Mara ya kuwaza ndiyo inayoweza kuzungumzika vingine kwani
haikuweza kuwa pamoja,
tumefanya sana,tumepigana sana,tumeona sana,yote yakiwa
yanaeleweka,yanapokuja mengi yanakuwa na uchangamfu,kwa pale moja litakalo leta
umoja kuwapo na utofauti,kwa mmoja aliye na umoja ni rahisi kuelewa utofauti ya
kuwa ametoka huko,tusizungumze vitu tukiwa na maana ya wote,bora ikawe ni kwa
umoja unaoleta umoja ili kuikimbilia kheri,
kheri ya wote ipo mbali palipo na
yale ya kuchanganya yanayovunja umoja,ikiwa kwa upande mmoja kueleweka hivi na
baada ya muda kueleweka vile,baadaye ukaseme ulikuwa hauelewi ni kwa sababu
ya muda,imekuja kubwa ukataka ndogo na ndogo umeishindwa,maana unapofikiri
kukataa basi umeweza kukubari katika lilelinalokubarika,
yakaja machache yakawa
mengi,yakaja mengi na kuonekana machache,yote yakitumia muda ambao unaeleweka
tofauti,wenyewe huja kwa namna ile ya kusemeka,
upita kwa namna ile ya
kuhadithika,kwani yaweza kupita mbali na kuwa historia,
yaani ni kipindi kirefu
sana
Umoja wangu ni katika kuyaunganisha mawazo yangu,ni katika
kuunganisha mawazo yangu yanayoitembeza akili yangu,haki kwa aadui kuwaza kuua
ikiwa upendo kwa adui mfu,maana hata lile la kuua si lamaana kwake,labda tuone
kwa umoja,pengine labda tunakataa kuona kwa umoja,pengine ndiyo maana ya
ufilisi wa mali zetu,ikiwa po na utofauti chuki huwa karibu
umoja hujaa mahala
pamoja na kushindwa kubebeka,hiyo ikiwa nguvu zimezidi pamoja,kwa upande
fulani hatutazungumza ya
kufundishwa ili wengine wasielewe,basi tuongee ya asili ili na sisi wenyewe
tuendelee,tena hapo tutaelewa wote,pale ukimkuta mwalimu hajaelewa basi
ahairishe somo,ubongo ni wa pamoja kwa kujua leo si kujifanya
kulijulikana,
maana kila leo linatoka lake,hili litasema lina umoja wake,lile
litazungumzia umoja,
lile litaleta umoja,malengo yatakuwapo,hapo hapo panapokuwa
na maungano,sio mwingiliano kwani uweza wa umoja ni mapigano,na sio kama meza ilivyogeuzwa kwa kula chakula cha jana
tukidhani cha leo hakijapikwa,wandugu wanaficha cha leo maana na kesho
kitafika,kwa kufikiri ya leo pia,kumbe hata bila jana leo siyo siku
nzuri,asante kwa chakula leo imeonekana,ni umoja usiojali siku,ni umoja
unaojenga siku
Tusirudie tena tukashindwana kuelewana,hapa na maandishi
kidogo kwani utakumbuka yale ya ndugu mtayaona,watu hawa,sisi yaani na wao
pia,usifanye kwa vile zimewekwa alama,
ujue hata ni wapi pa kuweka
alama,ukafikiri kwa madini,ukayaona ya leo maana hazina yetu ni ile ya
jana,
basi hata ikawa zamani,tunasubiria kupata nguvu ili watupe
mashamba,
tunasubiria kumaliza ili watupe makazi,tunasubiria kueleweka angalau
tukaletana pamoja,
hapa sio ya mbu wala kipindupindu inzi,ni ukali usioleta
madhara na hasara kwa mpigaji,hakuna kupigana kwani kuelezana utaratibu kwa pamoja.
By.Benson G.Makaya
No comments:
Post a Comment