Tuesday, October 30, 2012

KAULI NA VITENDO


Unaweza kusema unataka kushika na wakati bado hujashika, ikiondoka dhana ya kwamba haujui, pengine kisifuatwe kile ambacho Yule mmoja akasema,maana ushauri unapatikana kwa kila mmoja, unapofanya yale yanayo kufurahisha maishani mwako usijaribu kuifananisha na kwa mwenzio, maana Kauli zinaweza kuwa sawa huku matendo yakiwa tofauti.

Usifuate mkumbo kama  hujaweza kutoa kauli, kubali unapokosea si ya kuwa hakuna aliyepatia, nikisema mimi nimesema mimi, nikisema sisi basi tumesema Pamoja, mengine huwa yanatia hamasa ya kufanya ikiwa yanaeleweka mambo yaliyozoeleka hufanyika kwani yanaeleweka na isije ukaamini  sana lako ambalo limefanywa na mwengine.

Siwezi kusema kauli zangu ni nzuri kwani hata wengine wanayaona matendo kwa namna ile wawezavyo, matendo yako yanaweza kuwa mabaya na kauli zikafanya kulainisha matendo hayo. simaanishi mmoja akisema nenda na wewe uende, bali ikawe mmoja kasema nenda na ikafikirika utaendaje, tofautisha kauli  yako kwa namna unavyoweza kutenda, ama matendo yako ili kuweza kutamkwa.

BABY GIRL..

A BUTTYFULL BABYGIRL

ONCE SHE CAME INTO MY LIFE....I  felt no regret as what was going it was just the pasts, but it came a time she deliver something to me, That’s love.

Once you see her smile, you can smile too...once she cry, know she cry for you two, you are genius my beautiful baby!! she knows how her parents feel for her, she knows why God created her, she is an angel, she gives comfort when sadness, she love when you give ,you are the future beautiful role model of mine,im proud for a beautiful baby girl.

She always keeps me fight for I have her, she always gives me hopes for how she use to try, when she try and keep trying, for the love I have I give you a million my lady, I’m sorry for not being there when you needed me, I would love to hear all that your beautiful words and posses you have. Shine my girl my time is not enough .

I better keep all your beauties in my heart as you seem to show it all,
 I LOVE YOU MY BABY GIRL.

Monday, October 29, 2012

USHAURI.


Hapa hakuna nasaha maana si la muhimu kwa yeyote,kwa aliye na umuhimu wa kutaka kuelewa hukaa chini na kusikiliza ushauri,ushauri  si wa bure,ushauri ikiwa ni njia za kutaka ya kule,pengine ukaja japo mchango maana wengi wao wameshauri sana,maisha ya mwanadamu hayapaswi kutembea na ushauri,maana haifai ikafika siku na ushauri akafa bila ya mafanikio,maana kama mwanadamu unashauriwa unastahiri kushaurika.

Mshauri si ushauri,pengine ikafikirika tofauti ya kitu na mtu,kheri ya vyote kuwa wote,maana unaweza penda ushauri bila ya mshauri,kubali yale unayoyafikiria ni kweli,ikiwa umekataa hata kwa kushauriwa basi ni kheri,huu wangu ushauri naupeleka kwako ili ukashauri,pengine mkiwa wawili wewe Pamoja na akili yako,zako ni uwingi usioleta namna ya ushindi maana umetajika kwa wingi,hapa tukasema heli mchina mmoja kuliko mabata kumi,maana kazi ya bata ni kula,kujisaidia na kuogelea.ushauri  mwingine huja baada ya kujua machache ya mwanzo pia

Haifai kukataa ushauri ikiwa umekuja bure,leo kila kitu kimekuwa bidhaa na matapeli watakao kuja hawata taka hata senti,maana wao walishazurumiwa haki zao kwa kutokupenda ushauri,ushauri wa mshauri ni kushindwa ushauri,maana mwanzo ikasemwa pokea ushauri wa bure ili kufikiri zaidi yale yako,maana pengine haikupaswa kushaurika zaidi ya kupokea lawama za kutokushaurika.

SIMAMA...


Haitakuwa njema kwa kuokota bila ya kumfikiria Yule aliyedondosha,haitakuwa na maana ya kuinama bila ya kuangalia pale utakaposimama,leo ikiwa inazungumziwa sana ni lazima kuifikiria kesho itakujaje,yamekuwa magumu sana kwa kulinganisha namna za kufanya,yaani mambo huja kwa kuwa yana njia zake,ikiwa kitu kimedondoshwa kisije bahati ya kuwa umeokota,mara hapo ikafanana na namna ya vidude vilivyo ama ndiyo bahati zilivyo,fikiri endapo utasimama na kukuta umeokota mke,maana ndiyo bahati yenyewe.

