa nakuona haya inaweza kuja na baadae tusiitane wanafiki,maana watoto wengine wana tabia mbaya sana,hawawaheshimu hata wakubwa  zao.

Punguzo linazidi kukujaa,
ongezo linazidi nifika maana,hapa ndiyo ulijua tu,
hapa ndiyo ulijua kama nasikia joto ama vile nitakiwapo kuvaa sweta,hata kama sio baridi,umenikinga sana na mvua kwa kiti kunipisha,heshima ya upendo sio moja kwa chozi la kushoto kudondoka,mengi yanatokea karibu kushikiria mkia,hapo ukitaka nisidondoke,leo ije isikatazwe nawe kwa kujua ni mpya,maana nap engine ulielewa yako sana mama,kwani hata hali ya hewa ya mwili wangu kuifahamu,kujua marelia inaanza hii ikiaminika vilitoka katika nafsi,ndani lifikiriwapo jambo kama vile ilivyo kwa yako nafsi.

Tungetafuta wangepata ,tungetafuta ingewezekana,
tungetafuta nisingepata,maana kwa uwepo wa peke yako nasema asante mungu,maana amenijuza wewe sasa,mwelekeo na mwenendo akinionyesha kwa kisomo ni jitihada zangu,ingawe jitihada ziwe za nini,maana nasoma mwisho nisielewe kwa nini kutokujua kushona nguo uvaayo,maana zamani  hawakuvaa nguo hivyo,vile ilikuwa adamu na hawa.

Mengi yamepita ni magumu kuyapata kwa kusema,
ikiwa ni maumivu basi karibu tunafika vumilia mama,ni hapo tu karibu ya kuwa na uvumilivu,fahamu zangu zinaendana na mengine ya  umri wako,nifanye vile utakavyo,nami ntakusikiliza bado nakusikiliza mama,bado nahitaji kukusikia mama,bado nina hitaji la kukufikia mama,huko ni mbali kumbukumbu zinanijia,ntakuja karibuni ya moyoni yatakufikia,salamu kwako mama mpendwa,
Mwenyezi Mungu atajalia daima

By.Benson G.Makaya

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...