ni salamu bora kwa ajili
yako,pengine uangalie chini na kukaa kitako,ni gharama kubwa sana
kwa zawadi yako,hakika unamtukuza
mungu wako pengine ni zile aina na namna zako subiri leo uone kesho yako si kutishana bali ni habari zako,mungu wasaidie wengine hata watembeako,muda mwingi pale jua
lizamapo,Kuitana wifi na rafiki zako madada zangu ndiyo wale rafiki
zako ntaongea mengi temeke sijafika labda gongo la
mboto,ningeona tofauti kwa yale mambo yako,mapenzi bora hujulikana
yatokeapo,mapenzi bora ni kwa mtoto wako,nafsi zikaungane na kuwa zako maana ya
muunganiko wangu kutoka kwako,maisha ni mafupi tule kiapo,maisha ni matamu japo
tuyaonjapo.ufikiri mbele na sio utokako,tufikiri mazuri mpaka tufanikiwapo
Imani yangu ni katika ndoto zako imani yangu ni katika
ukifanyacho,maana umekuwa kidonda ,hata ukauma kwa utamu,Mawazo yako
yameniinua,nimekuwa mpana wa kufikiri kwa kuona wale wanaotaka kukununua,pengine isiwe
siri kuona ama tukaona kwa vile tukasikia,hapa utasikia machache sana kwa
kubania yaliyomuhimu maana imekuja
wakati chako kikawa kizuri zaidi,yaani umepitiliza katika unyoofu niliouzoea
katika mambo niliyoyategemea,umekuwa kibiriti kwangu my dear,umeniwasha na
mwisho nikamalizika umenipuliza kabisa,umeniwasha asante kwa kuitikia,umenilaza
na asante kwa kuitikia.
Maisha yamekuwa bora kwangu nahitaji kukutumikia,umekuwa
kinara wangu kwa mataa kunimulikia umeniwasha kupindukia,nalijaribu kuangalia
pembeni sikusikia,kabla sijasikia ya nani ntayafikiria?umemaliza mawazo kwa machache
kuchangia ,unyooshe kijiko ya kuwa sukari yenyewe ni ndogo ya kurumangia ,mtamu
usipungue kamwe nawe enedelea kunibembeleza,sipati raha lakini moyoni
najisikia,nafsi yangu umeiweka angani mwezi na jua havijulikani
No comments:
Post a Comment