Usipojua leo ule nini kesho huja na kukufanya  ushindwe kula hata maini,nimeona mengi..umeona mengi,,ikiwa unamsemea mwenzako ana nini fikiri ya kuwa umefanya nini,fikiri endapo umefanya nini ni sawa na kesho ikaja na yako yakawa kama maini,maisha ni mapambano..maisha ni kusimama vijana wakisema kidete,kwa imani yenye msimamo ndiyo kuweza kufanya vitu vilivyo simama,hakika haina haja ya kifikiri wakati hauna uwezo wa kusimama,japo  kiakili.

Usiogope ya  mtaani kwa kuwa bado hujasimama,usiombe samahani kwa kusema kana kwamba unataka kusimama,labda kwa waliokuwa wamesimama wakae,ama kwa ilivyo kusimama na kuwaziba walio mbele,hakuna anayeweza kukueleza yale unayoyataka ikiwa yamesimama katika fikra zako,pengine ukielewa tofauti ya jambo yapasa kusimamia lengo na kueleza Mawazo yako.

Thursday, October 18, 2012

BAADA YA HABARI....



Huwa yanakuwa mazungumzo kwa kuwa aliyeleta habari alidai kumaliza kutoa maelekezo,leo ukiwa unazungumza kwa kutaka kuhadithia habari bila kujua hiyo ndiyo habari yenyewe,pengine ikawa ni taarifa kwa kuwa habari yenyewe ni kama muhtasari,ukijaribu kuonja ni vigumu kuondoa ladha tumboni,labda isingetangulia taarifa basi hakika ingekuja habari kamili ingawaje imeonekana hakuna aliyesikiliza habari kwani baada ya habari kuisha mazungumzo yanaweza yasiendane na habari.


Haki sawa kwa kila mwanajamii,haki si sawa kwa mtoto na mkubwa,labda iwe umesikiliza tofauti na kuona mageuzi katika kichwa cha habari,lakini mazungungumzo yaliyofika baada ya habari yameonekana ni habari yenyewe.mengine hayapaswi kuyazungumzia humu maana wengi wao wamekuja kwa kasi wakitaka japo kuelewa kichwa cha habari lakini wameonekana wataelewa habari yote ikiwa bado umri hauruhusu.


Msomaji wa habari anapaswa kuwa kama daktari,maana kuna mengine yametukia sasa hivi,kuna mgonjwa ameingia wodini baada ya daktari kumaliza muda wake wa kazi,muda mwingine ni wa ziada,muda baada ya kazi..ukifanya kazi muda baada ya kazi bado huitwa ni kazi lakini unakuwa umejitahidi kwa kuzidisha muda,pengine ndiyo huwa ni kazi nzuri zaidi,pengine huwa ni taarifa nzuri zaidi..ikiwa mtangazaji kamaliza habari labda atuletee mazungumzo ili ijulikane baada ya habari nini kifuate ama kilifuata.

NAFASI YANGU ILIPO.


Kama nikianza na kupanga mstari kwa kuwa ni foleni baadaye ntajikuta nipo pale pale tu ikiwa kuna uvumilivu wa kile kilichotakiwa kufanyika maana kwa muda kumepelekea machache kusemeka na kuonekana ni bora , bila mshangao imehitajika kitu cha kunyooshea ili kuunyosha mstari angalau wa pili naye akafuatia humo humo, maana kwa kawaida ya foleni wengine watataka kutanua ikiwa wana uchukuzi wa nafasi ndogo wakizifuata njia ama nia.

Jaribu kuamini kama unapopita mguu wa kushoto na wa kulia unapita humo, pengine yasiwe madharau kwa waliojisahau maana hawakupaswa kupita huko ulipopita zaidi ya kujua umepitaje, ukiwa mwalimu,ukiwa mwanafunzi maana hawa watu wanahitaji kurandana, ingawaje siyo lazima sana kwani nafasi nyingine wanapaswa kupewa wasiojiweza.

