Monday, June 4, 2012

MKAO..

Tuchague pale tunapofanya,tunakuwa kwa vile hali zinatufanya kwa kuchanganya na mengine ni kama kutoa,labda pale tunapofikiria tofauti,zikiwa hazina idadi kwani ndiyo hatutaelewana,pengine tuendelee kutoelewana,yanaskika mengi yanaogeleka mengi na ndiyo tuendelee kuyatenda hayo,tukiwa hatukutaka kutenda mojamaisha ikiwa ni kutafuta tu,tuseme njia ndiyo zinauwalakini muda mwingine tujachague kudanganya,maana tumedanganya mengi sana kama ni kusema uwongotena ni walongo kabisa,muda mwingine tupeleke mbele mambo yetu kwa maana tulikuwa vile kwa kipindi kile,sasa wakati unajificha tena na mambo yenyewe yakidanganya kama itakuwepo tena pale.

Tunapopotea tunajua maana ya kuwepo,ali ikafika tukataka kurudi pale palipo salama maana ndiyo nyumbani,haya yasipoteze maana kwa kutokueleweka ama ikiwa ni kudanganyika tena ikieleweka hivyo iwe ni mtu amechagua mwenyewe,ikiwa kama nafasi inayoshikirwa na mtu wa kwanzahuogopa kuwa ya mwisho,pale tukaseme basi kristu turudie na uje upate mateso tena tutaambiwa tunamchezea mungu ya kuwa alikuja mwanzoni,pengine hata wa mwisho akaogope kuwa wa kwanza,ikiwa kuna bahati ndiyo maana na furaha zikaja,kuwa wa kwanza sio nafasi ya mchezo mchezo hata kwa wale waliopungukiwa akili wa wao ieleweke kwamba mtu huyo yupo halisi katika kuufata uzima.

Usahihi huj ani baada ya kutokea,pengine yaliyotokea si magumu sana bali yalipewa muda,na hapa tukae chini tuone kama muda tuliojipatia ni dhahiri yastahiri kufanya masahihisho,pengine tukawa tumewahi sana na baadaye tukaja kufeli katika namna ile ya mwanzo,ambayo hiyo ilikuwa kama tunafanya na sio kujifunza,pengine tunapofanya mambo yetu tunajitahidi sana,na ikawe kwa mwanadamu kuonekana ni mpaka kuweza,hapa tukijua hakuna kuweza kwa sababu hata ilivyoonekana ni vibaya kwa kusema haikugundulika vile.

Tukae tuote tena,tukae tufikiri tena,tukae tuwaze na kujua yapi ni mema maana kwa kuyatenda mabaya,ama yale mema basi yakawe katika usahihi saidi,yakaunganike kupitia mawazo ya zamani na maumbile ya sasa,kwani kinachotakiwa kufanyika sio tu kulima bali hata kutengeneza majembe kwa ajiri ya walimaji ili kuondoa utegemezi,tukiwa tunategemea sana hapo tunakuwa hatueleweki yakuwa tumeshikiliwa misimamo,hapo tunahitaji jambo ushirikiano.

NGOJA MPENZI..

Nashukuru kwa uwepo wako,usinikimbie ukaniacha mwenzako,nimechoka na mengi huko nitokako,nsubiri karibu mpenzi naja kwako,umalikia na mengine yote sifa zako,nimekaa nakuwaza na hata kwenye mizunguko,Baraka zikujae maisha yaje kwako,busara,utii na tija katika malengo yako,pengine ni fikra zangu pale nikugombezapo,wewe sio mwanangu nikuchunge uendako,umejua mengi mengine katika nafsi yako,napokuwa karibu kufanya ushindi nanyoosha mkono wako,rangi na sura havijalishi tuendako,tukae tufikiri maisha si kunibagua mwenzako.

Nakuwa mshindi pale nikuonapo,nakuwa sishindi pale usipokuwepo,hata nikajaribu kufumba haya yangu macho,imani na mawazo yote yapo kwako,najiskia furaha ninaposikia kauli kutoka kwako,nakupenda ua langu pamoja na familia yako,chochote sitaki ahidi nisitekeleze lawama kwako,ninachokiweza subiri mpenzi muda hujapo,hapa tulipo nahisi kama pepo,hapa tulipo najiskia vizuri ukiwepo,mara nyingine kimwili nisipokuwapo unanishika mkono japo kwa imani kuona kilichomo.

Najaribu tena kurefuka mpenzi nikufikie,najaribu tena mpenzi kujirekebisha ili usichukie,nione peke yangu kwa machozi usintilie,nione peke yangu pendo langu ulifikirie,karibu siku tutaona yaliyonona,karibu siku tutakuwa waliooana.Napigana kesho ya leo yasinisumbue,napigana leo na kesho nikuandalie,karibu sana,karibu sana kwa sebule..hizi zitakuwa bora hasa kwa viumbe watakao kuwa bora,bora tuijaze dunia pamoja,bora tukasherehekea pamoja,ikiwa nafsi yangu ilishakuwa moja,sina la tofauti la msingi kujikongoja,

Mawasiliano kwetu isiwe taabu,mawasiliano kwetu kama kipindi  cha mababu,hali zinabadilika ya leo uizoee,hali zinagawanyika haya ni ya kesho tukayafurahie,pengine tukapate pale ilipotakiwa,pengine pakawa kwetu palipotakiwa,kesho ntakuja kituoni mpenzi ngojea,kesho inakuja penzi letu bora linajongea,isipite siku bila kuongeza,isipite siku bila kuongea,niko pamoja nawe bila kujali dhambi yako,niko pamoja nawe tuyaone mema zaidi yatokeapo,hii ya kwetu isiwe ya kuumiza matumbo,hii ya kwetu iwe ya kuyajaza matumbo hakika tungoje,hakika tusubiri bado muda kidogo,kwani kumbuka furaha ya mtu inatokana na mtu mwenyewe. 

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...