Ridhika katika kufanya maisha yako yawe unavyotaka,maana
nikasema mazuri pengine ndiyo mabaya kwa kulinganisha na yale mazuri ya wengine,maisha
hayajawa mpira mpaka ikaja kuyapiga ikiwa kama dana dana,shida yapasa mtu
kuzipata peke yako,ridhiki ikiwa yako haina unyang’anyi kwani kwa kile
ulichokiandaa ndiyo hicho kitapendezea kulika,kuweka mezani chakula si kwamba ule
hadi meza,maana njaa lazima itakuja,ikiwa kama ni ridhiki lazima chakula
kitaandalika tena na endapo itakutwa meza haipo itastahiri kulika mpaka sahani
zenyewe.
Maisha hayajawa mchanga mpaka yakafika namna ya kuchanganya
watu pasipo kuelewa nini cha kufanya,wengi wakiwa wanatafuta ridhiki wakiamini
pesa ndiyo tatizo la kulitatua tatizo husika pekee,ukiamini endapo ukiwa una
pesa yote yanaweza kurudi mwanzo,ikiwa ni njaa,sahani Pamoja na meza yenyewe.maana
unaweza kutokudhani baadaye kwa kutokujua unataka nini.ridhiki yako ikawa kama
ni mnyororo uliojifunga maana hakuna wa kumuuliza nani aliyefunga.
Ridhiki haiokotwi bali inatafutwa,yakiwa saba bora kuchagua
lile la mwisho maana usije kuridhika na moja wakati haba lipo,haipaswi kuchukia
na hoja moja wakati ya wengine yanaonekana kama vioja,yaweza kuwa yako,unaweza kuwa
wewe.ridhiki haimfuati mtu,ridhiki haichagui kabila wala mahala,ridhiki huenda
pale kwake kuliko na usahihi,mwanadamu anapaswa kuwa makini ili kuelewa popote
yake,ikiwa kama mdomo umekosa ridhiki kwa kula basi hata pua zitanusa,pengine masikio
yakasikia lile lililosemeka na vingine vikawa vile vilivyoungika.
NENDA UKIJIAMINI
KATIKA MWELEKEO WA NDOTO ZAKO..ISHI MAISHA YALE ULIYOKUWA/UNAYO YAFIKIRIA.