Lugha hii ikichanganywa na nyengine unapata wengine tofauti maana utakuja wakati na kusema umejileta ,kwa kuwa kile kilichoonekana sasa hivi yapasa kujua ndani yake kuna nini Kama vile leo inavyokuwa ni mkopo na kesho ni siku ya kulipa deni lakini unaweza kwenda ‘tena’ baada ya kusamehewa deni na zaidi  kukopa tena, madeni yanapokuwa mengi unajileta na kujisogeza kwenye mtego wa kuichanganya nafasi yako kuchanganyana na ya kule usiyoyategemea.

Wednesday, October 17, 2012

UFALME..

 
Hasa pale ukafika wakati maana ni wazi hata ukiwa mfalme inapasa kuunyofoa ufalme wako,ilifika kipindi kuonekana kufungwa njia katika baadhi ya sehemu,ikiashiria hatari ama kirahisi zaidi ikawa si ruksa kupita,lakini ukiwa mfalme unaruhusiwa kwa kuwa wewe ni mkubwa,zama za kizamani sana ambazo zinafanya watu kuendelea kunyonywa bila ya kujua,eti leo ukapange foleni kwa kuwa umekatika mguu na mwengine akaje ya kuwa jana alikuwa akichezea mtoto kwenye vumbi basi mafua yamemshika sana anaomba kupita,kwa maana ana ahadi  na daktari.
 
 
Kali chache kuliko chungu,maana chungu hazina utamu kama ukali wa uchungu,ikiwa inatakiwa kutizamia mbele siyo kwa kuwa ndiyo unapoelekea,kwani hapo yapasa kutazamia namna ya mwelekeo.ufalme umetawala kwa kila asiye mfalme maana kwa kwenda na nyakati imeonekana ni kheri kuhifadhi kuliko kuweka kwani zikijaa mfalme anaweza kuziihitaji kwa kauli inayosemeka kama amri.
 
 
Pengine leo ikakupase uone ufalme wako,leo ukajifanye ni mfalme wa mambo yako kwani ikiwa tangia uwe mtoa huduma hujafikiri kuunyofoa ufalme,kuondoa lile lililo na uhakika wa kukaa milele kwa vile litajirudia tena,kwa nafasi za ufalme zilizotengwa imeonekana wazi unatembea katika reli isiyokuwa kama tazara..maana unawezajishirikisha kwa kujiona Mfalme bila kujua namna gani ya kuweza kuunyofoa,si mbaya kwa usiye jua kujifanya unajua,maana ndiyo nguvu ya mfalme Juha.

KICHWANI...

Kichwa kinajaa mengi kutokana na namna ya mtu unavyokuwa,ukiwa umelala kubali kuota ndoto maana ndiyo sehemu yake,unaweza kuota mchana kuwa usiku,hapa ni pale unapoiamini ndoto ya uwongo kuwa ya kweli,yaani ni sawa na kulazimisha kuvaa nguo ya mtoto ya jinsia tofauti,sijui ikichanika labda italeta maana,maana wengine huwa kazini wakifanya yao,pengine ukiwa kazini ukifanya yako,yakajaa pengine ya kuwa hakuna sehemu ya hifadhi basi yakabaki katika hifadhi ya kuingia na kutoka.
 
 
Hapa mawazo yanaweza kuongezeka zaidi,maana unaweza kuona kile ambacho hujawai kukiona na kukuta kwamba ni kweli ilipasa kukiona,maana ukiwa hujakiona basi utakiona,hapo ni sawa na mtoto kabla ya ukubwa,ni sawa na mzazi kabla ya uzazi,maana vyote vinapotokea hutokea si katika namna ya kuumizana,bali katika namna ambayo kichwa kinaweza kuyafikiria,kichwa hufikiri kutokana na mtu mwenyewe na wala siyo kitu,maana inaweza kutokea hatari ya kukimbia na kila mtu akakimbia kivyake,hapo kila mtu akiwa ameyajaza yake katika kichwa chake.maana ya mbio kujulikana ni tofauti.mtu hufahamu ukweli wa kitu kwa vile anavyofahamu yeye.
 
 
Hakuna maigizo yanayoweza kuja bila kutoka kichwani,haimaanishi kuigiza kwa vile tunavyofikiria kwa kuanza kutafuta vile vya kweli,ukiwa na imani ya kuona utaona maana kuna walioona lakini hawakuweza kuona,hivyo nikiwa na maana ya nafsi na kichwa cha mtu mwenyewe alivyokijaza,ukijaza mchanga kichwani lazima utakuta umesambazwa na machozi,maana unapofika wakati wa mlima na hata pale wakati wa mteremko,kukiwa na mengi sana mengine hayapaswi kufikirika ikiwa siyo chaguzi lako.
 
