Mara kwingi ninapotoka ninakutana na watu wazuri,wakiwa wao
ndiyo wao hasa ndiyo ikawe hata maana ya kukutana,pengine tukimaliza mkutano
upate japo neno jema kwamba karibu kwenye mkutano,sijui ikiwa imetendeka nini
ndani humo,maana kabla tulisema bila kujuana,pale ikaenda kimeisha kikao
tupeane karibu,hizi zikiwa na maana ya sijapenda ulichokifanya na vile karibu
sana,maana utasisitizwa hata siku nyingine,hapa sio kujua kwa kuwapo,ni kujua
kwa kuelewa,tumejuana kwa kukutana.
Pengine sio bahati mbaya ila ni nzuri iliyokuwa na
ubaya,kama vile jamaa alisema kuhusu mwongo ya kwamba ”
Kuna mtu anauongea uongo si kwasababu amedhamiria ila ni kwasababu anajua huo
ndio ukweli huyu hawezi kuwa mwongo, bali huyu haujui ukweli”.kwa kweli
sio kosa la kukutana,bali ni vyema tumekutana ili kuelezana,pengine kila mtu
awe na lake ili kuweza maana,pengine ili
kucheka zaidi ama kununa,maana ya kununa siijui zaidi yake,pengine ni kufa tu..
Sasa si italeta ugomvi,tena itakuwa
ni bahati mbaya,maana kuna watu wanajua kununa kweli kweli,hapo bila ya kujua
wanapoteza namna ya kucheka,kutabasamu..maana maisha ya mwanadamu aliyefanikiwa
kiroho na namna awezavyo ni kucheka,hata kutabasamu maana ni mwanzo wa kucheka.
Hakuna maana ya kusema wewe ni nani
wakati wewe ni nani,maana inahitaji uje kwa adabu tena ukitaka kusema wewe sio
nani,maana hakuna aliyekutilia maanani,’hapo mwanzo alikuwepo sungura na fisi’,hadithi
hizi hatuzitaki siku hizi.asante sana kwa kukutana maana imefika kipindi
nimekueleza hata yale ya jana,ngoja kesho ije tutafayaje kama sio kusikiliza ya
jana?kama umeyaacha mawili kayachukue,ikiwa haiwezekani ingia hivyo hivyo
mkutanoni.