La kwanza mimi silitaki kuliona,Linavyokuja utasema
limetumwa,maana kasi sio kasi,mwendo kasi sio mwendo kasi,wala hata mwendo
kenda sijui tukaita nini,dunia inaendelea kukuwa na mambo yake,hakuna chaguzi
lililokuwa sahihi,kama vile mwalimu alikosa na na baadaye akawapa mtihani
mnadhani kuna kupata swali hapo?maana kama vipi maksi zitaganywe,tena kila mtu
akabaki na chaguo lake,maisha ya kuishi kipumbavu siyapendi!!!sasa sijui
tunaishi vipi,maana mwalimu akiwa chizi kuliko mwanafunzi hapo lazima mzazi
aingilie kati,maana laaana za siku hizi ni za wazee wale waliodhurumiwa mali
zao,sijui hawakupata vyao?ama ndiyo walivyovitunza na baadaye kugawa kama vyao…hili
zoezi ni kubwa kwanza mimi sitaki kuliona
La pili niache nitafanya baadaye,maana nimechoka na
mizunguko ya matembezini,pengine tukisema mjini na wakati ni temboni tutakuwa
tunajizungumza bila kujijua,pengine tunasema kama mwanafunzi anapotaka kuwa
kama mwalimu,maana mwanafunzi anachofundishwa ndicho hicho hicho cha ualimu,napenda
saana kuwa mwalimu,najua napofundisha wanafunzi wangu watatamani kuwa kama
mimi,maana kama mtu hajalionyesha lake..mpe lako pengine,majaribu ni
kuweza,ukiwaza yangu yako utayaweza.hili liache ntaliongelea baadaye kidogo
La tatu ahh me siliwezi,lakini ngoja nijaribu..ndiyo baadaye
imekuja,tumeskia tukisema jaribio ni kuweza,maana alijaribuje?kama alifanya
basi aliweza,na ndiyo maana hata kulikuwa kunakungoja,ngoja ni kusikiliza,baada
ya kuendelea kusikiliza matumaini yatakuwa sikilizia,matumaini yamekuwa baada
ya kutaka kujaribu,tena matumaini ni yale ya kushinda,maana lilikuwa
haliwezekani ‘lakini ‘imeleta matumaini ya kutaka kujaribu,na mtu anapojaribu
iwe katika kuweza ama kushindwa kwa kuelewa huanza moja,hiyo yote ikiwa ya
kutokujaribu tena,swala lingine linalokuja
La nne kutokujua kama kuweza,hili linapoteza matumaini,najua
wengi wao watachukua vyao pale mchele wanapoanika nje,hata ndege,kuku,njiwa na
vitu kama hivyo,hapa nikitizama nyuma naona kama hatukujua kama kunawezakana
pengine tukajaribu kwa nguvu zote,maana wote hao ni ndege tu,sasa sijui ndege
ndo nanii….?nikisikia hili neno nakumbuka ‘aeroupleni’kipindi kile darasa la
ngapi sijui,tuna hamu ya kusafiri,lakini tuna hofu ya maisha yetu,ikiwa
kimazingira yatayotofauti ikiwa bado kuna kutokujua kuweza
‘Hofu haionekani kwa macho’kila mtu anayo