 

RADHI...

 
Ikiwa kwa yote yaliyopo, yaliyotokea,yalivyo ama kwa vile tu mtu unavyoweza kumfahamu mwenzako,kwa namna ya kusema na kumjua,ntaomba radhi pale ntakapoyakosea maisha yangu,sifa za kidunia ni jambo jema sana ya kuwa pengine umekuja kwa sababu iliyojengeka na hiyo,ntaomba radhi kwa wachache watakao soma na bila kuelewa kwa sababu kuna wale walioelewa,pengine hakuna maana ya kuelewa tofauti kama hujaelewa hapa ntaomba radhi tena kwa kuwa umeelewa tofauti,
 
 
Raha nyinngine jipe mwenyewe,makosa mengine tatua mwenyewe,wanadamu hawana dogo maana hata ikiwa katika usafiri kuna kubanana na kukanyagana wao watataka radhi,hapa pengine ukiwa na majibu yako kwa kuwa haukuomba radhi mapema na si kwamba ulikosea,bali ni katika namna ya utofauti,kwani unaweza kwenda polini kumkamata simba ili kumfuga naye akakudhuru tena bila radhi kwa sababu ameelewa tofauti nini maana ya adui,radhi si kwa ajili ya kujeruhi tu,hata kwa kuona kwamba imetokea,hapo ukihusisha muda pekee.
 
 
Muda mwingine ni wazi machache hayastahiri kutokea,dunia imeumbika kwa kusema yote ni mazuri na ilikuwa hakuna haja ya kuomba radhi kwa kuwa mti mzuri hutoa matunda mazuri pengine uwe tasa.na kama kuna utasa basi itapasa kuomba radhi kwa kutokufahamika,zaidi maisha yaendelee kwa kuwa kuna mengi ya baadhi ambayo yanaweza kukuletea hadhi.

MBADALA....

Hapa nikiwa nataka mabadiliko,yaliyo katika mazungumzo ama yakabadilika yenyewe kutokana na mfumo wa kubadilisha badilisha unavyoleta mabadiliko,pengine nikiwa sitaki kutoka kwa kuwa kuna mbadala basi ikaje zamu yangu nikaamua kutoka kwa kuwa ilitakiwa kubadilika,kubadilishana maana kukiwa kuna kitu kilishikiliwa,unaweza  unayoyafanya yakawa siyo yale yanayofanyika,hapo mambo yatabadilika kwa matokea halisia.
 
 
Wengi wao wengine hao hufikiri kile cha mtu ndiyo chao,hapo wakifanya mbadala,maana kuna kuwa na mbadala wa kufikiri katika kile kizuri ama kibaya ikiwa vyote ni vitu lakini kukawa na mbadala wa mawazo katika kujua kile ni kizuri ama ni kibaya,pengine ikawa ni kizuri kile kilichosememwa ni kibaya,hapo  ni baada ya kizuri kufanya mbadala na kibaya,pengine endapo  mazingira yamesema.na hapo kunakuwa na mbadala zaidi kwa pale utakapotaka kusema mwenyewe ikiwa tayari mazingira yalishasema..
 
 
Kesho isingeweza kuja bila kubadilishana na siku njema ya leo,hapa ukisema bora kesho maana ya kutokuielewa leo,ama ukaielewa kwa kubadilishana na fikra za kutokuelewa,hapa ukiwa umefanya mbadala wa fikra na zaidi ikatokea katika matendo,kwani mwanzo ilisemwa kwa kuwapo na jambo Fulani,na ukiona mwisho umekuja jua lazima kuna mabadiliko,hayo yakiwa kama siyo kimatendo basi ni namna ya muda ulivyotumika.

UNAPOZUNGUMZA…

 
Wakati na muda unavyokwenda…kwa kuongea mazuri ama  vile ukaja muda ikatulazimu kufanya,ikiwa mwengine akilalama kwa kuzungumza sana akiwa na maana ya kuchoka ya kuwa amezidisha,ukiwa hauhitaji kuongea sana zaidi ya jambo kutendeka,hapa wachache wakikuangalia kama umeweza ama ulikuwa umezungumza tu,hapa wachache watakushangilia ya kuwa umetenda kweli,licha ya kuweza kutokana na baadhi ya nafsi kushindwa kutimiza malengo waliyonayo,na hiyo siyo kwamba wamekuwa wakisema sema bila kufanya,pengine yapasa kufahamu cha kufanya kabla ya kuzungumza.
 
