Bila wewe
nisingekuwepo.
nguvu na
imani imepitia kwako,umekuwa mshindi kwa
njia zako za ukuzaji,umeweza hakika nakupa saluti,maana jeshi
uliloliunda si kama vile likafikirika,nguvu zimeongezeka kuona uwepo wako
mama,sio tu leo ndiyo maana naendelea kupigana,mimi na nafsi yangu
pamoja,nikiwa naimani kwa zuri la kujengwa hung’aa limalizwapo,maana ndiyo
sijui utakuwa mwisho ama ni mwanzo wa kutembea,hapa sasa ntakuwanimesafiri muda mrefu
sana,
machoni
pangu umekuwa mbali hata sitaki kukusahau,
ni hapa bado
nina hitaji la kukuona mama,unajua kwa nini hata sikuite mama,maana sidhani
hata ingekuwa vile isingekuwa hivi,umenijaribisha kwa mengi sana,hiyo ikiwa ni
njia ya kutaka nifanikiwe,sisemi mengi yakuwa nakuona haya inaweza kuja na
baadae tusiitane wanafiki,maana watoto wengine wana tabia mbaya
sana,hawawaheshimu hata wakubwa zao.
Punguzo
linazidi kukujaa,
ongezo
linazidi nifika maana,hapa ndiyo ulijua tu,
hapa ndiyo
ulijua kama nasikia joto ama vile nitakiwapo kuvaa sweta,hata kama sio
baridi,umenikinga sana na mvua kwa kiti kunipisha,heshima ya upendo sio moja
kwa chozi la kushoto kudondoka,mengi yanatokea karibu kushikiria mkia,hapo ukitaka nisidondoke,leo ije isikatazwe nawe kwa kujua ni mpya,maana nap engine
ulielewa yako sana mama,kwani hata hali ya hewa ya mwili wangu kuifahamu,kujua
marelia inaanza hii ikiaminika vilitoka katika nafsi,ndani lifikiriwapo jambo
kama vile ilivyo kwa yako nafsi.
Tungetafuta
wangepata ,tungetafuta ingewezekana,
tungetafuta
nisingepata,maana kwa uwepo wa peke yako nasema asante mungu,maana amenijuza
wewe sasa,mwelekeo na mwenendo akinionyesha kwa kisomo ni jitihada zangu,ingawe
jitihada ziwe za nini,maana nasoma mwisho nisielewe kwa nini kutokujua
kushona nguo uvaayo,maana zamani hawakuvaa nguo hivyo,vile ilikuwa adamu na hawa.
Mengi
yamepita ni magumu kuyapata kwa kusema,
ikiwa ni
maumivu basi karibu tunafika vumilia mama,ni hapo tu karibu ya kuwa na
uvumilivu,fahamu zangu zinaendana na mengine ya umri wako,nifanye vile utakavyo,nami ntakusikiliza bado nakusikiliza mama,bado nahitaji kukusikia mama,bado nina
hitaji la kukufikia mama,huko ni mbali kumbukumbu zinanijia,ntakuja karibuni ya
moyoni yatakufikia,salamu kwako mama mpendwa,
Mwenyezi
Mungu atajalia daima
By.Benson G.Makaya
No comments:
Post a Comment