Monday, June 4, 2012

NGOJA MPENZI..

Nashukuru kwa uwepo wako,usinikimbie ukaniacha mwenzako,nimechoka na mengi huko nitokako,nsubiri karibu mpenzi naja kwako,umalikia na mengine yote sifa zako,nimekaa nakuwaza na hata kwenye mizunguko,Baraka zikujae maisha yaje kwako,busara,utii na tija katika malengo yako,pengine ni fikra zangu pale nikugombezapo,wewe sio mwanangu nikuchunge uendako,umejua mengi mengine katika nafsi yako,napokuwa karibu kufanya ushindi nanyoosha mkono wako,rangi na sura havijalishi tuendako,tukae tufikiri maisha si kunibagua mwenzako.

Nakuwa mshindi pale nikuonapo,nakuwa sishindi pale usipokuwepo,hata nikajaribu kufumba haya yangu macho,imani na mawazo yote yapo kwako,najiskia furaha ninaposikia kauli kutoka kwako,nakupenda ua langu pamoja na familia yako,chochote sitaki ahidi nisitekeleze lawama kwako,ninachokiweza subiri mpenzi muda hujapo,hapa tulipo nahisi kama pepo,hapa tulipo najiskia vizuri ukiwepo,mara nyingine kimwili nisipokuwapo unanishika mkono japo kwa imani kuona kilichomo.

Najaribu tena kurefuka mpenzi nikufikie,najaribu tena mpenzi kujirekebisha ili usichukie,nione peke yangu kwa machozi usintilie,nione peke yangu pendo langu ulifikirie,karibu siku tutaona yaliyonona,karibu siku tutakuwa waliooana.Napigana kesho ya leo yasinisumbue,napigana leo na kesho nikuandalie,karibu sana,karibu sana kwa sebule..hizi zitakuwa bora hasa kwa viumbe watakao kuwa bora,bora tuijaze dunia pamoja,bora tukasherehekea pamoja,ikiwa nafsi yangu ilishakuwa moja,sina la tofauti la msingi kujikongoja,

Mawasiliano kwetu isiwe taabu,mawasiliano kwetu kama kipindi  cha mababu,hali zinabadilika ya leo uizoee,hali zinagawanyika haya ni ya kesho tukayafurahie,pengine tukapate pale ilipotakiwa,pengine pakawa kwetu palipotakiwa,kesho ntakuja kituoni mpenzi ngojea,kesho inakuja penzi letu bora linajongea,isipite siku bila kuongeza,isipite siku bila kuongea,niko pamoja nawe bila kujali dhambi yako,niko pamoja nawe tuyaone mema zaidi yatokeapo,hii ya kwetu isiwe ya kuumiza matumbo,hii ya kwetu iwe ya kuyajaza matumbo hakika tungoje,hakika tusubiri bado muda kidogo,kwani kumbuka furaha ya mtu inatokana na mtu mwenyewe. 

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...