Mara nyingine itakuja kipindi hata yale yasiyo kuwa na maana kwa mtu mmoja kutendeka kwa kuwa mtu  aliyezungumzia ni wa maana,bila kufikiri unaweza kulamba kalata dume,pengine hata ukiwa na mapenzi na hilo dume kwa kuwa na uzalishaji lakini kuna nyingine hufanyika kwa kuwa wachache walishafikiria mwanzo,tena tofauti si kama ilivyozoeleka,hakatazwi mtu kusema bata ni kuku,maana hapo inahitajika sababu,ikiwa kuna wale watakao pata kuwa bata ni kuku na wapo watakao kosa ya kuwa kweli bata si kuku.tunahitaji mazungumzo mazuri.
 
 
Hii imekuwa kama chaguzi maana kuna wengine hutumia kuzungumza wakiwa hawana ya kutenda,kama vifaa hakuna yapasa kuomba kwa jirani akiwa hana kazi navyo,maana baadaye anaweza kusema kwanini hukusema mwanzo,bila kudhani kama mwisho wake ndiyo umefika au ni mwanzo wenyewe maana kuna kuchelewa,,leo unahitaji kusema maana pengine hata ya moyoni yatatoka ikiwa yana milango yake,unapozungumza jaribu kuuweka kuwa ni moyo umezungumza .maana japo tutasubiri kwa kauli ya upendo utakaposema kusubiri.

Monday, October 8, 2012

PESA..


Nikisema iilkuwa wakati wa matumizi nitadanganya umma,ila kama sikuweza kusikia basi kushuhudia baadhi ya matukio ya kipindi icho,vijana wa kisasa wanasema wanakumbuka enzi zao,enzi ni nyuma na ujenzi,maana inawezekana enzi zikawa ni nzuri kuliko ujenzi,unaweza kujenga kile usichikitegemea na bila kujua utachanganyikiwa kwa kuporomoka hadi kujikuta huna maana kabisa..kile kinachopoteza hata thamani ya kukopeshwa hicho kitabaki na maana pekee,pengine ikiwa wanaotumia hawana maana pia,bora kuwa hauna maana kuliko kufanyishwa hauna maana.

Wengine watasema naleta vita kwani wao wameshazoea kama miaka ile ya 75,unajua ili kubadilisha namna ya kukaa ni kumweka adui pembeni,dawa ya adui hakuna asiyeijua kama siyo aibu za kuoneana rangi,ikiwa moja imependeza na nyingine imeiva,zote nzuri tuangalie wasije badilisha mpaka zikawa sita maana kila kijiji itabidi kitumie pesa zake,tena  karatasi za kuingilia na kutoka’ zikae sawa maana mda si mrefu adui anaiporomosha thamani.

Nimebaki na maswali mawili matatu yanayonishusha thamani,pengine kujumlisha ni kutoa,maana ikiwa kukuwa kwa mgomba ni kukomaa lazima tuangalie na virutubisho,unaweza kukua mwili tu..leo ukajibadilisha rangi hii,kesho ukaona upendeze na nani na fulani…yote yako hayo,kama unazo zaidi ya moja zenye thamani moja mpe hata wa jirani ya mbali ya nchi nyingine pengine zinaweza kupanda thamani zikiwa huko maana nabii hasifiki kwao.

USWAHILINI KUNA VITUKO


Nashangaa sana kuona watu wakiangaika na katiba ikifika muda wa kenda miaka sasa,nashindwa kuelewa nilichosomea ni nini maana ni wazi siwezi kuandika katiba,hapa lazima nikuulize kijana mwenzangu ikiwa ni utani kwa mzee akimwambia kijana mwenzangu..sikuweza kufikiri wala kujua endapo piki piki hizi za wachina zinavyotenegenezwa kwa wingi na kuingia kama karanga,ushuru bure kama unapeleka kule,leo ije waseme hakuna spea,hizo zikiaribika ndiyo mwisho wa safari yake ya maisha,wakisahau jamani hizi pikipiki ndiyo zinazotuendesha,wakisahau yaliyo katika katiba ndiyo yanayotuendesha,tena siyo kibinafsi.
.
Tumezoea kuendesha bila kujua kama tunaendeshwa,kama swala ni kukubariana basi liwekeni kwa wananchi watamtafuta aliyeitunga ya kwanza,maana nashangaa kila siku kubishana,yaani kama ulikuwa unaishia vizuri,sasa unang’ang’ania kuishi vibaya,wewe kijana angalia usije kufa umri si wako,wazee mnayafahamu haya ila hampaswi kuitwa wapumbavu.usitegemee kufa kwani ni bahati mbaya,kama unauwezo amka kesho nenda kajikwae  barabarani,na wala siyo lazima iwe kwa  wote,

