Thursday, August 16, 2012

AHADI


Kama unavyoweza kusema utarudi tena,ikiwa umeahidiana kitu ki maongezi pengine hata vitendo,au vile jana ulisema na leo imetokea basi hakika na kesho inapaswa kutegemewa yakuwa dunia ni duara,pengine Mungu angewaahidi wana wa Israeli kupitia musa wazungushwe hata pengine wangemsaliti kwa asilimia kubwa sana,maana wengine wangejifanya wanajua kurekebisha bila ya kuhofia  yatakayo haribu kwa vile kiongozi alivyo sidhani kama ahadi zinabadilika zaidi ya kutokutendeka,maana hapo utabadilishana ya moyoni,muda unayake kaa ukiwa na subira ya kile ulichoahidiwa kesho

Hakuna na kuogopa zaidi ya kuamua vile vinavyokuja bila ya ahadi maalumu huwa havidumu,pengine ikiwa ahadi inafikirika kwa siku nyingi sana,pengine uyo aliyeahidi akiwa mwongo  ndiyo vile maana ya kutokutendeka,na kama ilikuwa ni mara moja basi haina haja ya kutegemea ya pili,pengine kama Mungu angeahidi kufika katika nchi waliyoahidiwa,na baada ya kikwazo cha bahari wakadhani sio Yule mungu musa aliyemtuma kuwafikisha wanawe mahala,lakini walivuka na kufika pale,tena waliandaliwa,uliye na imani tofauti fikiri hili ni kama neno.ahadi hata kama ni tofauti lakini ziwepo uzikute upande wa kutumia iache subra yako.

Kesho ndiyo siku njema mahala hata nilipo ni zamani,kila dakika ya kufikiri inakwenda bila hata ya kudhani umeahidiwa nini,pengine ahadi yako bado hazijatoka au yapasa kuomba tena na bora kesho ije maana yale yote ya jana yanategemeana,sidhani kufika kumi bila moja iliyopo,pengine mungu amekuahidi kitu kimoja tu pengine kila mtu akamshukuru mwenyezi Mungu vyema akafanya hivyo pengine utende yanayostahiri kwa kila mmoja wetu ili usiweze kugombana kwa zawadi zitakazo kuja kwa ajili yako ikiwa zilikuwa na ahadi.

KUWA HURU..


Kuwa na uhuru kunakufanya uwe na mafanikio,yaani ukiwa na uhuru wa maamuzi na kutenda,pengine kila mtu anatenda yake,hata Yule unayemwita mwehu naye anatenda,pengine hapa ndiyo tukafikiri nakujua kuwa  palipo na mwanadamu panahitaji akili,yaani fikra zilizotimia,ikiwa inajua nini kile inachokifikiria,pengine tumekuwa na uhuru tangu mda mrefu na tumeshindwa kufanya lolote,sisi ni wapumbavu..yaani hatuna akili maana tuliyotenda ni sawa na bure,uhuru wa bure,tena ingalikuwa wanaotupa uhuru hawatukufahamu  tungalikuwa  udongo kabisa.

Sijamwona huyu wa kunitisha maana mengine aliyasema baba,ndiye aliyenipa uhuru wa kuishi hapa duniani,mengine wala hata si haba maana hata watoto wadogo wa sasa wanayo.waswahili tunasema samaki mmoja akioza wote huoza,tukisahau walikula mpaka maiti..au mtoto wa nyoka sio nyokaa..?uhuru mwengine unatia raha sana,maana unaweza ukajiona mfalme lakini ukafika muda uliopangwa ukahisi njaa,pengine wengine wanapitisha hata siku ngapi,pengine wakiwa na ufalme wao ama vile kwa ukwabela wao,huru ikiwa inahitaji kutokea maana kuna utofauti mtatu,ama mbili kubadilishana na moja au moja kubadilishana na kila moja nyenzake,kuwa huru kuelewa..

Ilipofika siku yake ilitokea,maana wale walio na mafanikio katika mambo yao wataelewa,jinsi vile namna waliweza kukumbuka mpaka kufikia hapo,uhuru hauhusiki na utumwa.ukitakiwa kuwa mtumwa basi unatakiwa utambue mafanikio yako,sasa ujue kwa kutumia akili yako,maana mwishoni tutaona matendo yako,baada ya kifo kuna maneno machache tu..kama tungalikuwa huru kufungua mbingu basi ingeeleweka kwa uchache wake.
kuwa huru katika maisha yako maana kile kilichoandaliwa kwa ajili yako kitatimia

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...