Monday, October 29, 2012

USHAURI.


Hapa hakuna nasaha maana si la muhimu kwa yeyote,kwa aliye na umuhimu wa kutaka kuelewa hukaa chini na kusikiliza ushauri,ushauri  si wa bure,ushauri ikiwa ni njia za kutaka ya kule,pengine ukaja japo mchango maana wengi wao wameshauri sana,maisha ya mwanadamu hayapaswi kutembea na ushauri,maana haifai ikafika siku na ushauri akafa bila ya mafanikio,maana kama mwanadamu unashauriwa unastahiri kushaurika.

Mshauri si ushauri,pengine ikafikirika tofauti ya kitu na mtu,kheri ya vyote kuwa wote,maana unaweza penda ushauri bila ya mshauri,kubali yale unayoyafikiria ni kweli,ikiwa umekataa hata kwa kushauriwa basi ni kheri,huu wangu ushauri naupeleka kwako ili ukashauri,pengine mkiwa wawili wewe Pamoja na akili yako,zako ni uwingi usioleta namna ya ushindi maana umetajika kwa wingi,hapa tukasema heli mchina mmoja kuliko mabata kumi,maana kazi ya bata ni kula,kujisaidia na kuogelea.ushauri  mwingine huja baada ya kujua machache ya mwanzo pia

Haifai kukataa ushauri ikiwa umekuja bure,leo kila kitu kimekuwa bidhaa na matapeli watakao kuja hawata taka hata senti,maana wao walishazurumiwa haki zao kwa kutokupenda ushauri,ushauri wa mshauri ni kushindwa ushauri,maana mwanzo ikasemwa pokea ushauri wa bure ili kufikiri zaidi yale yako,maana pengine haikupaswa kushaurika zaidi ya kupokea lawama za kutokushaurika.

SIMAMA...


Haitakuwa njema kwa kuokota bila ya kumfikiria Yule aliyedondosha,haitakuwa na maana ya kuinama bila ya kuangalia pale utakaposimama,leo ikiwa inazungumziwa sana ni lazima kuifikiria kesho itakujaje,yamekuwa magumu sana kwa kulinganisha namna za kufanya,yaani mambo huja kwa kuwa yana njia zake,ikiwa kitu kimedondoshwa kisije bahati ya kuwa umeokota,mara hapo ikafanana na namna ya vidude vilivyo ama ndiyo bahati zilivyo,fikiri endapo utasimama na kukuta umeokota mke,maana ndiyo bahati yenyewe.

Usipojua leo ule nini kesho huja na kukufanya  ushindwe kula hata maini,nimeona mengi..umeona mengi,,ikiwa unamsemea mwenzako ana nini fikiri ya kuwa umefanya nini,fikiri endapo umefanya nini ni sawa na kesho ikaja na yako yakawa kama maini,maisha ni mapambano..maisha ni kusimama vijana wakisema kidete,kwa imani yenye msimamo ndiyo kuweza kufanya vitu vilivyo simama,hakika haina haja ya kifikiri wakati hauna uwezo wa kusimama,japo  kiakili.

Usiogope ya  mtaani kwa kuwa bado hujasimama,usiombe samahani kwa kusema kana kwamba unataka kusimama,labda kwa waliokuwa wamesimama wakae,ama kwa ilivyo kusimama na kuwaziba walio mbele,hakuna anayeweza kukueleza yale unayoyataka ikiwa yamesimama katika fikra zako,pengine ukielewa tofauti ya jambo yapasa kusimamia lengo na kueleza Mawazo yako.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...