Nina imani ya kuwa na wengi walio soma na wasijue wamesoma nini,hili ni kosa la kutokuambiwa kama ubongo hautanuliwi na ulimi,ni namna ya kuuweka makini,ili kesho-kesho kutwa isije ikaja usiamini.unawezashindwa kuelewa ni kwanini yale maneno yamekutazamia wewe,maana hata kama ni mimi lakini ni namna unavyoichukulia wewe,huu ni uswahili na haina kustaajabu yaliyo na vituko uswahilini.

UANADAMU UTATA..

Naomba samahani kwanza kwani kwa hili tendo nilijua kwanza,kama hujui kwanini unaishi,ulipo  na ulivyo utakuwa ni mpumbavu anayepaswa kuishi na wapumbavu,maana inaweza kuwa ni wa milele,kama hujui upo duniani kwa ajili ya nini? embu jiulize sasa,kaa chini fikiria na muulize hata mwenzako,ndiyo inawezekana kufanya kile ambacho hakipo katika mategemeo yako lakini ikawa kipo katika njia ya kuendea kwako,fikiri mara ya tatu na kujilaumu kwa kufanya na kuona umekosea,

Namna ya matendo na jinsi ulivyo ndiyo yanafanya maisha yako,kumbuka kipindi unapewa mitihani kama ulikuwa unafanyiwa na mwenzako,maana sasa shida ndiyo mitihani yako,jirani yako ndiyo Yule aliyekuwa akikusaidia hata kwa chumvi inapokata mida ya giza’.pengine wengine hawaelewi kwa kuwa na kuishi kivingine,kama sijakosea mwanadamu lazima aishi maisha yake halisia,hasa pale anapokuwa mtu mzima,watoto huwa wanachukulika hawana makosa kwa kuwa kwao wao ni vigeni,hata hawapaswi kukaa sebureni.

Mwanadamu anastahiri upendo,mwanadamu anastahiri namna ya kujiona mtu katika dunia,maana umekuja kwa ajili hiyo,unapoambiwa mbaya shukuru mungu maana wazuri mungu kawanyima ubaya,kubari kuwa yangu ni kama yako,na kama huja baada ya kuona muda unaobidi kutumika ni ule ule lakini kinachobidi kutendwa kimetofautiana,mwanadamu tafuta ridhki yako ujione mfalme,ukiona mwenzako anamsema mwenzako angalia isije kuwa ni kawaida yako,fanya mambo yako…

JIULIZE...


Unaposhindwa kabisa ama kuweza pia ni kheri ukajiuliza,jiulize kama ni kweli unahitaji mafanikio ambayo yatakukidhi,ukiwa na akili timamu,ukiwa na akili zako unazozifahamu,isieleweke kuzingulika kwani mwisho wa siku utajizingua mwenyewe,usiwe na haraka ya vitu usivyovifahamu,usiwe na  haja ya kutaka pasipo kufahamu,ikiwa kwako jiulize kama ipo kama kwangu,yako ni yako lakini ni katika usawa wa matendo,wacha niseme hivi ilivyo ikiwa katika kuelewa.

Angalia usije ukapotea maana na njia zimekuwa ni nyingi sana,anafatia na maswali ya kujiuliza unaweza kwama na kuoneka ulitungwa hadi  swali sijui jibu atakuwa nalo nani..kwani ingelikuwa ni kiulizo basi ni lazima ungenijibu wewe,mara nyingine gadhabu hutumika kwa kuona maswali magumu yakikusonga,mara nyingine maswali huwa marahisi ikawa unayefanya magumu jiulize mepesi yapi?maana swali la mtihani jepesi si ya kuwa umelipatia maksi..

Nilijiuliza nikasema sina haja ya kuuongelea mtihani labda iwe katika chumba chake,nikajiuliza yajana niliyoyaweza leo kumbe ni  mepesi,ndiyo maana nikawa najiuliza sana kuhusiana na siku ya kesho.utu uzima unamajina zaidi ya pesa ilivyo,maana mwanadamu haendani na fashion ingawa anaitengeneza mwenyewe,jiulize  kama shavu lako la kushoto liko sawa na la kulia,ili utakapopigwa hata la kulia ukageuzia na kushoto.

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO : Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha...